Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
Majira ya Saa 1:00 Usiku kwa Masaa ya Afrika ya Mashariki,Mnyama mkubwa mwituni, Simba SC watashuka dimbani katika dimba la Benjamin Mkapa kuwakaribisha wana alizeti Singida Big Stars.
Mechi inategemewa kuwa ngumu, maana katika mchezo wa kwanza pale Liti, Singida, timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya 1-1.
Simba itashuka dimbani ikiwategemea wachezaji wake mahiri kama Chama, Saido, na wengineo huku Singida Big Stars ikiwategemea zaidi akina Bruno, Kazadi na mastaa wengneo.
Je, Simba ataweza kuzoa alama zote tatu? Au Singida ndio atakayeibuka kidedea? Tukutane saa 1:00 usiku kwa live updates...
Ubashiri wangu: Simba 2-1 Singida