FT: Ufaransa 3-0 Iraq | World Cup 2026 | Lincoln Financial Field | Juni 23, 2026| Mbappe anaendelea kukiwasha

FT: Ufaransa 3-0 Iraq | World Cup 2026 | Lincoln Financial Field | Juni 23, 2026| Mbappe anaendelea kukiwasha

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kombe la Dunia linaendelea tena leo ambapo Ufaransa watakuwa uwanjani dhidi ya Iraq

Naamini chama langu France litamkana sana mpenda vita Iraq

Soma Pia: FT: Ufaransa 3-1 Senegal | World Cup 2026 | MetLife Stadium | 16 Juni, 2026

Ingawa walionyesha kiwango kisichoridhisha katika kipindi cha kwanza dhidi ya Senegal kwenye mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Dunia, Ufaransa walizinduka na hatimaye kushinda mabao 3-1, na hivyo kufanikiwa kufungua mashindano makubwa kwa ushindi kwa mara ya saba mfululizo
======
Hadi sasa timu hazijarejea uwanjani. Ni kutokana na mvua inayoendelea katika dimba la Philadelphia.

Mchezo umeendelea huku Ufaransa ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0, ambapo mshambuliaji wake nyota, Kylian Mbappé, ameendeleza ubora wake kwa kufunga katika mchezo wa pili mfululizo.

Ushindi huo unaifanya Ufaransa kufuzu rasmi hatua ya 16 bora na kuendelea kujiimarisha kama moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa kwenye Kombe la Dunia 2026.
 
Back
Top Bottom