FT: Wydad Casablanca 1-0 (Penati 4-3) Simba S.C | CAF Champions League | Simba yaondolewa kwa mikwaju ya penati

FT: Wydad Casablanca 1-0 (Penati 4-3) Simba S.C | CAF Champions League | Simba yaondolewa kwa mikwaju ya penati

mwarabu feki

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2023
Posts
811
Reaction score
1,811
Wanathiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiimbaaaaaaa[emoji350][emoji350]
Hayawi hayawi Sasa yamekuwa, Ile siku iliyosubiliwa Kwa hamu na waarabu wote hatimaye imefika..
Ni siku ya hukumu kwa mnyama Simba
Ni siku ambayo taifa la Tanzania linaenda kupata aibu kwa kipigo kizito watakachoenda kushushiwa Simba na waarabu wa Morocco.

Mwana kulitafuta mwana kulipewa, mtoto akililia wembe mwache umkate,
wameingia cha kike eeh waaah!!!

Kuwa nami mwarabu feki upate kile kitakachojiri pale katika Dimba la Mohamed V (machinjioni) Jijini Casablanca...

Mechi hii ya kukata na shoka itaanza majira ya saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika mashariki na itarushwa na Azam Sports kupitia Channel ya ZBC2

Kaa nami mwanzo Mwisho......

Rest in peace Simba[emoji3545]
Fu0eN9_WwBMcbgb.jpg

Timu zote tayari zimeshaingia uwanjani kupasha misuli tayari Kwa mpambano huu wa Leo [emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]

00" Mpira umeanza hapa katika uwanja wa Mohamed V Wydad ndio wamekuwa wa kwanza kugusa Mpira ule

03" Wydad wameanza kusaka bao la mapema

06" Simba wanapata kona ya kwanza ya mchezo ila haikuzaa bao

13" Milango bado migumu kwa pande zote mbili

20" mashambulizi yanaongezeka kuelekea lango la Simba, ila golikipa Ally Salum anakaa vema na kuondoa hatari ile

24" Goooooooo Wydad wanapata goli la kwanza

30" Simba inapataa faulo eneo zuri lakini mpira unaokolewa na kuwa ni wa kurusha kuelekea lango la Simba

45"+1 Imeongezwa Dak 1 ya nyongeza hapa
Mpira ni mapumziko Wydad wanaongoza Kwa goli moja

Kipindi cha pili kimeanza

46" wanaanzisha mashambulizi kupeleka lango la wydad

49" Wydad wanafanya shambukizi Kali lakini mpira unaenda nje

60" mashambulizi ni makali sana langoni mwa Simba ila Bado wameshikilia bomba

90"+4 Zimeongezwa Dak 4, bado Wydad wako mbele Kwa goli 1 kwa bila

Naam mpira umekwisha..

Hatua inayofuata ni mikwaju ya penati kuamua mshindi

Wenyeji wanafanikiwa kusonga mbele kwa penati 4-3 baada ya Shomari Kapombe na Clatous Chama kukosa mikaju yao.

View attachment 2602892View attachment 2602894
 
Jioni moja ya mwaka 2003, jijini Cairo nchini Misri kulikuwa na mechi nzito, uwanja ukiwa umetapika kulikuwa na shujaa mmoja aliyekuwa golini akiibeba timu yake ya Simba Sc kwa kupangua mikwaju ya penati na kuivua taji mabingwa watetezi Zamalek. Shujaa huyo si mwingine ni Juma Kaseja. Dunia ikabaki imeduwaa.

Leo 28.04.2023 miaka 20 baadae, Simba ipo tena uarabuni kucheza na bingwa mtetezi ambaye ni Wydad, katika mazingira yaleyale.

Simba atashuka akiwa na mtaji wa goli 1-0 katika mchezo wa kwanza, uliopigwa Tanzania. Je historia kujirudia? Simba ataweza kuivua Wydad ubingwa akiwa kwao kama ilivyokuwa miaka 20 iliyopita pale Zamalek. Sababu wanayo, uwezo wanao nia pia wanayo.

Ni mechi ya kufa au kupona, ewe Mwana Simba uliyepo Ndola, Tanga, Entebbe, Nakuru na maeneo mengine tembea kifua mbele, usiwe mnyonge kwa Simba hii mwarabu atakufa kwao. Je Shujaa atakuwa nani? Baleke, Chama, Inonga au Kiungo punda Mzamiru?

Mechi itakuwa mubashara kuanzia Saa 4:00 Usiku kwa Masaa ya Afrika Mashariki na mchezo utakuwa live kupitia ZBC 2 ya AzamTv, Chaneli 225 ya DStv, Canal Plus na Bein Sports.
D6146EEA-3ED0-492D-8985-4A66873C8369.jpeg
 
Back
Top Bottom