FT: Yanga 1-1 Al Hilal Club (CAF Champion League) | Mkapa Stadium | 8-10-2022

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
FULL TIME
90' Zinaongezwa dakika 4
89' Wageni wanafanya shambulizi kali lakini Diarra anaokoa
80' Kasi ya mchezo inazidi kuongezeka, Yanga wanaendeleza kasi kutafuta goli la pili
75' Shuti la Mayele linagonga nguzo na kurejea uwanjani
73' Al Hilal wanafanya shambulizi kali, inakuwa kona, ya tatu kwa AL Hilal
72' Yanga wanapata kona ya 11, anapiga Aziz Ki inaokolewa
70' Al Hilal wanafanya shambulizi kali, mpira unatoka nje
Abdulrahman Yusuph anaisawazishia Al Hilal
67' GOOOOOOOOOOOOOOOO
64' Morrison anachezewa faulo
60' Mayele anakosa nafasi ya wazi baada ya mpira kuwa na kasi
54' Kasi ya mchezo imeongezeka kwa timu zote
Mayele anaipatia Yanga goli la kwanza kwa shuti la nje ya 18
52' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
46' Yanga wameanza kwa kasi
Kipindi cha pili kimeanza

MAPUMZIKO

45' Yanga wanapata kona, Ki anapiga inaokolewa
44' Al Hilal wanaruhusu lango lao kufikiwa mara kwa mara
40' Yanga wanarejesha kasi yao waliyoanza nayo lakini wapinzani wao wapo makini
31' Yanga wanapata kona, anapiga Aziz Ki shambulizi linaokolewa
28' Al Hilal wanapanga mashambulizi taratibu
25' Kasi ya mchezo imebalansi, timu zote zinamiliki mpira kwa zamu
20' Al Hilal wanapata faulo nje ya 18 ya eneo la Yanga
19' Wageni wametulia na sasa wanapiga pasi kadhaa, wamefika langoni mwa Yanga kwa krosi
12' Shambulizi kali langoni mwa Al Hilal Club lakini walinzi wanaokoa
11' Morrison anawatoka walinzi, mpira unambabatiza beki inakuwa kona nyingine
10' Yanga wanapata kona
4' Yanga wanafanya shambulizi la kushtukiza, inakuwa kona, inapigwa haizai matunda
3' Presha ya mchezo ipo juu lakini ni Yanga ndio wanaomiliki mpira muda mwingi
1' Yanga wanafanya shambulizi kupitia kwa Morrison, inakuwa kona

Mchezo umeanza, Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania

Timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza mchezo



Kikosi cha Yanga kuelekea mchezo wa leo Oktoba 8, 2022

================
Wakuu leo ndiyo leo, mtoto hatumwi dukani, ngoma ya mtoto haikeshi, usiku wa deni haukawii kukucha.

Leo majira ya saa 10:00 jioni, katika dimba la Benjamin Mkapa, Yanga watashuka dimbani katika mchezo wao dhidi ya Al Hilal ya Sudan katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Ikumbukwe, katika michezo yao ya awali, Yanga waliwatoa Zalan na Al Hilal wakawatoa St. George ya Ethiopia.

Yanga inafundishwa na Kocha Prof. Nabi huku wapinzani wao wakinolewa na Kocha Ibenge. Iwe jua iwe mvua timu ya Yanga inahitaji ushindi wa kuanzia goli 3 ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.

Mechi itakuwa mubashara kupitia Azam Sports 1HD.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
We mzee shindwa na huu wanga wako.
Kila kitu kinaanzia rohoni ndipo hudhihirika kwenye ulimwengu wa damu na nyama. Yanga walitoe hilo limwenge kwenye nembo yao.
Mwenge pia una laana, umelaanika. Soma Isaya 50:11

Isaya 50:11
[11]Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
Behold, all ye that kindle a fire, that compass yourselves about with sparks: walk in the light of your fire, and in the sparks that ye have kindled. This shall ye have of mine hand; ye shall lie down in sorrow.
 
LILEPO HAT TRICK [emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Roho ya Chuki na ya Kishetani itoke Kwa Jina la Yesu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mimi naipenda sana Yanga. Mshana Jr, GENTAMYCINE na wanazi wengine wa Simba hapa jukwaani wanalijua hilo.

Ila kwenye ukweli lazima tuse.

Isaya 50:11
[11]Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
Behold, all ye that kindle a fire, that compass yourselves about with sparks: walk in the light of your fire, and in the sparks that ye have kindled. This shall ye have of mine hand; ye shall lie down in sorrow.
 
Huwezi kuipenda Yanga then ukaiomba ifungwe. Hii ni roho ya Kinafiki na Kishetani

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
KILA LA KHERI Chama La Wana Yanga.
.
Morrison kule Kisinda huku alafu Mayele paleeee Azizi Ki na FeiToto hapo katikati halafu nyuma yao Aucho halafu Wizara ya Ulinzi ni Bangala na Job halafu tena kwenye mabawa ni Kibwana Shomari na Sodaaa ya Bembaa.
.
ALOOOOHHH!!! Golini akae hata JUMA MGUNDA HAWATOKIIIIIII!!!!!!!![emoji2][emoji2][emoji2]
.
Kwanini leo Asubuhi tusianzie Bunju tuwapime kwanza umri [emoji881] ndio badae kipigwe?[emoji2955]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…