Wana Yanga eeh nilikuwa na nyinyi katika kipindi kirefu kabla ya kuifikia siku hii ya leo.
Nimewapa support na kuwashangilia (kasoro tu kuwaombea kwasababu siamini kwenye mambo hayo)
Al Hilal ni timu kubwa na ngumu kiupinzani tofauti na Zalan, matokeo haya ya leo kufikiria kuwa mkiwa ugenini mtapindua meza ni probability ngumu sana.
Hongereni kwa perfomance yenu uwanjani bado mna nafasi (japo kihalisia ni ndogo)
Naomba niishie hapa na kwa sasa comment zinazofata baada ya hapa naomba msizizingatie maana ni utani tu.