FT: Yanga 2-2 Azam FC | NBC PL | Uwanja wa Benjamin Mkapa | 06/09/2022

FT: Yanga 2-2 Azam FC | NBC PL | Uwanja wa Benjamin Mkapa | 06/09/2022

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Majira ya saa 1:00 usiku, mabingwa watetezi wa taji, Yanga SC watashuka dimbani kumenyana na Azam Fc katika muendelezo wa ligi kuu ya NBC.

Yanga itashuka dimbani kutafuta alama 3 huku Azam Fc nayo ikijaribu kutafuta alama 3 huku ikiwa haina kocha mkuu.

Mechi inategemewa kuwa ngumu na ushindani, tukutane hap kwa live updates.

Mchezo unaendelea, Azam FC imekuwa ikitanguli mara zote kisha Yanga inarejesha mashambulizi, mabao ya Azm FC yamefungwa na Daniel Amoah dakika ya 25 na Malickou Ndoye dakika ya 65.

Mabao ya Yanga yote yamefungwa na ni Feisal Toto katika dakika ya 57 na 77.

Mashambulizi ni makali, hakuna timu ambayo inakaa nyuma, kila upande unapanda kushambulia unapopata nafasi hiyo.

Zimeongezwa Dakika 3

Mchezo umemalizika kwa matokeo ya 2-2.
 
The Citizens first eleven
IMG-20220906-WA0027.jpg
 
Leo nataka nithibitishe usemi wa wana Yanga wengi kuwa Yanga ni kubwa kuliko TFF na sheria zake

Nikumuona Tuisila Kisinda kwenye line up kweli nitathibitisha kuwa Yanga ni Club kubwa na haiyumbishwi na TFF
 
We mandonga Yanga anashinda 2:1
Yanga ana asilimia nyingi za mushinda kutokana na chemistry walionayo

Tofauti na Azam ambauo bafo inataguta muunganiko tena katika nyakati ambazo kocha ni mgeni na hii ni mechi yake ya kwanza

Kwa mchezaji mmoja mmoka Azam nawaona wako bora kuliko yanga
 
Leo nataka nithibitishe usemi wa wana Yanga wengi kuwa Yanga ni kubwa kuliko TFF na sheria zake

Nikumuona Tuisila Kisinda kwenye line up kweli nitathibitisha kuwa Yanga ni Club kubwa na haiyumbishwi na TFF
Una hamisha magoli nmekuuliza issue ya kocha wenu kuwapa taraka imefunika mechi ya ya leo nyie mmefaidika nini?
 
Pale ramli za ulozi zinapoletwa kwenye mpira.Mkuu mpira ni uwezo siyo ramli.

Kwa mjibu wa vikosi vya timu zote mbili Yanga sc inashida dhidi ya Azam fc.

●Nisamehe kwa kuingilia ramli yako.
Nadhani mwamuzi ni dakika 90..hebu tuupe muda wakati
 
Una hamisha magoli nmekuuliza issue ya kocha wenu kuwapa taraka imefunika mechi ya ya leo nyie mmefaidika nini?
Hilo nililiacha nikijua utajiongeza, hujui kuhusu promo na kiasi gani inaweza kuwasaidia nyinyi katika mapato hususani katika game ambayo nyinyi mko nyumbani?

Huelewi kwanini Manara aliwahi kumlalamikia Ahmedy Ally kusema kwenye derby ya Yanga na Simba amekuwa mbinafsi hakuwahi kuiongelea kwenye media?
 
Leo ni siku mbaya sana Kwa Wananchi maana rekodi ya unbeaten inaenda kuvunjwa na wanalambalamba
 
Hilo nililiacha nikijua utajiongeza, hujui kuhusu promo na kiasi gani inaweza kuwasaidia nyinyi katika mapato hususani katika game ambayo nyinyi mko nyumbani?

Huelewi kwanini Manara aliwahi kumlalamikia Ahmedy Ally kusema kwenye derby ya Yanga na Simba amekuwa mbinafsi hakuwahi kuiongelea kwenye media?
Una akili ila unazitumia vibaya football sio mziki kwamba unategemea Kiki, au huyu akitoa single inafunika ya mwingine football ina mashabiki hawaendi na trend
 
Una akili ila unazitumia vibaya football sio mziki kwamba unategemea Kiki, au huyu akitoa single inafunika ya mwingine football ina mashabiki hawaendi na trend
Kama promo umeamua kuipa jina la trend basi tuna safari ndefu kwenye soka letu
 
Back
Top Bottom