FT: Yanga S.C 2-0 As Real Bamako | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium | 08.03.2023

mzee wa bwaksi

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
2,255
Reaction score
3,972
Mabingwa wa kutandaza soka tamu, soka la kuvutia, soka la kumtoa nyoka pangoni, soka ice cream, soka lenye viwango vya Dunia, hapa nawazungumzia Young Africans leo mida ya saa 1.00 usiku watashuka pale dimba la Benjamini Mkapa kutafuta alama tatu zingine ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuingia robo fainali ya michuano ya shirikisho barani Afrika.

Ikumbukwe kuwa mchezo wa awali uliopigwa huko nchini Mali timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana 1-1 hivyo mchezo wa leo utakuwa mkali kwa timu zote.

Timu zote zimeshaingia kiwanjani na kinachosubiriwa ni kipyenga cha mwamuzi ili kuashiria kuanza kwa mchezo huu

”"""""'"""''''''''''''''''"""""""""""'''''''''''''''''''''''''


00" Mpira umeanza As Real Bamako ndio wameanza kukanyaga gozi la ng'ombe

07" Gooooal..... Fiston Mayele anapachika goli la kwanza Kwa Yanga..
Ni shangwe hapa Benjamini Mkapa Wananchi wamenza Kwa Kasi kubwa

20" Yanga bado wanaongoza bao Moja Kwa bila huku wakitandaza mpira safi mpira mtamu kama asali..

40" Mabadiliko Kwa Yanga ameumia Tuisila Kisinda ametoka kaingia Jesus Moloko

45+3" Dakika 3 za nyongeza kuelekea mapumziko.. bado matoke Yanga inaongoza kwa goli moja
Naam ni mapumziko wachezaji wa timu zote mbili wanaelekea vyumbani kupata mawaidha ya walimu wao.

Tukutane kipindi cha pili
49' Mchezo hauna kasi

55' Yanga wanafanya mashambulizi
Bangala anakosa penati

68' Gooooooooooooooooo
Moloko anaipatia Yanga goli la pili baada ya beki wa Bamako kujichanganya

90" Zimeongezwa Dak 4, Yanga bado ipo mbele Kwa goli 2-0
Naaam mpira umekwisha kwa Young Africans kuibuka na ushindi wa magoli mawili Kwa bila hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuingia robo fainali.
Hadi wakati mwingine... Tchaoooo
 

Attachments

  • Screenshot_20230308_155049_Instagram.jpg
    90.5 KB · Views: 6
  • YANGA YAICHAKAZA BAMAKO 2-0, YACHUNGULIA ROBO FAINALI.jpg
    529.5 KB · Views: 5
Mmeroga au mnaenda kichwa kichwa?

Mnakumbuka alichofanywa Simba Lunyasi dhidi ya Raja

Mimi sio Yanga wala Simba ila kuna mganga huku anaitwa mkoma koma Mmavimavi anajua sana dawa ya kutofungwa mchezaji aikifika golini anaona ugali na maharage tu na sio goli
 
Chonde chonde , wakae na Mayele, wamshauri, wapinzani Sasa wanaojua stail yake ya uchezaji. Asilazimishe afunge yeye tu ili ateteme, atumie nafasi za mwanzo kutoa assist baada ya timu kushindwa angalau goli 3 , basi aanze kulazimisha kufunga. Pamoja na kuwa anafunga magoli ila anapotezea nafasi nyingi Sana za wazi ambapo Kuna mtu yupo kwenye nafasi nzuri zaidi na anamwona lakini hampi mpira ,analazimisha kupiga Mpira ama unakuwa blocked au unatoka nje.

Wachezaji wamwelewe Ki Aziz kuwa anatoa pasi za haraka na mpenyezo ,ukimpa pasi wahi mbele sio kuzubaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…