FT: Yanga SC 1-1 Simba SC | Ligi Kuu NBC '22/'23 | Benjamin Mkapa Stadium

FT: Yanga SC 1-1 Simba SC | Ligi Kuu NBC '22/'23 | Benjamin Mkapa Stadium

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
52,812
Reaction score
71,392
01' Kipute kinapulizwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

01' Simba wanakuwa wakwanza kulifikia lango la Yanga, pasi ya mwisho inakosa tija.

03' Simba wanapata faida ya faul ya kwanza baada ya Okrah kuangushwa.

04' Onyango anashindwa kuufikia mkwaju wa adhabu ndogo kutoka kwa Chama.

06' Simba wanacheza kuelekea lango la Yanga lakini hesabu zao zinashindwa kukaa sawa.

11' Yanga wanafanya shambuli la pili linalolenga lango, shuti la Kisinda linapanguliwa na Aishi Manula.

13' Kisinda anawekwa chini na Zimbwe Jr, faulo kueleka Yanga.

14' Aziz Ki anaachia mkwaju wa unaoishia kwenye mikono ya Aishi Manula.

14' [emoji460] Okraaaaaaa, pasi maridadi kutoka kwa Chama inamaliziwa na Okra. Ni counter iliyoanzia kwa Aishi Manula baada ya kudaka mpira wa Aziz Ki. Shot on target ya kwanza kwa Simba inazaa goli.

15' 🟡 Okra anapewa kadi ya njano kwa kuvua jersey wakati akishangilia bao lake.

20' Zimwe anautoa mpira uliokuwa unamuelekea Kisinda na kuzaa kona.

21' 🟡Mkude yuko chini, nahodha Feisal Salum anapewa kadi ya njano kwa kumchezea ovyo Mkude wakati hana mpira.

22' Okra yuko chini baada ya kudondoshwa na Djuma Shaaban.

26' 🟡 Mzamiru anapewa kadi ya njano kwa kucheza ndivyo sivyo.

37' Simba wanatawala mchezo kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Yanga wanausaka mpira bila mafanikio.

40' Chama anadaka mpira katika harakati za kuokoa, faulo inapigwa na Aziz Ki bila kuleta matokeo.

41' Djuma Shaban anambwa kadi ya njano kwa kumchezea ndivyo sivyo Inonga.

42' 🟡 Kadi ya njano kwa Dkt. Aucho baada ya kumshusha chini Okrah akichanja mbuga na mpira wa counter attack

44' Aucho anawekwa chini na Mzamiru karibu kabisa na 18, nyuma ya mpira anakaa Aziz Ki kuchonga faul.

45+1' [emoji460] Aziz Ki unauweka uwanja sawa kwa mkwaju mkali wa adhabu ndogo unaomshinda Aishi Manula, Yanga 1-1 Simba.

45+2' Mpira mapumziko.

======

45' Kabumbu limerejea.

52' Mayele anaruka juu na kupiga mpira wa kichwa, mpira unapaa juu ya lango.

54' Boli linatembea kwa upande wa Yanga kwenye kipindi cha pili.

55' [emoji680] Sakho anaenda benchi na nafasi yake kuchukuliwa na Habib Kyombo.

56' Kyombo anajipeleka chini kwenye boksi, refa anamwambia nyanyuka.

59' Simba wanaingiza mpira kati na Dikson job atibua, kona. Mpira wa kona unaondolewa na Fiston Mayele.

63' Habib Kyombo anaachia mkwaju mkali unaoishia kwenye nyavu za pembeni.

65' Dickson Job ananawa mpira katika harakati za kuokoa, Phiri anapiga mkwaju mkali wa adhabu unaopaa sentimita chache juu ya lango la Yanga.

68' [emoji680] Tuisila Kisinda anaenda bench na nafasi yake kuchukuliwa na Farid Mussa.

68' Okrah anajaribu mwenyewe huku Chama akiwa mwenyewe, goal kick.

70' Phiri anajaribu kuingiza kwenye dimba la Yanga, mabeki wanasimama imara na kuondoa motion.

71' 🟡 Kadi ya njano kwa Aziz Ki ikitimiza nne kwa Yanga na nane kwenye mchezo.

73' Diarra yuko chini akigangwa.

77' Feisal anaachia mkwaju, Manula anadaka na kuachia kiasha anadaka tena.

78' Bigirimana anaingia kuchukua nafasi ya Moloko.

79' Almanusura Mayele ateteme baada ya krosi kumpita Manula lakini anashindwa kuitumia fursa vyema.

83' Kyombo anajaribu na kutengeneza kona bila matokeo.

84' Habib Kyombo anapokea kadi ya 5 ya njano kwa upande wa Simba.

86' Mwenda yuko chi na mpira unasimama.

88' [emoji680] Nyoni anaingia kuchukua nafasi ya Israh Mwenda.

90+3' Mpira unatamatika dimba la Benjamin Mkapa, Yanga 1-1 Simba.

===========
Naaam, wasalam wakuu,

Ile siku maalumu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu hatimaye imefika. Pambano lenye hadhi la watani wa jadi katika soka la bongo, Yanga na Simba.

Karibuni katika matukio mubashara (live updates) ya mtanange huu wa kukata na shoka baina ya mahasimu wa soka la Bongo #KariakooDerby Yanga na Simba, utakaochezwa saa 11 jioni Estadio De Benjamin Mkapa leo jumapili 23-10-2022.

Huu ni mchezo wa namba 64 wa Ligi Kuu ya NBC 2022/2023, Yanga akiwa ni mwenyeji wa mchezo wa leo dhidi ya mtani Simba.

Mchezo uliyopita wa Ligi Kuu msimu wa 2021/2022 uliochezwa April 30, 2022, timu hizi zilitoshana au kuchoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana/suluhu ya 0-0. Kwa maana hiyo huu ni mchezo wa mzunguko wa kwanza kwenye msimu wa 2022/2023.

Timu hizo zinaingia uwanjani zikiwa na alama 13 kila moja, lakini Simba ipo kileleni kutokana na wingi wa mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya Yanga ambayo inashika nafasi ya pili, kila moja amecheza mechi tano.

Pia michezo mingine (Derby) ya hivi karibuni ni ule wa Mei 28, 2022 kwenye nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup ambapo, Simba alifungwa goli moja bila majibu, ambapo shuti kali la Feisal Salum ‘Fei Toto’ liliwalaza na viatu mashabiki wa Simba siku hiyo.

Vilevile mnamo Agosti 13, 2022 kwenye mechi ya ngao ya Hisani, Simba alitepeta tena kwa Yanga kwa kufungwa goli 2 kwa moja. Fiston Mayele "Mzee wa kutetema" akiingia kambani mara mbili siku hiyo na mashabiki wa Simba wakitoka vichwa chini.

Kwa miaka ya karibuni Simba imekuwa ikishindwa kupata ushindi mbele ya Yanga katika michezo ya Ligi Kuu Bara kwani mara yao ya mwisho kushinda ilikuwa bao 1-0, Februari 16, 2019 lililofungwa na mshambuliaji, Meddie Kagere.

Kwenye mechi za kimataifa, tarehe 16/10/2022 Yanga imetolewa kwenye michuano ya CAF CL na Al Hilal baada ya kufungwa 1-0 na kushukia kwenye michuano ya CAF CC ambapo pia amepangiwa Club Africain kwenye mchezo wa Play off kuelekea makundi.

Pia Simba mechi ya mwisho kimataifa imetoka kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Primeiro De Agosto ya Angola na hivyo kufuzu hatua ya makundi ya CAF CL.

Je, leo itakuwaje baina ya miamba hii miwili? Nani ataibuka kidedea? kaa nami hapa mwanzo, kati na mwisho kupata kila kinachojiri kutoka katika dimba hili lenye kumbukumbu nzuri ya Hayati Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Azam Sports 1 HD wataurusha mpambano huu mubashara (live).

Je, "Watatetema" au "watapiga saluti?" Hahaha #𝑯𝒂𝒊𝒏𝒂𝑴𝒃𝒂𝑴𝒃𝒂𝑴𝒃𝐚

𝐕𝐢𝐤𝐨𝐬𝐢 𝐯𝐲𝐚 𝐥𝐞𝐨:

𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐅𝐈𝐑𝐒𝐓 𝐗𝐈
1. 𝐃𝐢𝐚𝐫𝐫𝐚 𝐃𝐣𝐢𝐠𝐮𝐢
2. 𝐃𝐣𝐮𝐦𝐚 𝐒𝐡𝐚𝐛𝐚𝐧
3. 𝐊𝐢𝐛𝐰𝐚𝐧𝐚 𝐒𝐡𝐨𝐦𝐚𝐫𝐢
4. 𝐁𝐚𝐧𝐠𝐚𝐥𝐚 𝐘𝐚𝐧𝐧𝐢𝐜𝐤
5. 𝐉𝐨𝐛 𝐃𝐢𝐜𝐤𝐬𝐨𝐧
6. 𝐀𝐮𝐜𝐡𝐨 𝐊𝐡𝐚𝐥𝐢𝐝
7. 𝐅𝐞𝐢𝐬𝐚𝐥 𝐒𝐚𝐥𝐮𝐦
8. 𝐌𝐨𝐥𝐨𝐤𝐨 𝐉𝐞𝐬𝐮𝐬
9. 𝐌𝐚𝐲𝐞𝐥𝐞 𝐅𝐢𝐬𝐭𝐨𝐧
10. 𝐀𝐳𝐢𝐳 𝐊𝐢
11. 𝐊𝐢𝐬𝐢𝐧𝐝𝐚 𝐓𝐰𝐢𝐬𝐢𝐥𝐚

𝐒𝐮𝐛𝐬: 𝐌𝐬𝐡𝐞𝐫𝐲 𝐀., 𝐌𝐰𝐚𝐦𝐧𝐲𝐞𝐭𝐨 𝐁, 𝐁𝐚𝐜𝐜𝐚 𝐈., 𝐁𝐢𝐠𝐢𝐫𝐢𝐦𝐚𝐧𝐚 𝐆, 𝐌𝐚𝐮𝐲𝐚 𝐙, 𝐅𝐚𝐫𝐢𝐝 𝐌, 𝐀𝐦𝐛𝐮𝐧𝐝𝐨 𝐃, 𝐍𝐤𝐚𝐧𝐞 𝐃, 𝐌𝐚𝐤𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐇.

MFUMO: 4-2-3-1
Kocha: Nasrideen Nabi / Cedric Kaze

𝑺𝑰𝑴𝑩𝑨 𝑭𝑰𝑹𝑺𝑻 𝑿𝑰
1. 𝑴𝒂𝒏𝒖𝒍𝒂 𝐀𝐢𝐬𝐡𝐢
2. 𝑰𝒔𝒓𝒂𝒆𝒍 𝐌𝐰𝐞𝐧𝐝𝐚
3. 𝑯𝒖𝒔𝒔𝒆𝒊𝒏 𝐌𝐨𝐡𝐚𝐦𝐞𝐝
4. 𝑶𝒏𝒚𝒂𝒏𝒈𝒐 𝐉𝐨𝐚𝐬𝐡
5. 𝑯𝒆𝒏𝒐𝒄𝒌 𝐈𝐧𝐨𝐧𝐠𝐚
6. 𝑴𝒌𝒖𝒅𝒆 𝐉𝐨𝐧𝐚𝐬
7. 𝑺𝒂𝒌𝒉𝒐 𝐏𝐚𝐩𝐞
8. 𝑴𝒛𝒂𝒎𝒊𝒓𝒖 𝐘𝐚𝐬𝐢𝐧
9. 𝑷𝒉𝒊𝒓𝒊 𝐌𝐨𝐬𝐞𝐬
10. 𝑪𝒉𝒂𝒎𝒂 𝐂𝐥𝐚𝐨𝐮𝐭𝐮𝐬
11. 𝑶𝒌𝒓𝒂𝒉 𝐀𝐮𝐠𝐮𝐬𝐭𝐢𝐧𝐞

Mfumo : 4-2-3-1

Kocha: Juma Mgunda/ Seleman Matola

𝑺𝒖𝒃𝒔: 𝑩𝒆𝒏𝒐 𝑲, 𝑵𝒚𝒐𝒏𝒊 𝑬,𝑮𝒂𝒅𝒊𝒆𝒍 𝑴, 𝑲𝒆𝒏𝒏𝒆𝒅𝒚 𝑱, 𝑲𝒂𝒑𝒂𝒎𝒂 𝑵, 𝑩𝒂𝒏𝒅𝒂 𝑷, 𝑩𝒐𝒄𝒄𝒐 𝑱, 𝑲𝒚𝒐𝒎𝒃𝒐 𝑯, 𝑲𝒊𝒃𝒖 𝑫.

𝐑𝐄𝐅𝐄𝐑𝐄𝐄: 𝐑𝐀𝐌𝐀𝐃𝐇𝐀𝐍 𝐊𝐀𝐘𝐎𝐊𝐎
 
ARSENAL HUKU JUU KUNA BARIDI KALI SANA. Timu karibu zote zimecheza mechi 11 na sisi washika bunduki tumecheza 10 lakini cha ajabu nikwamba hawajatutoa kwenye nambari one licha ya wao kucheza mechi nyingi kuliko sisi ZE GUNNERZ. Hongereni sana wana Arsenal Tanzania na dunia nzima kwa ubingwa wa EPL 2022/23 hakika sisi ni unstoppable.
 
Mie Katika Kumbu Kumbu Zangu Miaka Nenda,Miaka rudi...Asenali huwa Wako Vizuri Mwanzoni kama vile Baskeli Ya Miti kwenye 'Slope' ..!

Sasa Shughuli huwa pale Baskeli imeshamaliza 'Slope' inahitajika kuanza kupanda...! Utashangaa Kila mmoja ana overtake...!
 
Naaam, wasalam wakuu,

Ile siku maalumu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu hatimaye imefika. Pambano lenye hadhi la watani wa jadi katika soka la bongo, Yanga na Simba.

Karibuni katika matukio mubashara (live updates) ya mtanange huu wa kukata na shoka baina ya mahasimu wa soka la Bongo #KariakooDerby Yanga na Simba, utakaochezwa saa 11 jioni Estadio De Benjamin Mkapa leo jumapili 23-10-2022.

Huu ni mchezo wa namba 64 wa Ligi Kuu ya NBC 2022/2023, Yanga akiwa ni mwenyeji wa mchezo wa leo dhidi ya mtani Simba.

Mchezo uliyopita wa Ligi Kuu msimu wa 2021/2022 uliochezwa April 30, 2022, timu hizi zilitoshana au kuchoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana/suluhu ya 0-0. Kwa maana hiyo huu ni mchezo wa mzunguko wa kwanza kwenye msimu wa 2022/2023.

Timu hizo zinaingia uwanjani zikiwa na alama 13 kila moja, lakini Simba ipo kileleni kutokana na wingi wa mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya Yanga ambayo inashika nafasi ya pili, kila moja amecheza mechi tano.

Pia michezo mingine (Derby) ya hivi karibuni ni ule wa Mei 28, 2022 kwenye nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup ambapo, Simba alifungwa goli moja bila majibu, ambapo shuti kali la Feisal Salum ‘Fei Toto’ liliwalaza na viatu mashabiki wa Simba siku hiyo.

Vilevile mnamo Agosti 13, 2022 kwenye mechi ya ngao ya Hisani, Simba alitepeta tena kwa Yanga kwa kufungwa goli 2 kwa moja. Fiston Mayele "Mzee wa kutetema" akiingia kambani mara mbili siku hiyo na mashabiki wa Simba wakitoka vichwa chini.

Kwa miaka ya karibuni Simba imekuwa ikishindwa kupata ushindi mbele ya Yanga katika michezo ya Ligi Kuu Bara kwani mara yao ya mwisho kushinda ilikuwa bao 1-0, Februari 16, 2019 lililofungwa na mshambuliaji, Meddie Kagere.

Kwenye mechi za kimataifa, tarehe 16/10/2022 Yanga imetolewa kwenye michuano ya CAF CL na Al Hilal baada ya kufungwa 1-0 na kushukia kwenye michuano ya CAF CC ambapo pia amepangiwa Club Africain kwenye mchezo wa Play off kuelekea makundi.

Pia Simba mechi ya mwisho kimataifa imetoka kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Primeiro De Agosto ya Angola na hivyo kufuzu hatua ya makundi ya CAF CL.

Je, leo itakuwaje baina ya miamba hii miwili? Nani ataibuka kidedea? kaa nami hapa mwanzo, kati na mwisho kupata kila kinachojiri kutoka katika dimba hili lenye kumbukumbu nzuri ya Hayati Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Azam Sports 1 HD wataurusha mpambano huu mubashara (live).

Je, "Watatetema" au "watapiga saluti?" Hahaha #𝑯𝒂𝒊𝒏𝒂𝑴𝒃𝒂𝑴𝒃𝒂𝑴𝒃𝒂
😂😂😂Iseeeh
 
Kuna timu inaingia leo lakini haina amani! Zile shangwe za siku zote hawana! Wanajikaza tu kisabuni.🤣
 
Back
Top Bottom