FT: Yanga SC 4-1 Tanzania Prison | NBC PL | Azam Complex, Chamazi | 28/05/2024

Jaluo_Nyeupe

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Posts
2,824
Reaction score
2,264
Leo majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Azam Complex, timu ya Tanzania Prisons itajipanga mistari miwili kutoa heshima kwa mabingwa wa nchi timu ya Yanga. Baada ya hapo kutapigwa kabumbu kali la kufungia msimu.

Mechi hii inategemewa isiwe na ushindani mkali sana kwani Prisons hayupo katika hatari kubwa ya kushuka daraja wala hawanii nafasi nne za juu.

Mechi hii inatarajiwa kutengenezwa nafasi nyingi za magoli kuelekea kwa Aziz Ki ili aweze kumshinda mpinzani wake katika kutafuta kiatu cha dhahabu.


Kikosi cha Yanga kinachoanza

Kikosi cha Prisons kinachoanza
 
Tumalize ligi na kombe, kiatu cha mfungaji bora, MVP, wachezaji 6 bora kwenye kikosi bora msimu huu, kocha bora na timu bora kiujumla ya msimu huu.
Sisi ni Yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…