Jack Palladino
JF-Expert Member
- Feb 24, 2018
- 7,231
- 22,494
Wananchiiii💚💛
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dhambi jamani 🤣🤣
Mbona wako lukuki?Uwanja mweupe
Uto wamesusia timu yao
BAHLABANE BA NTWA[emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089]
Kila la heri kwa Wananchi.Kumekucha tena wakuu, habari zenu wapenda soka? Ni imani yangu kua mko poa.!
Leo ndo ile siku ambayo wananchi wamekua wakiisubiri Kwa hamu kubwa. Si mlisikia kua kutesa Kwa zamu? Naam Yao imepita sasa ni zamu ya watoto wa Jangwani kula Utawala.
Leo jumamosi ya May 13 2023 kuna mtanange mkali sana, mchezo wa NBC PREMIERE LEAGUE kati ya Yanga sc kutoka mitaa ya karikoo Dar es Salaam dhidi ya Dodoma Jiji.
Huu utakua mchezo wa 28 kwa wote Yanga SC na Dodoma Jiji maarufu kama Walima Zabibu.!
Yanga sc mwenye pointi 71 akiwa anaongoza league atapambana kupata ushindi maana anahitaji pointi 3 tu ili afikishe pointi 74 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine kwenye ligi, hivo atakua ametangaza ubingwa na kutwaa taji la 29. Ubingwa huo utakua ni wa pili mfululizo baada ya mwaka jana kubeba taji hilo. Kwa upande wa Dodoma jiji wao wakiwa na pointi 31 watapigana wapate ushindi ili wajinusuru na kushuka daraja kwani japokuwa wapo nafasi ya 10 kati ya timu 16 zilizopo ligi kuu, Lakini tofauti yao na timu iliyo nafasi ya 13 kwenye mstari mwekundu ni pointi mbili tu!
Yanga sc waliotoka kupata ushindi wa 2-0 mechi iliyopita dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika kusini kwenye kombe la shirikisho barani Afrika watalazimika kushinda hii mechi ili kuhamishia nguvu kwenye michuano ya kimataifa kwani tayari wapo mguu mmoja fainali.
Mechi ya leo pia ni muhimu kwa mshambuliaji wao hatari Fistoni Kalala Mayele mwenye goli 16 akiwa ndiye kinara wa mabao mpaka sasa atatamani kufunga zaidi ili avunje rekodi yake ya magoli aliyofunga msimu uliopita ambayo ni goli 16, je Leo atatetema mbele ya Walima Zabibu? Tusubiri.
Mara ya mwisho hizi timu zilipokutana Dodoma Jiji alichezea kichapo cha bao 2-0. Shukurani Kwa Fistoni Mayele Kwa kupachika bao zote mbili wavuni.
Basi macho na masikio leo saa 10:00 jioni katika dimba la Azam Complex Stadium Chamazi. Updates zote utazipata kupitia huu Uzi..
Kila la kheri Wanachi [emoji169][emoji172]
#Daimambelenyumamwiko
Mchezo umeanza
1' Mayele anafika langoni kwa Dodoma, shuti lake linapaa juu
3' Dodoma wanapiga shuti off target
4' Dodoma Jiji wanapata kona ya kwanza
Wanangu wa hombolo,ihumwa majengo,makutupora,chamwino,makole,kizota,area d pigeni hao UTO
BAHLABANE BA NTWA