Samedi Amba LLC
Member
- Apr 5, 2024
- 81
- 117
Habari wanaJF,
Natumaini mko salama. Nimejibanza sehemu fulani hapa Morogoro ili kuandika maneno haya. Jua linawaka dane, feni inazunguka juu yangu, na hamna usumbufu wowote. Natumaini na wewe unaendelea vizuri. (Na endapo kuna mambo hayaendi, komaa tu. Haya ni mapito. Punde msimu utageuza, na utavuna mema ya bidii yako ya sasa).
Leo nimekuja na wazo fulani nlolopata katika pitapita zangu. Kuna jamaa mmoja anaitwa Dave Ramsey, ambaye alibuni kanuni ya 7 Baby Steps to Financial Freedom (Hatua Saba Rahisi za Kupata Uhuru Kiuchumi).
Nikaona nisijitunzie kanuni hizi, bali nzilete hapa ili tujifunze wote.
✅ Kuondokana na madeni
✅ Kujiwekea akiba ya dharura
✅ Kuwekeza kwa ajili ya baadaye
✅ Kujenga utajiri
✅ Kuwa wakarimu
Kauli yake kuu ni: "Ishi kwa njia ambayo watu wengi wanaona ni upuuzi kwa sasa, ili uweze kuishi kwa njia ambayo itawashangaza baadaye." Hii inamaanisha kufanya maamuzi bora ya kifedha leo ili ufurahie uhuru wa kiuchumi kesho.
💰 Wafanyakazi wa mshahara: Weka angalau mshahara wa mwezi mmoja ili uwe na uhakika wa kodi, chakula, na matibabu vitu visipoenda vizuri.
💰 Wamiliki wa biashara na wenye kipato kikubwa: Anza na TZS 3,000,000+ itakayokusapoti nyumbani na dukani.
✔️ Akaunti za akiba benki au SACCOs ili kukupa nidhamu.
✔️ Kwenye kibubu nyumbani. Hakikisha tu kuwa hii ni siri yako mwenyewe (na epukana na chuma ulete 😎 ).
Naweka akiba ya angalau 5% hadi 25% ya kipato changu.
🔹 Tafuta njia za ziada za kipato (side hustle ni muhimu!).
🔹 Weka akiba kabla ya kutumia—ikiwezekana, tumia njia za kujiwekea akiba kiotomatiki.
🔹 Tumia Kanuni ya 5 hadi 25—anza kidogo lakini uwe na uendelevu mzuri.
Huu ni mwanzo tu! Kesho, tutazungumzia namna ya kudhibiti madeni—bila kujiumiza.
💬 Je, ni changamoto gani kubwa ya kifedha unayokabiliana nayo? Tayari una akiba ya dharura? Toa maoni yako!
Natumaini mko salama. Nimejibanza sehemu fulani hapa Morogoro ili kuandika maneno haya. Jua linawaka dane, feni inazunguka juu yangu, na hamna usumbufu wowote. Natumaini na wewe unaendelea vizuri. (Na endapo kuna mambo hayaendi, komaa tu. Haya ni mapito. Punde msimu utageuza, na utavuna mema ya bidii yako ya sasa).
Leo nimekuja na wazo fulani nlolopata katika pitapita zangu. Kuna jamaa mmoja anaitwa Dave Ramsey, ambaye alibuni kanuni ya 7 Baby Steps to Financial Freedom (Hatua Saba Rahisi za Kupata Uhuru Kiuchumi).
Nikaona nisijitunzie kanuni hizi, bali nzilete hapa ili tujifunze wote.
Dave Ramsey Ni Nani?
Dave Ramsey ni mtaalam wa fedha kutoka Marekani anayejulikana kwa ushauri wake rahisi na unaoeleweka kuhusu fedha. Hatua zake 7 za kifedha zinasaidia watu:✅ Kuondokana na madeni
✅ Kujiwekea akiba ya dharura
✅ Kuwekeza kwa ajili ya baadaye
✅ Kujenga utajiri
✅ Kuwa wakarimu
Kauli yake kuu ni: "Ishi kwa njia ambayo watu wengi wanaona ni upuuzi kwa sasa, ili uweze kuishi kwa njia ambayo itawashangaza baadaye." Hii inamaanisha kufanya maamuzi bora ya kifedha leo ili ufurahie uhuru wa kiuchumi kesho.
Muhtasari wa Hatua 7 za Kujikomboa Kiuchumi
Katika mfululizo huu wa makala, tutazungumzia:- Kuwa na Akiba ya Dharura ya Mwanzo – Weka akiba ya TZS 100,000 ikiwa una kipato kidogo, mshahara wa mwezi mmoja ikiwa umeajiriwa, au TZS 3M+ ikiwa una biashara. Hii itakusaidia kujitengemea wakati wa dharura.
- Lipa Madeni Yote (The Debt Snowball Method) – Mikopo kama MKOBA, SONGESHA, MPAWA na mengine kama hayo yanaweza kukufanya ushindwe kuendelea kifedha. Tutajifunza jinsi ya kuyalipa haraka kwa njia ya "snowball" (au mtiririko wa uzito).
- Weka Akiba ya Miezi 3–6 – Naamini unafahamu kiasi unachokitumia kwa matumizi ya kila mwezi. Chukua kiasi hicho, zidisha mara 3 hadi 6, halafu dhamiria kuhifadhi kiasi fulani cha kipato chako ili kufikia lengo hili. Kawaida, itakuchukua miezi 3 hadi 6 (na wakati mwingine hadi mwaka) kuadjust baada ya kupoteza kazi au fursa. Akiba hii itakusaidia kumudu gharama zote za kawaida hali inapobadilika.
- Wekeza 15% ya Kipato Chako kwa Ajili ya Kustaafu – Usije fikiri kuwa waajiriwa pekee ndo hustaafu. Hata wewe mjasiriamali unaweza kujiwekea kikokotoo binafsi ya kukusaidia baadaye nguvu zinapopungua.
- Weka Akiba kwa Ajili ya Elimu ya Watoto Wako – Ada za shule zinaweza kuwa mzigo mkubwa kama haujajipanga. Tutajadili njia nzuri za kuweka akiba kwa hili. (Na hasa mikopo ya HESLB. Nina marafiki zangu wameapa kuwa watoto wao hawatasoma kwa mikopo, maana waliteseka kulipa). Tutajadili zaidi, na kuona cha kufanya ili kumudu hali hii.
- Dhamiria Kuhamia Kwako – Kumiliki nyumba yako kutakuondolea kero ya kodi, itakupa amani ya moyo, na wigo mpana zaidi wa kutumia hela ulizonazo. Tutaangalia options zilizopo hapa Bongo.
- Kuza Mali Zako, Tenda Wema/Ukarimu – Wekeza kwa akili, anzisha biashara zingine, saidia jamii yako. Utoaji wa sadaka na kusaidia wengine hufungua milango ya mibaraka maishani.
_________________________________________________________
Hatua ya Kwanza: Anza na Akiba ya Dharura
Kwa Nini Hii Ni Muhimu?
- Watanzania wengi hutegemea mikopo ya simu (MPAWA, SONGESHA) kukidhi mahitaji ya dharura. Wafanyakazi huchukua mikopo ya dharura (emergency loans, salary advance na top up).
- Akiba ya dharura hukusaidia kuepuka kulazimika kukopa kwa shida ndogo ndogo (matumizi).
Unapaswa Kuweka Akiba Kiasi Gani?
💰 Wenye kipato kidogo (wadada wa kazi, walinzi, garden boys, wafanya usafi): Anza na TZS 100,000. Dunduliza kwa miezi kadhaa, utafika. Hutalazimika kupiga simu mtoto anapoumwa ghafla.💰 Wafanyakazi wa mshahara: Weka angalau mshahara wa mwezi mmoja ili uwe na uhakika wa kodi, chakula, na matibabu vitu visipoenda vizuri.
💰 Wamiliki wa biashara na wenye kipato kikubwa: Anza na TZS 3,000,000+ itakayokusapoti nyumbani na dukani.
Pa Kuweka Akiba Hii?
✔️ Akaunti za pesa za simu (M-Pesa, Airtel Money, Mix by Yas) kwa upatikanaji wa haraka.✔️ Akaunti za akiba benki au SACCOs ili kukupa nidhamu.
✔️ Kwenye kibubu nyumbani. Hakikisha tu kuwa hii ni siri yako mwenyewe (na epukana na chuma ulete 😎 ).
_________________________________________________________
Njia Yangu Binafsi – Kanuni ya 5 hadi 25
Nimejianzishia kanuni rahisi ya kuweka akiba ya dharura:Naweka akiba ya angalau 5% hadi 25% ya kipato changu.
- Nikipata TZS 10,000, naweka akiba ya TZS 500 hadi TZS 2,500.
- Nikipata TZS 1,000,000, naweka akiba ya TZS 50,000 hadi TZS 250,000.
Anza Kuweka Akiba Leo
🔹 Punguza matumizi yasiyo ya lazima (mfano, soda ya kila siku, na manunuzi nje ya bajeti).🔹 Tafuta njia za ziada za kipato (side hustle ni muhimu!).