chuma jr
Member
- Oct 17, 2015
- 88
- 135
Kutokana na kutembea sana humu JF nimekutana na baadhi ya member wakiuliza njia za kutumia ili waweze kulinda mawazo yao ya biashara mimi kama member mwenzenu nilikuwa katika sintofahamu hiyo nilikuwa sijui wapi niende nikalihifadhi wazo langu kisheria hivyo nilipita humu lakini sikupata muelekeo rasmi sababu wengine walitaja BRELA ndipo unaenda kusajiri wazo wengine walisema cosota lakini kidogo nilipata idea kisha nikajiongeza hivyo ningependa kuleta mrejesho na muongozo utakaowasaidia members wengine wenye mawazo ya biashara lakini hawajui wapi wakasajiri ili endapo kama wanaenda kuomba ufadhili wa mtaji au kuomba partner wa biashara unakuwa na hofu ya kuibiwa wazo lako na usiwe pa kumpeleka huyo mtu sasa fuata njia hizi.
1}Andika au record hilo wazo lako ukirecord hakikisha linahifadhiwa kwenye CD na sio sehemu tofauti na CD
hakikisha wazo lako linakuwa kwenye mtiririko ufuatao
a}mwanzo-hapa mwanzo unaanza kutoa kama muhtasari wa wazo lako.
b}katikati-hapa ndipo unaliweka wazo lako lote bila kubakisha.
c}Mwisho- hapa unahitimisha kwa kutoa matarajio yako kama wazo lako likianza kufanya kazi ni faida zipi unazitarajia kama ni faida binafsi au na taifa kiujumla.
Ukishaliandaa hilo wazo kwa mtiririko huo nenda COPYRIGHT SOCIETY TANZANIA (COSOTA) ukiwa na karatasi iliyobeba hilo wazo lako au CD iliyokuwa na sauti yako au ya mtu mwingine aliyerekodi ukienda huko andaa 10,000 ya fomu then 20,000 ya kujisajiri yani ada ya mwaka hiyo kuwa mwanachama then 1,000 ya kujaza fomu ya usajiri wa kazi yako jumla unatakiwa kuwa na 31,000 tu ila viambatanisho muhimu lazma uwe na kitambulisho na pasport size mbili hapo kwenye kitambulisho unatoa copy ndipo unawapatia ila sijajua kama cha shule kinatumika.
Baada ya kujaza fomu zote utakazopewa na ukilipia hiyo 31,000Tsh utasubiri wazo lako lipitiwe na wana baraza la cosota hao ndo wataamua kama kweli linahitajika kuhifadhiwa kama wazo unique au ni wazo ambalo lishawahi kusajiriwa hivyo tayari lina mwenyewe kama ni wazo jipya halijawahi kuonekana na halina utata wowote basi utapewa hati ya umiliki wa hilo wazo lako lakini hiyo hati utailipia elfu 10,000 tu hivyo utakuwa na uwezo wa kwenda kwa mtu ukaliwasilisha hilo wazo na asikuzidi akili na kwa usalama wake unaweza kumuonesha ile hati ya cosota ili ajue kuwa unalilinda kisheria lakini pia ukishakuwa mwanachama pale cosota unaweza kusajiri wazo lingine na lingine na mengi zaidi au kazi yoyote ya ubunifu wako utasajiri kwa elfu moja 1000 utasubiri baraza lipitie hiyo kazi yako kisha utalipia elfu kumi 10,000 ya kuchukua hati ya umiliki hivyo kila kazi utakayo isajiri itapewa hati yake.
Lakini kama wazo lako tayari lishakuwa developed yani linafanya kazi tayari lakini unaweza kulilinda pia ukaenda kusajiri kama kampuni au biashara ili mtu asiweze kufuata nyayo zako akaleta ushindani hiyo kama ukipenda mwenyewe lakini sio lazma.
Yangu ni hayo tu ndugu zangu kutokana na msaada ninaoupata kupitia members wa JF hivyo na mimi nimeona nisiwe mchoyo kushare nanyi huu utaratibu najua kuna wengi wanapitia hali ya kutokujua ni wapi watayalinda mawazo yao ya biashara kisheria ili yasichukuliwe hivyo nadhani hii itasaidia watu wengi sana,ADMINS mnaweza kupin hii thread ikae juu ili ionekane kirahisi na kama sijaiweka kwenye jukwaa linalohitajika mnaweza kunisaidia kuipeleka kwenye jukwaa husika.
ASANTENI SANA