Fuata njia hizi kulinda wazo lako la biashara

Fuata njia hizi kulinda wazo lako la biashara

Ni lini ulisikia COSOTA wamemsaidia mtu? Hivyo vyombo vipo kimaslahi zaidi wala havifanyi chochote. Hata hawa sijui TFDA, TBS hakuna wanachokifanya zaidi ya kukusanya hela .

Nilisajili kinywaji (spirit) nikafuata utaratibu wote .. na nikapewa documents zote. Haikupita muda serikali ikatangaza kuondoa viroba kwenye soko la vinywaji .. hadi naandika hapa sikupata msaada wowote.

Kama una wazo lako la biashara mshirikishe mwenye mtaji mfanye kazi lakini hakikisha kuna kitu unakifanya wewe kama wewe ili kulinda wazo lako.

Narudia COSOTA hawatakusaidia kwa lolote; mwenye pesa ni wa kuogopa.

Hapa mimi nasambaza mbolea ya maji .. sijapata pesa kwa ajili ya kusajiri, wapo wanaonifuata na kunishauli tushirikiane tukasajili .. nawakatalia. Ninachokifanya ni kwamba nimekuwa na shamba darasa ambapo wale wanaobisha kwamba mbolea yangu haijasajiriwa nawaeleza kuwa kusajiri ni kutafutia ulaji wengine.

Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno.
Sawa mkuu
 
naona kila mtu ako na mawazo yake juu ya hii thread lakini ukija kusema kwamba mtu atalifanyia editing halafu akalisajiri maneno yanaweza kutofautiana lakini mtu akisoma wazo lako original na editing ya wazo lako unakuta mlengo ni ule ule original yako inaweza ikawa ni karanga kupitia mitandao ya kijamii kisha editing ikawa ni kuuza karanga vilele lakini yeye asiseme kuuza kwenye mitandao akatafuta njia nyingine lakini ni wazo ambalo umeliwaza wewe na mwengine akalijua kwa namna moja au nyingine au pengine na yeye aliliwza kama wewe lakini ni kitu ambacho hakipo nchini au dunani hivyo hapo ndo inakuja kazi ya wanabaraza kuanza kuchambua na kugundua kama hayajagongana au kama yamegongana lakini kuna mtu ambae alikuwa wa kwanza kwenda kulisajiri na yeye ndo atakaekuwa mmiliki wa hiyo idea hivyo huwezi kusema hilo wazo ulilonalo kichwani ukakuta mtu kashalisajiri ukasema kakuonea ulitaka upewe hati ya umiliki wakati wazo lipo kichwani tu au cosota wataota kuwa na wewe una wazo la biashara linahitaji kusajiriwa na huwezi ukaliweka wazi wazo lako ukasema eti ni wazo lako kisha uweke onyo kwa atakaelichukua sasa utampeleka wapi na una kidhibiti kipi cha kuthibitisha kuwa kweli lile ni wazo lako labda ukamloge asee maana kule ndo hakunaga kuomba ushahidi kule hakuna sheria kule ni vitendo tu lakini kama mahakamani huwezi kunisimamisha kama huna kidhibiti chochote ndo maana zikawekwa hizi mamlaka za kwenda kufanya usajiri ndugu zanguni tusiwe wabishi sana.
OVER
 
Hakuna wazo jipya...Kumbuka kuwa ukijarifiria nakuenda kuliwekea Copyright kuna aliliwaza na hana wazo la biashara. Hata likiwa na Copyright mtu ypypte anaweza litumia kwa kubadili maneno machache tu......
Njia pekee nayo amini kuhusi kulinda wazo lako..Nikuliweka katika vitendo..Ndipo kuliombea Copyright. Hapo hata mtu akiliiba na kulitumia, atakamatwa oale itakapo onekana wewe umeanza kulifanyia kazi mapema sana.
bado ni ngumu h
Mkuu nadhani hii siyo maana ya mtoa mada, kwa jinsi nilivyomuelewa kwa mfano wewe Tutor B una idea yako lakini huwezi kupata capital kwa sasa hivyo unakuja kunishirikisha ili mimi bunyebunye nitoe pesa na wewe utoe wazo hilo, kisha tugawane kutokana na makubaliano yetu.

Lakini kwa uswahili na kugeuka kwa sababu mimi nina pesa na wazo pia nimeshalipata kutoka kwako naamua kufanya peke yangu.

Hivyo kama umefuata utaratibu aliotoa hapo juu mtoa mada unaweza kupata msaada COSOTA.
Ahsante.
Kwa hiyo wakati unanishirikisha hilo wazo lako kunakuwa na mashahidi ili nisikugeuke?
 
Barikiwa KWA JUMBE,

Kwa kuongeza tu usajili COSOTA upo WA mtu binafsi, ndio umeeleza hapo, lkn pia upo KWA wale wenye kampuni. Tofauti ni kwenye malipo na dokumenti za umiliki. KWA umiliki WA mwenye kampuni, Shari asajili kampuni ya aina yeyote,

Kwa Masada zaidi ya kusajili kampuni, nipigie 0684205039
IMG_20170801_195508_611.jpeg
 
Kutokana na kutembea sana humu JF nimekutana na baadhi ya member wakiuliza njia za kutumia ili waweze kulinda mawazo yao ya biashara mimi kama member mwenzenu nilikuwa katika sintofahamu hiyo nilikuwa sijui wapi niende nikalihifadhi wazo langu kisheria hivyo nilipita humu lakini sikupata muelekeo rasmi sababu wengine walitaja BRELA ndipo unaenda kusajiri wazo wengine walisema cosota lakini kidogo nilipata idea kisha nikajiongeza hivyo ningependa kuleta mrejesho na muongozo utakaowasaidia members wengine wenye mawazo ya biashara lakini hawajui wapi wakasajiri ili endapo kama wanaenda kuomba ufadhili wa mtaji au kuomba partner wa biashara unakuwa na hofu ya kuibiwa wazo lako na usiwe pa kumpeleka huyo mtu sasa fuata njia hizi,

1}Andika au record hilo wazo lako ukirecord hakikisha linahifadhiwa kwenye CD na sio sehemu tofauti na CD
hakikisha wazo lako linakuwa kwenye mtiririko ufuatao
a}mwanzo-hapa mwanzo unaanza kutoa kama muhtasari wa wazo lako.
b}katikati-hapa ndipo unaliweka wazo lako lote bila kubakisha.
c}Mwisho- hapa unahitimisha kwa kutoa matarajio yako kama wazo lako likianza kufanya kazi ni faida zipi unazitarajia kama ni faida binafsi au na taifa kiujumla.

Ukishaliandaa hilo wazo kwa mtiririko huo nenda COPYRIGHT SOCIETY TANZANIA (COSOTA) ukiwa na karatasi iliyobeba hilo wazo lako au CD iliyokuwa na sauti yako au ya mtu mwingine aliyerekodi ukienda huko andaa 10,000 ya fomu then 20,000 ya kujisajiri yani ada ya mwaka hiyo kuwa mwanachama then 1,000 ya kujaza fomu ya usajiri wa kazi yako jumla unatakiwa kuwa na 31,000 tu ila viambatanisho muhimu lazma uwe na kitambulisho na pasport size mbili hapo kwenye kitambulisho unatoa copy ndipo unawapatia ila sijajua kama cha shule kinatumika.

baada ya kujaza fomu zote utakazopewa na ukilipia hiyo 31,000Tsh utasubiri wazo lako lipitiwe na wana baraza la cosota hao ndo wataamua kama kweli linahitajika kuhifadhiwa kama wazo unique au ni wazo ambalo lishawahi kusajiriwa hivyo tayari lina mwenyewe kama ni wazo jipya halijawahi kuonekana na halina utata wowote basi utapewa hati ya umiliki wa hilo wazo lako lakini hiyo hati utailipia elfu 10,000 tu hivyo utakuwa na uwezo wa kwenda kwa mtu ukaliwasilisha hilo wazo na asikuzidi akili na kwa usalama wake unaweza kumuonesha ile hati ya cosota ili ajue kuwa unalilinda kisheria lakini pia ukishakuwa mwanachama pale cosota unaweza kusajiri wazo lingine na lingine na mengi zaidi au kazi yoyote ya ubunifu wako utasajiri kwa elfu moja 1000 utasubiri baraza lipitie hiyo kazi yako kisha utalipia elfu kumi 10,000 ya kuchukua hati ya umiliki hivyo kila kazi utakayo isajiri itapewa hati yake,

lakini kama wazo lako tayari lishakuwa developed yani linafanya kazi tayari lakini unaweza kulilinda pia ukaenda kusajiri kama kampuni au biashara ili mtu asiweze kufuata nyayo zako akaleta ushindani hiyo kama ukipenda mwenyewe lakini sio lazma.

yangu ni hayo tu ndugu zangu kutokana na msaada ninaoupata kupitia members wa JF hivyo na mimi nimeona nisiwe mchoyo kushare nanyi huu utaratibu najua kuna wengi wanapitia hali ya kutokujua ni wapi watayalinda mawazo yao ya biashara kisheria ili yasichukuliwe hivyo nadhani hii itasaidia watu wengi sana,ADMINS mnaweza kupin hii thread ikae juu ili ionekane kirahisi na kama sijaiweka kwenye jukwaa linalohitajika mnaweza kunisaidia kuipeleka kwenye jukwaa husika.
ASANTENI SANA
Apa nimepata mwanga niliokuwa natafuta
 
Hv Kusajili wazo Bunifu lazima niende Ofisi za COSOT????
 
Back
Top Bottom