Kumekuwa na kasi ya usambaaji wa taarifa na propaganda nyingi kuhusu ugonjwa wa Corona na chanjo ulimwenguni. Propaganda hizo zimeibua nadharia nyingi miongoni mwa jamii.
Shirika la Afya ulimwenguni limefanya jitihada mbalimbali katika kudhibiti ueneaji wa propaganda katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Wataalamu wa Afya wanashauri wanajamii kuzingatia taarifa za ugonjwa na chanjo kutoka katika vyanzo vinavyoaminika
Aidha, unasisitiza kuwa unapopata taarifa zozote mpya kuhusu ugonjwa usizisambaze mpaka uhakikishe zimetoka katika vyanzo sahihi