Unaulizia kusafisha ikiwa imefungwa kwenye injini au ikiwa imetolewa?
Ikiwa imefungwa kuna additives kutoka kwa kampuni mbalimbali kama Liqui Moly, Wynns, STP n.k., ambazo zinawekwa kwenye tanki la mafuta kufanya hiyo kazi ya kusafisha injector nozzles.
Ikiwa imetolewa hapo nafikiri ukiwaona Bosch pale karibu na former national milling ya TAZARA, wataweza kukusafishia kwa uzuri. Pia kuna Vigor Diesel walio Mbagala Zakheim jirani na NMB.