Fukaza fukuza ya Makocha Taifa Stars ina faida yoyote?

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari,

Kuna hili sekeseke na mihemko ya kufuka machoka kwa kipindi kifupi sana kwa timu yetu ya Taifa.

Kabla ya huyu Ettiene Ndayiragije kocha ambaye tuliwapora Azam Fc kwa lazima na mbwembwe nyingi leo kamati ya TFF imemfungisha mizigo na kuondoka.

Tuliku na mtaalamu Emmanuel Amunike huyu alifanikiwa kuifikisha Taifa Stars mbali kidogo ukilinganisha na wengine waliopita.

Pamoja na wengine wengi hapo njuma hili sekeseke la fukuza fukuza limewasomba.

Tujiilize maswali kidogo juu ya huu utaratibu wa kufukuza makocha kwa timu yetu pekee (Taifa Stars)

✓ Tungefahamishwa kabisa scouts wanao husika kutafuta hawa makocha ni hakina nani?

✓ Kama wapo huwa wanapewa vigezo na sifa zipi nikiwa na maana ya malengo ya timu tufike wapi?

✓ Kuna watu katika hiyo kamati wananufaika na fukuza fukuza na umekuwa mradi hivyo biashara ili iweze kukua inabidi swala lidumu?

✓ Tunafaidika na nini na fukuza fukuza kwa upande wetu wa maendeleo kwa timu yetu ya Taifa Stars?

✓ Huyu aliyefukuzwa ameshindwa nini na huyo anayekuja ana utofauti upi tutakapo mleta?

Kwa ujumla tuangalie sana haya maamuzi na tusiwe watu wa kukurupuka, badala ya kupiga hatua mbele zaidi tutajikuta tunarudi nyumba hatua nyingi bila kustuka.

Tutabaki watu wa kukuza Curriculum Vitae (CV) za hao makocha tunao wafukuza fukuza leo.

Nawasilisha Mzee Mkoloni

Cc: Kichwa Kichafu.
 
Coaches are hired to be fired. Nothing special on that.
 
Ungeanza kuwauliza timu yako upotolo kwani hawakai na makocha muda mrefu labda ungepata mwanga kwanini Taifa stars makocha hawakai
 
Kuna vya kumlaumu Mwalimu na kuna vya kuwalaumu wachezaji, timua timua sio suluhisho, i think we need to reshuffle our training programs, players and management

Wachezaji kushindwa kujitoa/kujituma/kupambana tumlaumu kocha?
 
Wafukuze, wasifukuze. Hamna cha tofauti, Taifa Stars ni ile ile.
 
Huyo kocha mrundi hana jipya. Nimefurahi sana alivyofukuzwa.
 
Nakumbuka kipindi TFF imemsainisha Ndayiragije kuinoa Starz, mkurugenzi wa ufundi Oscar Milambo alisema kwamba malengo makubwa waliyompa Ndayiragije ni kuhakikisha Starz inafuzu michuano ya CHAN ambapo tulikuwa tunakutana na Kenya first leg,

Pia lengo jingine ni kuhakikisha Starz inafuzu kwa kuingia group stage ya World Cup qualifying games ambapo tulikuwa tumepangiwa kucheza na Burundi hatua ya mtoano

Na kiukweli, tulifanikiwa kufuzu kushiriki CHAN baada ya kuwatoa Kenya na Sudan

Kisha tulifanikiwa kumtoa Burundi na tukaingia group stage ya World Cup qualifying games, ambapo so far tuna point 4 na mechi mbili mkononi kutamatisha group stage round

Sasa kwa malengo aliyopewa vs mafanikio tulifikia,
bado naona kama alistahili kuendelea kuwa na Starz

Ila kwa maamuzi waliofanya TFF basi naanza kupata shaka kuwa hii fukuza fukuza ya makocha inawezekana kukawa na 'dili' ktk kusainisha makocha wapya

TAKUKURU pigeni kambi vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…