Fukuza Robetinho Bakiza Mgunda

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
2,345
Reaction score
6,970
Cheka sana lakini Omba yasikukute!

Sababu kuu ya kusajiliwa mwalimu Robetinho ilikuwa ni kuifanya Simba ifuzu nusu fainali kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.

Yeye mwenyewe (Robetinho) amewahi kukaliliwa wakati akizungumza na vyombo vya habari ya kwamba "Simba ni timu kubwa na ni lazima ifike mbali mwaka huu,siyo kufika nusu fainali tu bali kubeba ubingwa, mimi kama kocha siwezi kuwa na malengo ya kufika nusu kwasababu nusu kwangu siyo mafanikio, nitaiongoza Simba mwaka huu ifike fainali na ikiwezekana ichukue ubingwa"

Kama ndivyo ilikuwa sababu kuu ya kuletwa Simba nadhani ni wakati wa yeye kuondoka na kuiachia timu Mgunda achukue nafasi. Tukumbuke Robetinho ameletwa kuinoa Simba si kwamba ilikuwa ikifanya vibaya chini ya Mgunda. Simba ya Mgunda naamini ingeingia nusu fainali kwasababu ya aina ya uchezaji na mfumo wake, kipindi cha Mgunda Moses phiri alikuwa ni mdedly kweli kweli, leo Moses phiri anawekwa benchi kisa mfuga Rasta Kibu D ambaye kwa mtazamo wangu ni kama mbahatishaji tu.

Hebu fikiria leo tungekuwa na Baleke pale mbele, Moses phiri akiwa kwenye ubora wake, Clatous Chama, na Saidoo ntibanzokiza, naamini Wydad alikuwa anakufa kwa Mkapa chuma 3 kama amesimama.

Tuna bahati kukutana na Wydad akiwa dhoofu bin hali lakini tumeshindwa kufanya kitu, huu mwaka ulikuwa wetu kabisa wa kuingia Nusu ila kwangu sababu ni Robetinho ingawa watu wengi wanaona kama anafanya vizuri ila kwangu huyu kocha ni bora ya Mgunda, yeye ashukuru Mungu upepo unamtembelea tu lakini pale hamna kocha na hili litathibitika hivi karibuni, najua mtanishambulia kwa maneno makali lakini ukweli utadhihirika tu.

Niwahakikishie ndugu zangu wana lunyasi ya kwamba,kama tutaendelea na kocha Robetinho hao Utopolo watachukua Ubingwa na mwakani na hakuna wa kuwazuia, naamini Mgunda angempa sana Nabi changamoto ila kwa Robetinho bado sijaona, sisi kuwafunga Utopolo tarehe 16 ilikuwa tu tumejipanga kisaikolojia ila naamini yule mchawi Nabi akishaipata dawa ya Robetinho na mfumo wake hakika tuta-tafutana!

Namkubali sana Kocha Mgunda kuliko Robetinho.

Alamsiki.
 
Aahaaaaa
 
Robertinho haondoki ng'oo nimekaa pale.

TZ tunahitaji Makocha washindani wengi ili ligi yetu ikue zaidi na zaidi duniani kiubora.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Daah, nadhani wewe ni mbongo fleva au Msingeli, soka hasa la Simba ungefanya likupite hivi.

Ntibanzokiza? Huyu ni mmoja wa watu anayeua counter zote za Simba, anapoteza mipira vizuri sana.

Robertinho, kwangu mimi ni FUNDI zaidi kimchezo, katumia kikosi alichokikuta, kilichochoka, kusonga mbele!

MO kaikimbia timu baada ya kujua utawala wa MSOGA umerudi, kama MANJI alivyowakimbia Yanga alipojua Msoga era imetamatika.

Simba FANS hawana deni na timu yao, kimpira kwasasa hapa TZ, nafasi ya PILI ndo bingwa, ya kwanza ilishauzwa na TFF, si ya kugombea.

Robertinho ataendelea kuwepo sana.
 
Nonsense Manchester city and PYRAMIDS had invested alot of money in football but none of them won either UEFA champions league or Caf champions league how much money did simba invested you pathetic fans
 
Kuna kocha anayesema tunaenda kufungwa mapema?
Simba ina Wachezaji wa kiwango cha chini ikilinganishwa na Wachezaji wa timu zingine zilizoingia klabu bingwa.
Hebu FIKIRIA Luis Miquison alikuwa bora sana akiwa Simba, lakini ameenda Al ahly anaonekana ana kiwango Dunia, Je, wale waliosalia Simba si watakuwa chini sana.
Hivyo, tukubali kuwa usajili wetu ni wa bei Chee. Hivyo, tulipofikia ni mafanikio makubwa.
By the way, group la Simba wote wametolewa.
 
KUHUSU SUALA LA USAJILI.

NASHAURI YAFUATAYO.

1. NIMESIKITIKA UONGOZI KUMUACHA BENO KAKOLANYA.
Kupata Golikipa aina ya kakolanya itakuwa mtihani mkubwa sana.
Sijui kama Tutakuwa na Golikipa No 2 mwenye ubora wa Kakolanya.
Sijui kama hatutaenda Nje kutafuta mbadala wa MANURA.

2.UBAHILI NA 10% KWENYE IDARA YA USAJILI.
tumeshuhudia wakiletwa wachezaji cheep mno kwenye usajili wachezaji wenye uwezo mdogo sana na gharama ndogo sama

3. USAJILI WA QUALITY NDOGO NA KUKOSA SCAUT WAZURI.

I. Ismail sawadogo.
II .mohamed Qottara
III. Augustino Okkrah. (9)
IV. Peter Banda.
V. Sadio Kanute atafutiwe mbadala(8)
VI. Sackho nae Atupishe.

4. WACHEZAJI WAZAWA NAPO NI SHIDA.
Changamoto ya umli.
Nyoni, Boko, mkude,
Viwango vidogo.
Kapama, Gadiel, Mwanuke,

MASHABIKI TUMECHOSHWA KUISHIA ROBO FAINALI.
TUNA HELA ZA KUTOSHA KWA AJILI YA USAJILI.
HELA YA SUPER CUP 4 BILION.
HELA YA CAF. CAFCL 2 BILION

UONGOZI PUNGUZENI UBAHILI
ROBERTINO ASAJILI.
 
Simba Ina wachezaji wachache wa kucheza Nusu Fainali.

WACHEZAJI wengi walionao Simba sio wa Nusu Fainali.

Siku wakija kulijua Hilo ndipo watafika huko nusu Fainali.
1. SIMBA HII NI MBOVU MNO IMEBEBWA NA UONGOZI KUWA PAMOJA FRIENDS OF SIMBA WAMEKUBALI YAISHE.
2. UBORA WA MWALIMU ROBERTINHO
 
Mna hela ya kutosha [emoji3][emoji3] ,
 
mgunda anachoweza ni mambo ya kibongobongo ambayo ninyi simba huwa hamuachi, maandalizi ya timu ya ufundi/uchawi kuloga mechi. wazungu hawana hayo. utamfukuzaje mtu aliyeisaidia simba kutetemesha nchi nzimaya morocco? hadi mfalme wao hakula chakula hadi mpira ulipoisha nchi nzima walikuwa wanaiogopa simba na almanusura simba wawatoe wale watu, bahati yao tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…