TUKANA UONE
JF-Expert Member
- Jan 3, 2018
- 2,345
- 6,970
Cheka sana lakini Omba yasikukute!
Sababu kuu ya kusajiliwa mwalimu Robetinho ilikuwa ni kuifanya Simba ifuzu nusu fainali kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.
Yeye mwenyewe (Robetinho) amewahi kukaliliwa wakati akizungumza na vyombo vya habari ya kwamba "Simba ni timu kubwa na ni lazima ifike mbali mwaka huu,siyo kufika nusu fainali tu bali kubeba ubingwa, mimi kama kocha siwezi kuwa na malengo ya kufika nusu kwasababu nusu kwangu siyo mafanikio, nitaiongoza Simba mwaka huu ifike fainali na ikiwezekana ichukue ubingwa"
Kama ndivyo ilikuwa sababu kuu ya kuletwa Simba nadhani ni wakati wa yeye kuondoka na kuiachia timu Mgunda achukue nafasi. Tukumbuke Robetinho ameletwa kuinoa Simba si kwamba ilikuwa ikifanya vibaya chini ya Mgunda. Simba ya Mgunda naamini ingeingia nusu fainali kwasababu ya aina ya uchezaji na mfumo wake, kipindi cha Mgunda Moses phiri alikuwa ni mdedly kweli kweli, leo Moses phiri anawekwa benchi kisa mfuga Rasta Kibu D ambaye kwa mtazamo wangu ni kama mbahatishaji tu.
Hebu fikiria leo tungekuwa na Baleke pale mbele, Moses phiri akiwa kwenye ubora wake, Clatous Chama, na Saidoo ntibanzokiza, naamini Wydad alikuwa anakufa kwa Mkapa chuma 3 kama amesimama.
Tuna bahati kukutana na Wydad akiwa dhoofu bin hali lakini tumeshindwa kufanya kitu, huu mwaka ulikuwa wetu kabisa wa kuingia Nusu ila kwangu sababu ni Robetinho ingawa watu wengi wanaona kama anafanya vizuri ila kwangu huyu kocha ni bora ya Mgunda, yeye ashukuru Mungu upepo unamtembelea tu lakini pale hamna kocha na hili litathibitika hivi karibuni, najua mtanishambulia kwa maneno makali lakini ukweli utadhihirika tu.
Niwahakikishie ndugu zangu wana lunyasi ya kwamba,kama tutaendelea na kocha Robetinho hao Utopolo watachukua Ubingwa na mwakani na hakuna wa kuwazuia, naamini Mgunda angempa sana Nabi changamoto ila kwa Robetinho bado sijaona, sisi kuwafunga Utopolo tarehe 16 ilikuwa tu tumejipanga kisaikolojia ila naamini yule mchawi Nabi akishaipata dawa ya Robetinho na mfumo wake hakika tuta-tafutana!
Namkubali sana Kocha Mgunda kuliko Robetinho.
Alamsiki.