Katika siasa za ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), jina la Fulgence Lwiza limezidi kupewa uzito mkubwa katika Kata ya Yombo Vituka, Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam. Kwa sasa, hakuna anayeweza kupuuza nguvu, ushawishi na mvuto wa mwanasiasa huyu kijana ambaye amekuwa akigusa karibu kila eneo la maendeleo ya kata hiyo.
Lwiza ameibuka kama kiongozi anayesikiliza, kushughulikia kwa haraka changamoto za wananchi na kushirikiana nao bega kwa bega katika kuboresha maisha yao. Amegusa makundi yote ya jamii – kina mama, vijana, wazee, walemavu na hata watoto kupitia miradi ya kijamii yenye tija.
Ndiyo maana si ajabu kwamba ndani ya CCM, Fulgence Lwiza kwa sasa ndiye kivutio kikubwa kwa wajumbe wa chama hicho ngazi ya kata. Wengi wa wajumbe wameonesha waziwazi kumuunga mkono, wakisema ni mtu sahihi kwa wakati huu – mtu wa kazi, mtu wa watu.
Kinyume chake, mpinzani wake wa karibu, Ndugu Kashakara, anaonekana kukumbwa na hali ngumu ya kisiasa. Habari kutoka vikao mbalimbali vya mashauriano vinaonesha wazi kuwa Kashakara anakutana na vizingiti vikubwa, kiasi cha kuanza kukata tamaa hata kabla ya kufanyika kwa kura za maoni ndani ya CCM.
Maoni ya Wananchi
Katika kuangazia hali halisi, mwandishi wetu amezungumza na baadhi ya wananchi kutoka mitaa tofauti ndani ya kata ya Yombo Vituka, na haya ndiyo waliyoeleza kuhusu Fulgence Lwiza:
1. Bi. Hadija Mvungi – Mtaa wa Machimbo:
"Fulgence si mwanasiasa wa maneno, ni mtu wa vitendo. Ameleta maboresho kwenye huduma za afya hapa Machombo, na pia amekuwa mstari wa mbele kusaidia akina mama wajasiriamali. Tunamuona kama tumaini letu."
2. Bw. Emmanuel Kasambala – Mtaa wa Vituka:
"Huyu kijana ana moyo wa kusaidia. Kila mara kuna mkutano au changamoto inapotokea, yupo. Hana makuu. Wajumbe wa CCM wasifanye makosa, huyu ndiye anafaa kupewa nafasi."
3. Mama Subira Ally – Mtaa wa Mzambarauni:
"Siku hizi hata watoto wetu wanafurahia mazingira ya shule kwa sababu Fulgence alisimamia ukarabati wa madarasa. Hii ni kazi ya kweli. Tunamuunga mkono kwa nguvu zote."
4. Bw. Jackson Mang’enya – Mtaa wa Magogoni:
"Fulgence ni mfano wa viongozi wa kisasa. Hasa vijana tumevutiwa naye kwa sababu anatupa nafasi za kujieleza na kushiriki kwenye mipango ya maendeleo."
5. Dada Neema Shabani – Mtaa wa Machimbo:
"Kila kona ya kata, unasikia jina la Fulgence. Anafika hadi maeneo ya pembezoni na kujua shida zetu. Huyu anatufaa kuliko mtu mwingine yeyote kwa sasa."
Hitimisho
Kwa sasa, upepo wa kisiasa ndani ya Yombo Vituka unaelekea upande mmoja tu – upande wa Fulgence Lwiza. Uaminifu wake kwa wananchi, uwezo wake wa kusikiliza na kutatua matatizo, pamoja na mahusiano mazuri na makundi yote ya jamii, vinamweka mbali mbele ya wapinzani wake.
Katika safari ya kuelekea kura za maoni ndani ya CCM, jina la Fulgence linaendelea kuwa mwiba kwa wapinzani na faraja kwa wananchi. Bila shaka, Kata ya Yombo Vituka iko kwenye mwelekeo sahihi wa kupata kiongozi wa kweli anayewakilisha maslahi yao.
View attachment 3411835