star health talks
Member
- Apr 28, 2017
- 30
- 73
Full blood picture ni kipimo gani? Je, nikipima kipimo cha Full blood picture kila ugonjwa mwilini mwangu utaonekana?
Full blood picture au Full blood count kimekuwa ni kipimo kinachosikika sana kikitajwa mara nyingi kila tuendapo kupata huduma kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
Ukitumia tafsiri ya moja kwa moja kutoka kingereza kwenda Kiswahili ni rahisi kufikiri Full blood picture inaonyesha kila kitu mwilini, la hasha sio kweli, Full blood picture haioneshi kila kitu au kila ugonjwa mwilini tofauti na jina lake linavyosema.
Uhalisia ni kuwa Full blood picture inaangalia aina tu za seli katika mfumo wa mwili wa mwanadamu na wala sio magonjwa yote mwilini unavyoweza kudhani.
Full blood picture inaangalia aina kuu tatu za seli mwilini. Seli hizi ni chembe seli nyeupe “white blood cell”, chembe sahani” platelets” na seli za damu “ red cell line”.
Tukianza na seli nyeupe au kitaalam “white blood cells” hizi ni seli kinga zinazohusika na kuulinda mwili usipate au upambane pale upatapo magonjwa. Hizi ni seli ambazo huongezeka kwa wingi kipindi mtu kapata maradhi au infection kama ambavyo mara nyingi utaambiwa ukienda hospitali, hii nimeiongelea kwenye makala nyingine .
unaweza kugusa kiunganishi hiki kuisoma makala ya infection kwa kina hapa Kila nikienda hospitali naambiwa nina Infection, Infection ni nini? na kwanini kila mara naambiwa nina infection?
Chembe sahani au platelets hizi ni seli zinazohusika na ugandaji wa damu mwilini.
Seli za damu au kitaalam red cell line hizi zinaonesha wingi wa damu, na kama damu imepungua mwilini kipimo hiki kinaweza kikakupa viashiria ni kwanini damu inapungua, mfano kama ni upungufu wa madini chuma n.k
Kwa kifupi kabisa bila kwenda ndani kabisa hivi ndo vitu ambavyo Full blood picture inaonyesha na sio magonjwa yote mwilini kama ambavyo jina la kipimo linasema au unaweza kudhani linamaanisha.
Mwisho kabisa , majibu na usahihi wa kipimo hiki utategemea na ubora wa machine ya kupima kipimo hiki, ubora wa kemikali “ reagent “ inayotumika kupima, uhodari wa mtu anayekutafsiria majibu ya kipimo hiki maana sio kila mtu anaweza kusoma na kutafsri kwa usahihi kabisa kipimo hiki.
Shukrani za kipekee sana kwako ambaye umesoma mpaka hapa chini, nakutakia afya njema kabisa katika mapambano yako ya kila siku.