==
Ndugu Wananchi, akizungumza na wanahabari, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mrindoko, amesema:
“Chini ya Rais wa Awamu ya Sita, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkoa wa Katavi umepokea jumla ya Shilingi Bilioni 41.628 kwa sekta ya afya katika kipindi cha 2020/21–2024/25. Fedha hizi zimetumika katika ujenzi na ukarabati wa hospitali, vituo vya afya, zahanati, ununuzi wa dawa na vifaa tiba pamoja na kuimarisha huduma za kibingwa. Hatua hii imeimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi, kupunguza vifo vya kina mama na watoto, na kuongeza upatikanaji wa dawa hadi wastani wa asilimia 94.”
1. Mchanganuo wa Mapokezi ya Fedha za Afya 2020|2021–2024|25
| Na. | Mradi / Sekta | Fedha (TZS) |
|---|---|---|
| 1 | Hospitali ya Rufaa ya Mkoa | 18,386,053,967.19 |
| 2 | Hospitali 4 za Wilaya | 10,370,000,000.00 |
| 3 | Miradi ya UVIKO 19 (ICU & EMD) | 1,200,000,000.00 |
| 4 | Miradi ya Tozo | 1,750,000,000.00 |
| 5 | Ukarabati Hospitali Kongwe (Mpanda MC) | 900,000,000.00 |
| 6 | Ukarabati & Ujenzi wa Zahanati 36 na Vituo 20 | 6,721,961,459.59 |
| 7 | Vifaa tiba vya Hospitali | 1,200,000,000.00 |
| 8 | Vifaa tiba vya Vituo vya Afya | 600,000,000.00 |
| 9 | Vifaa tiba vya Zahanati | 500,000,000.00 |
| — | Jumla | 41,628,015,426.78 |
2. Ukuaji wa Miundombinu ya Afya
| Kipengele | Hali 2021 | Hali 2025 | Ongezeko |
|---|---|---|---|
| Jumla ya Vituo vya Afya | 102 | 161 | 59 |
| Zahanati | 80 | 127 | 47 |
| Vituo vya Afya | 17 | 28 | 11 |
| Hospitali za Wilaya | 0 (ukamilishaji haujakamilika) | 4 | 4 |
| Watumishi wa Afya | 898 | 1,754 | 856 |
| Magari ya Wagonjwa (Ambulance) | 10 | 17 | 7 |
3. Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
- Kukamilisha Wing A (Huduma za OPD, Mama na Mtoto, Radiolojia, vyumba vya upasuaji).
- Ujenzi wa jengo la Dialysis (umekamilika 100%, huduma zinaendelea).
- Ujenzi wa ICU na EMD (Huduma za dharura).
- Ujenzi wa nyumba ya mtumishi.
- Ununuzi wa vifaa vya kisasa: CT-Scan na mashine 2 za Digital X-Ray.
- Huduma za kibingwa zinazotolewa sasa: Upasuaji, mifupa, afya ya uzazi, ENT (Sikio-Pua-Koo), magonjwa ya ndani, na huduma za dharura.
4. Upatikanaji wa Dawa na Huduma
| Mwaka | Fedha za Ununuzi wa Dawa (TZS) | Wastani wa Upatikanaji |
|---|---|---|
| 2021 | 2,980,556,000.00 | — |
| 2024 | 3,380,560,000.00 | 94% (ongezeko la 11.8%) |
5. Huduma za Dharura (CEmONC)
- Vituo vyenye uwezo wa kutoa huduma za dharura kwa wajawazito (upasuaji): kutoka 8 (2021) hadi 14 (2025).
- Idadi ya wajawazito waliojifungua katika vituo vya afya: kutoka 40,269 (2021) hadi 48,322 (2025).