Mac Alpho
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 13,953
- 27,825
[emoji23][emoji23][emoji23]Hongera sana Rais Samia Suluhu kwa Hotuba bora kabisa ya karne
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23][emoji23]Hongera sana Rais Samia Suluhu kwa Hotuba bora kabisa ya karne
Mbona huwa ziko juu sana unakabidhiwa na Bible na kutambulishwa wazazi wa ubatizoHotuba za kipaimara
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]Lissu mtu na nusuDuh! Mbona body language ya mama haiko sawa, kama kapaniki hivi. Au kafuatilia hotuba ya TL?
unachekesha aiseeHongera sana Rais Samia Suluhu kwa Hotuba bora kabisa ya karne
Nenda kapitie hotuba ya Lissu uone alivyozungumzia suala la mbolea halafu njoo kwa Samia alivyozungumzia kuhusu mbolea, halafu walete wakulima waichambue, ndio utaelewa tuna rais wa kiwango gani cha chini cha upeo.Nimependa Rais alivyozungumzia bei ya mbolea.
Hotuba ya Tundu Lisu ni kama ya kaka mkuu wakati wa kufunga shule ya sekondari!
Yaani kwa kweli mi naona hotuba ya ajabu ajabu tu! Hajataja hata mkakati wake wa kuendeleza miundo mbinu!Rais Samia Suluhu anahutubia Taifa kuuga mwaka 2021 na ameanza na mfumuko wa bei.
Rais Samia ametaja changamoto ya mfumuko wa bei ulioshuhudiwa 2021 kuwa ni zao la ongezeko la bei za mafuta kwenye soko la dunia. Aidha Rais Samia amelitaja janga la COVID19 kuwa sababu nyingine ya ongezeko la bei za bidhaa
Rais Samia ameongelea athari za mvua zilizozidi kiasi.
Mwaka 2022 inategemewa kupata mbolea ambayo mkulima bei yake ameizoea. Rais Samia pia ameiongelea sekta ya utalii kuathiriwa na Uviko 19 na mwezi Disemba imeweza kujikongoja pamoja na hatua zilizochukuliwa.
=======
HOTUBA YA MHESHIMIWA SAMIA SULUHU
HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA WAKATI WA KUPOKEA KOMBE LA
UBINGWA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI
(CECAFA)KWA VIJANA WENYE UMRI YA CHINI YA MIAKA 23 NA KUWAPONGEZA WASHIRIKI WA
MASHINDANO YA OLIMPIKI MWAKA 2021
IKULU, DAR ES SALAAM, TAREHE 21 AGOSTI, 2021
Mheshimiwa Innocent Bashungwa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo;
Mheshimiwa Pauline Gekul, Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo;
Mheshimiwa Stanslaus Nyongo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii;
Dkt. Hassan Abbas, Katibu Mkuu, Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo;
Bi. Neema Msita, Kaimu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT);
Viongozi wengine wa Serikali mliopo;
Viongozi wa Vyama na Mashirikisho ya Michezo nchini (TFF, Bodi ya Ligi, Kamati ya Olimpiki na Shirikisho la Riadha);
Wachezaji wetu wa Timu ya Taifa Chini ya Miaka 23;
Wana-Riadha wetu mlioshiriki Michezo ya Olimpiki;
Ndugu Wana-Habari, Mabibi na Mabwana:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SALAMU
• Nianze kwa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutujalia uhai na kutuwezesha kukutana hapa. Tumekutana hapa,
kwanza, ili kuipongeza Timu yetu ya Taifa ya Chini ya Umri wa Miaka 23 kwa kuchukua Ubingwa wa Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati pamoja na wana-riadha wetu walioshiriki Mashindano ya
Olimpiki hivi karibuni.
• Hii sio mara yangu ya kwanza kukutana na Timu ya Taifa. Nakumbuka, mwaka 2017, wakati nikiwa Makamu wa Rais, nilipokea Kombe la Ubingwa wa Afrika Mashariki kwa Timu ya Vijana chini ya Miaka
17, Serengeti Boys. Kwa hiyo, hii ni mara ya pili kukutana na Timu zetu za Taifa zilizofanya vizuri ili
kuwapongeza.
Lakini, niseme tu, mbali na
kuzipongeza, tumekutana hapa ili kuzipa hamasa Timu zetu za Taifa za michezo mbalimbali kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya kimataifa na kulitangaza
vyema jina la nchi yetu.
RAMBIRAMBI
• Kabla sijaendelea zaidi, napenda kutumia fursa hii kutoa pole nyingi kwa familia ya mpira wa miguu Tanzania kwa kuondokewa na wadau wenu. Kwanza, aliyekuwa Mwenyekiti wa BMT na pia FAT, hivi sasa TFF, Marehemu Mzee Said El Maamry; na pili Mchambuzi wa Michezo Mashuhuri na Mtangazaji wa
Mpira wa TBC, Marehemu Alex Kashasha.
• Naomba tusimame kwa dakika moja tuwakumbuke. Mwenyezi Mungu azipumzishe roho zao mahali pema
peponi. Amina.
UMUHIMU WA MICHEZO
• Michezo ni sekta kubwa ambayo inaendelea kukua kwa kasi ulimwenguni. Kwa mujibu wa Jarida la Forbes, sekta hii inakadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani trilioni 1.3 na kutoa ajira nyingi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.
• Vilevile, michezo inasaidia kutangaza nchi. Wapo watu wengi duniani waliifahamu nchi yetu kwenye miaka ya 1970 na 1980 kupitia wana-Riadha wetu maarufu, Filbert Bayi, Selemani Nyambui na Juma Ikangaa; na nafahamu wengine wameifahamu nchi yetu kupitia Wanariadha wetu, Alphonce Simbu pamoja na mwanangu Failuna Abdi ambao walituwakilisha
kwenye Olimpiki ya Tokyo; na wengine kupitia Timu zetu za Taifa, hususan za Vijana na Wanawake, ambazo
zimefanikiwa kuchukua Makombe mbalimbali.
• Kwa upande mwingine, wapo Watanzania wengi
wameifahamu Argentina kupitia Maradona na Messi; Brazil kupitia Pele, Ronaldo na Ronadinho; Ethiopia kupitia Gebre Selassie, Liberia kupitia George Weah, Philipinnes kupitia Manny Pacquiao; Jamaica kupitia Usain Bolt. Hii inaonesha umuhimu wa michezo katika
kuitangaza nchi.
• Zaidi ya hapo, kama sote tujuavyo, michezo
inaburudisha, inajenga urafiki na halikadhalika mshikamano kwenye Taifa. Sambamba na hayo,
michezo ni afya. Mathalan, hivi sasa dunia inakabiliwa
na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza
(moyo, figo, kisukari, saratani au kansa, n.k.), ambapo mwaka 2016 yalisababisha asilimia 71 ya vifo. Kwa hapa nchini, takwimu zinaonesha kwamba, mwaka 2017, magonjwa yasiyoambukiza yalisababisha
asilimia 33 ya vifo. Ili kupunguza magonjwa haya, wataalamu wanatushauri kushiriki kwenye michezo au kufanya mazoezi. Tunatakiwa kufanya mazoezi kwa
angalau nusu saa kwa siku mara tatu kwa wiki.
PONGEZI
Waheshimiwa Viongozi na Wanamichezo mliopo;
• Kama mnavyofahamu, wakati nikilihutubia Bunge
tarehe 22 Aprili, 2021 niliahidi kwamba Serikali ya Awamu ya Sita itaendeleza juhudi za kuboresha na kukuza sekta ya michezo nchini. Ni kwa msingi huo, leo nimefurahi sana kuwepo mahali hapa kupokea Kombe hili la Ubingwa wa Afrika Mashariki kwa Vijana wenye Umri Chini ya Miaka 23. “Kila safari
huanza na hatua moja“.
• Hivyo basi, nawapongeza sana vijana wetu kwa
kutuletea kombe hili. Ni imani yangu kuwa, ushindi huu utaleta hamasa kwa Timu zetu nyingine za Taifa kucheza kwa bidii. Na katika hilo, natambua kuwa Timu zetu za Taifa za Mpira wa Miguu za Wanaume (Taifa Stars) na Wanawake (Twiga Stars) zipo kwenye maandalizi ya mashindano mbalimbali. Taifa Stars inajiandaa na Michezo ya Kufuzu kwa Mashindano ya Kombe la Dunia ya Mwaka 2026; na wanangu Twiga Stars wanajiandaa kushiriki Mashindano ya COSAFA
nchini Afrika Kusini.
• Vilevile, Timu ya Vijana ya Mchezo wa Wavu inajiandaa kwa Mashindano ya Afrika; na
halikadhalika, mwaka huu, mwezi Novemba, nchi yetu itakuwa mwenyeji wa Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa watu wenye Ulemavu. Niwasihi sana viongozi wa michezo kuwaandaa na kuwalea vizuri vijana wetu ili watuwakilishe vyema kwenye mashindano hayo na kuipeperusha vizuri Bendera yetu. Wachezaji wetu watapata hamasa na ari ya kucheza kwa kujituma
endapo watatunzwa na kulelewa vizuri.
MIPANGO YA SERIKALI KUKUZA MICHEZO
Ndugu Viongozi wa Michezo;
Ndugu Wachezaji, Ndugu Wana-Habari, Mabibi na Mabwana:
• Serikali imedhamiria kwa dhati kabisa kukuza na
kuendeleza sekta ya michezo nchini. Na katika hilo, kama alivyoeleza Mheshimiwa Waziri anayehusika na masuala ya Michezo, tayari tumeanzisha Mfumko wa Maendeleo ya Michezo ili kusaidia Timu za Taifa. Kwa kuanzia, Mwaka huu wa Fedha, tumetenga shilingi
bilioni 1.3; lakini tutaendelea kuutunisha Mfuko huo.
• Sambamba na hayo, tumeondoa VAT kwa ajili ya nyasi bandia ili kuwezesha viwanja vyetu kuboreshwa. Tutaendelea pia kuangalia maeneo ya vifaa vingine vya michezo, kama ilivyoombwa. Zaidi ya hapo, hivi sasa tunajenga Kituo cha Kulea Vipaji vya Michezo (sports
academy) kwenye Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya (Mwanza), na tutaendelea kujenga maeneo mengine. Aidha, tumepanga kujenga viwanja vitatu vya mazoezi (Dar es Salaam, Dodoma na Geita).
• Vilevile, tumeanza kufanya tathmini ya kujenga Kituo cha Kisasa cha Michezo na Kazi za Sanaa za Ndani (Arts and Sports Arena), ambacho ni ombi la muda mrefu la wanamichezo nchini. Kituo hicho sio tu
kitasaidia kuikuza michezo nchini bali pia kitaiwezesha
nchi yetu kuandaa michezo mikubwa ya kimataifa, hususan mpira wa pete, mpira wa wavu, mpira wa kikapu na bila kusahau ndondi. Tunakusudia kujenga vituo viwili; kimoja hapa Dar es Salaam, na kingine
kule Dodoma; lakini kwa awamu.
• Nitumie fursa hii pia kuwapongeza Wizara kwa
kushirikiana na Wizara nyingine kwa kurejesha upya hamasa ya michezo ya shule za msingi na sekondari na pia mipango yenu ya kufufua Mashindano ya Taifa
itakayoshindiwa na mikoa kwenye michezo
mbalimbali. Aidha, nawapongeza kwa kubuni wazo la kuanzisha Tamasha la Kila Mwaka (Tanzanite Women Sports Festival). Hatua hizi, naamini zitasaidia kukuza sekta ya michezo nchini.
• Lakini niseme, pamoja na jitihada hizi za kukuza
michezo, kuna haja ya kuwaangalia kwa jicho la pekee
wanawake, hususan wa mpira wa miguu. Leo
tumejisifu hapa kwamba wameleta makombe manne; lakini sisi kama Taifa tujiulize tumewafanyia nini? Hivyo basi, nitoe rai kwamba, Mfuko wa Maendeleo ya Michezo ulioanzishwa, uangalie maslahi au hatma ya baadaye ya wachezaji wetu, hususan wa Timu za Taifa za Wanawake ili wasihangaike sana baada ya kustaafu. Nakumbuka, Timu yetu ya Taifa ilipofuzu kushiriki Mashindano ya Kombe la Afrika, tuliwapatia wachezaji
viwanja kule Dodoma.
Lakini, kwa Timu za Wanawake, licha ya kuleta makombe, hatujawahi kuwafanyia chochote. Hivyo, ni vyema tulitafakari suala hili. Sisemi hivyo kwa kuwatetea wanawake bali kwa kutetea haki.
WITO
• Kabla ya kuhitimisha, naomba nitoe wito kwa Wizara, Mashirikisho na Vyama vya Michezo, Vilabu pamoja na wanamichezo wenyewe, kujipanga vizuri. Na hapa nina maneno kidogo kuhusu Kamati ya Olimpiki. Mwanzoni mwa hotuba yangu nimewapongeza
wanariadha wetu watatu walioshiriki Mashindano ya Olimpiki nchini Japan hivi karibuni. Hata hivyo, ukweli ni kwamba, kwa Taifa kubwa kama letu, kuwakilishwa na wachezaji watatu tena wa mchezo
mmoja ni aibu.
• Hivyo basi, natoa changamoto kwenu kujifanyia
tathmini ili kwenye Mashindano yajayo
yatakayofanyika Paris mwaka 2024 ushiriki wetu uwe mkubwa kwa idadi ya wanamichezo na sio viongozi; lakini pia tupate ushindi. Tanzania ina wanamichezo
wengi, hivyo, tujipange vizuri, ikiwemo kwa
kushirikiana na taasisi mbalimbali (majeshi, mikoa)
tunaweza kupata wachezaji wengi wazuri
watakaotuwakilisha na kutuletea ushindi. Hiyo ndiyo
changamoto ninayoitoa kwa Kamati ya Olimpiki
pamoja na viongozi wa michezo mingine.
• Sambamba na hilo, napenda kuungana na Mheshimiwa Waziri wa Michezo katika kuhimiza utawala bora kwenye sekta ya michezo. Jitihada zetu kukuza michezo hazitafanikiwa endapo suala la utawala bora halitapewa kipaumbele kwenye Vyama, Mashirikisho
na Vilabu vya Michezo. Hivyo, nawahimiza
kuimarisha utawala bora kwenye michezo. Mkifanya hivyo, mtatuhamasisha na sisi tuliopo Serikalini kushughulikia changamoto mliizotueleza.
• Na katika hilo, naiagiza BMT kulisimamia suala hili. Kwa bahati nzuri, Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT ni mwanamke; na kama tujuavyo, wanawake wakipewa jambo hawashindwi. Hivyo, naamini utakwenda kutumia maarifa yako kulisimamia suala hili. Sambamba na hilo, natoa wito kwa wanamichezo
kupata chanjo ya Corona ili kujilinda na ugonjwa huo lakini pia kuwawezesha kushiriki michezo nje ya nchi.
• Naihimiza pia sekta binafsi ya ndani na kutoka nje
kuwekeza kwenye michezo hapa nchini. Kama
nilivyosema awali, mchezo ni biashara kubwa duniani. Na hapa, naipongeza Kampuni ya AZAM kwa jinsi inavyojitahidi kuwekeza kwenye mchezo wa mpira wa miguu pamoja na ndondi (wenyewe wanaita vitasa).
Naziomba kampuni nyingine ziige mfano.
• Vilevile, natoa wito kwa vijana na pia wazazi kuwahimiza watoto wao kushiriki kwenye michezo. Kama nilivyosema, mbali na kwamba michezo ni ajira na biashara, michezo ni afya na pia michezo inasaidia
kuwajenga watoto wetu kwenye maadili mema. Na
kwa bahati nzuri michezo ipo mingi (mpira wa miguu,
pete, wavu, kikapu, riadha, mbio za baiskeli, kuogelea,
tennis, kuruka juu, sarakasi, n.k.).
• Mabibi na Mabwana; mwakani kutafanyika Mashindano ya Kombe la Dunia nchini Qatar. Hapa na Qatar sio mbali, hivyo, naamini tukijipanga vizuri nasi tunaweza kunufaika na Mashindano hayo. Kwa hiyo, natoa wito kwa wadau wa sekta ya umma na binafsi kujipanga ili kutumia fursa hiyo. Wizara ya Utalii wanaweza kutengeneza special packages ili kuwavutia watakaokwenda kuangalia mashindano hayo
kutembelea vivutio vyetu; na kwa Wizara ya Viwanda na Biashara na wafanyabiashara wanaweza kuangalia fursa ya kuuza bidhaa zetu nchini Qatar (nyama,
samaki, korosho, mchele, matunda, n.k.)
HITIMISHO
• Nihitimishe kwa kurudia kuwapongeza vijana wetu kwa kuchukua Kombe la CECAFA pamoja na wana-
riadha wetu waliotuwakilisha kwenye Mashindano ya Olimpiki mwaka huu. Nimekuja na zawadi ndogo kwenu kwa ajili ya kuwapa hamasa zaidi. Aidha, nazihimiza Timu za michezo mingine zitakazoshiriki kwenyemashindano ya kimataifa, vikiwemo vilabu, kujiandaa vyema na kucheza kwa kujituma ili
kupeperusha vyema bendera ya nchi yetu.
• Mwisho kabisa lakini sio kwa umuhimu, wakati tukiwa tumekaa pale mezani, Rais wa TFF, Bwana Wallace Karia, alinidokeza kuhusu ombi la Udhamini wa Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati kwa Timu za
Taifa za Wanawake. Alinishawishi sana kwa kutoa mfano wa Mashindano ya Kagame Cup, nami baada ya kutafakari, nimeamua kukubali ombi hilo; ambapo
nitatafuta baadhi ya watu nishirikiane nao.
• Baada ya kusema hayo.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
“Ahsanteni sana kwa Kunisikiliza”
Zile hela za kovid wangezichepusha kwenye pembejeo za kilimo. Madarasa yangejengwa kwa kutumia tozo.Nenda kapitie hotuba ya Lissu uone alivyozungumzia suala la mbolea halafu njoo kwa Samia alivyozungumzia kuhusu mbolea, halafu walete wakulima waichambue, ndio utaelewa tuna rais wa kiwango gani cha chini cha upeo.
Wakulima wote wa Tanzania wanataka bei ya mbolea iwe chini, sio blah blah za Samia.
... kwa mlioisikiliza, kazungumzia Katiba Mpya?
... Katiba Mpya imezungumziwa kuanzia dakika ya ngapi nisikilize?sikiliza hiyo clip
Imeegemea sana upande wa uwezo binafsi!!Tuache utani, mama hana wataalam wazuri wa uandishi wa hotuba maalumu kama hii ya leo.
Anyway #Kaziiendelee
sikiliza hiyo clip
Yule maza anaogopa hata kutaja neno katiba mpya, akijaribu hata kutaja moyo wake unakwenda mbio kwa woga.... kwa mlioisikiliza, kazungumzia Katiba Mpya?