Full Text: Taarifa ya Luhaga Mpina kuhusu Tume ya Chande ya Kuchunguza yaliyotokea 29.10.2025

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
BURIANI MASHUJAA WETU YANA MWISHO HAYA

Bonyeza HAPA kupakua Hotuba yake

Hapa Chini nimeweka Video ni Mapendekezo yake..

MAONI NA MAPENDEKEZO KWA UFUPI

Baada ya kufanya uchambuzi hapo juu ninatoa Maoni na mapendekezo kama ifuatavyo:-

(i) Kuundwa Tume Huru chini ya Umoja wa M ataifa (UN), Jumuiya ya Madola (Commonwealth) na Umoja wa Ulaya (EU) itakayohusisha makundi yote muhimu ya ndani na ya nje ya nchi kufanya uchunguzi kwa uwazi na bila upendeleo wa upande wowote.

(ii) Kulipa kifuta machozi kwa familia zote za marehemu na fidia na vifaa saidizi kwa watu wote waliopoteza viungo vya mwili. Pia kuwarejesha watu 245 ambao hawajulikani walipo hadi sasa.

(iii) Rais, Msajili wa Vyama vya Siasa, INEC , AG, Mahakama na wengine waliohusika wawajibike kwa kashfa ya kusababisha vifo vya watu zaidi ya 518 na majeruhi zaidi ya 2,390 wasio na hatia il i kuliponya taifa na 66 kudumisha Uwajibikaji (naungana na Maoni ya Tume kuwa asiwepo mtu wa kutolewa kafara -Sacrificial Lamb)

(iv) Vyombo vya Dola vikiongozwa na Afande CDF vimtake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na aliyekuwa Waziri wa Fedha (Waziri Mkuu wa sasa) waeleze yalipo matrilioni ya fedha za um ma yaliyoibwa na kufujwa, pia vyombo hivyo vi watake Viongozi hao kuweka wazi jedwali la mikopo na mikataba y ote ya raslimali iliyoingiwa kwa siri katika kipindi cha uongozi wao wa miaka 5 iliyopita. Aidha na ifahamike kuwa jukumu la kwanza la msingi la Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(v) Tume huru ya kimataifa itakayoundwa pamoja na mambo mengine ichunguze ukwasi wa baadhi ya Viongozi wanaotuhumiwa kuiba na kuficha fedha za umma nje ya n chi na kusaidia kutaifisha mali na fedha hizo na kuzirejesha nchini na hii ifanyike kwa kuhusisha Taasisi zinazoaminika kimataifa za uchunguzi wa fedha (Accredited Financial Investigators-AFI).

(vi) Watanzania wote wazalendo na wenye mapenzi mema na nchi yetu walioko ndani na nje ya nchi wanaombwa kufichua mitandao ya wizi na kuweka wazi nyaraka zinazohusu ufisadi ili umma uweze kuchukua hatua stahiki za uwajibikaji.

(vii) Uchaguzi wa tarehe 29 Oktoba 2025 ufutwe na kutangazwa uchaguzi mpya ili kuwapa nafasi wananchi kuchagua Viongozi wanaowataka katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani ili kurejesha umoja, mshkamano, amani na utulivu nchini.

(viii) Kesi ya kupinga kuenguliwa kugombea Urais iliyopo Mahakama ya Rufaa kati yangu mimi Luhaga Joelson Mpina na ACT Wazalendo dhidi ya INEC na AG . Pia kesi kati yangu mimi Luhaga Joel son Mpina na ACT Wazalendo dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (RPP) na AG. Aidha kesi nyingine ni kati ya ACT Wazalendo dhidi ya INEC na AG kuhusu uteuzi wa wabunge wa Viti Maalum zisikilizwe na kuamuliwa haraka ili kutenda haki na kuwa rejea muhimu kat ika safari ya ujenzi wa demokrasia nchini.

(ix) Wakati shauri likiwa Mahakama ya Rufaa kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa C hief Justice, Mheshimiwa Masaju ajitokeze hadharani kuueleza umma wa watanzania na dunia kwa ujumla status yangu ni ipi kwa sasa kwani nimekaa kwenye ugombea wa Urais wa kudumu na endelevu muda mrefu, kwa kuwa yeye ndiye aliye na kesi yangu na yeye ndiye aliyeshuhudia kiapo cha Mtawala katika Kambi ya Kijeshi badala ya Uwanja wa Jamhuri Dodoma kama ilivyozoeleka miaka yote.

(x) Mahakama iache kutumika kisiasa na kuwa sehemu ya kutakatisha uhalifu na kuwanyima haki wenye haki na badala yake ijijenge upya kama ilivyokuwa enzi za Jaji Mkuu, Hayati Fransis Lucas Nyalali.

(xi) Liundwe Baraza la Taifa la Katiba ambalo litateuliwa na wananchi wenyewe ba dala ya Bunge la Katiba linaloteuliwa na Rais , Katiba ya Wananchi haiwezi kuandikwa na wateule wa Rais na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi. Ripoti ya Tume ya Jaji Warioba itumike kama rejea na funzo kubwa. Katiba mpya ipatikane mapema mwaka 2027 badala ya m waka 2028 ilivyopendekezwa na Tume ya Jaji Chande.

(xii) Vyuo vikuu vya nchi yetu viruhusu midahalo ya Wasomi ambayo italiokoa taifa kama tulivyoshuhudia hivi karibuni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Chuo Kikuu ch a Havard Ma rekani anatoa mhadhara kwenye mdahalo lakini chuo chake midahalo haifanyiki kama ilivyozoeleka miaka ya nyuma katika u kumbi wa Nkrumah (Nkrumah Hall) ambao ndio uliokuwa chemchem ya mageuzi ya kifikra nchini. Mwisho nimalizie kwa kutoa masikiti ko yangu juu ya Raslimali za taifa letu ambazo tumezilinda kwa machozi, jasho na damu na wivu mkubwa tangu Uhuru mwaka 1961, leo zinauzwa na kumilikiwa na watu binafsi tena kwa siri. Fedha za umma zinatapanywa na kupelekea huduma za Kijamii na Kiuchumi kwa wananchi kudorora. Kwa mwendo huu watoto na wajukuu wetu watakuja kurithi nini?

Kwa nchi yetu ilipofikia kwa sasa lawama hizi tunapaswa tuzibebe watanzania wote kwa kutotimiza Wajibu wetu kikamilifu tuliopewa na Katiba na kuingia kwenye mtego wa ushabiki uliopitiliza wa Vyama vya Siasa na michezo, Vyama vya upinzani kukosa umoja na mshikamano na mambo ya kung‟ata na kupuliza hivyo kushindwa kutimiza wajibu wao kikamilifu katika kuisimamia Serikali.

JUNI, 2026

YALIYOMO KWENYE TAARIFA HII

1. UTANGULIZI ....................................................................................................... 1
2. CHANZO NA VICHOCHEO VYA MAANDAMANO ...................................................... 3
3. UHALALI WA VITENDO VYA SERIKALI WAKATI WA KUTULIZA GHASIA ................ 19
4. VITENDO VYA SERIKALI BAADA YA MATUKIO YA MAUAJI YA OKTOBA 2025 ........ 24
5. UHALALI WA MAANDAMANO YA OKTOBA 2025 .................................................. 31
(I) Madai ya kuwa Waandamanaji hawakutoa taarifa polisi................................. 32
(II) Madai ya kwamba eti Waandamanaji walizuia haki ya mpiga kura .................. 32
Upande wa CCM. ................................................................................................. 33
Upande wa ACT Wazalendo .................................................................................. 34
Upande wa CHADEMA .......................................................................................... 37
Mazingira ya Uchaguzi .......................................................................................... 38
(III) Madai ya kwamba Waandamanaji walikuwa na silaha (Bunduki) .................... 41
(IV) Madai ya kwamba Maandamano yalihatarisha usalama wa Taifa .................... 42
(V) Madai ya Waandamanaji walikuwa wafuata mkumbo .................................... 43
5. MASUALA YA KIUCHUMI.................................................................................... 44
6. JUMUIYA ZA KIMATAIFA ................................................................................... 48
7. UWAZI NA UWAJIBIKAJI KUHUSIANA NA MAUAJI YA OKTOBA 2025 .................... 49
8. HITIMISHO ...................................................................................................... 53
9. MAONI NA MAPENDEKEZO ................................................................................ 65

1

TAARIFA KWA UMMA YA NDG. LUHAGA JOELSON MPINA,
KUHUSU UCHAMBUZI WA MUHTASARI WA RIPOTI YA
TUME YA RAIS YA KUCHU NGUZA MATUKIO YA GHASIA
NA UVUNJIFU WA AMANI YALIYOTOKEA WAKATI NA
BAADA YA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2025 , LEO TAREHE
1 JUNI 2026, DAR ES SALAAM.

1. UTANGULIZI
Ndugu Waandishi wa Habari, kwanza nianze kwa kumshukuru
Mungu mwingi wa Rehema muumba mbingu na nchi kwa
kutujalia uhai na afya njema kuweza kukutana siku ya leo tarehe
1 Juni 2026 hapa jijini Dar es Salaam.
Pili nichukue nafasi hii kutoa pole n yingi kwa Familia ya Mzee
Joseph Magufuli Marco Nyahinga na watanzania kwa ujumla
kufuatia kifo cha Mama Suzana Ngolo Mussa Magufuli mama
yake mzazi na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea tarehe 25 Mei 2026
na kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele Tarehe 29 Mei
2026 huko Chato, Geita. Heri tumbo lililokuzaa na matiti
uliyonyonya Dk. Magufuli pumzika kwa amani Mama yetu kipenzi
umetoa mchango mkubwa kwenye Taifa.
Aidha niwashukuru ni nyi Ndugu Waandishi wa H abari kwa nafasi
hii mliyonipa ili niweze k utoa m aoni na mapendekezo yangu
baada ya kufanyia uchambuzi muhtasari wa Ripoti Tume ya Rais
ya kuchunguza matukio ya ghasia na uvunjifu wa amani
yaliyotokea wa kati na baada ya uchaguzi mkuu O ktoba 2025
iliyoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Mohamed
Chande Othman iliyowasilishwa kwa Rais tarehe 23 Aprili 2026.

2

Mtakumbuka kuwa m namo tarehe 21 Januari 2026 nilipokea
barua rasmi ya mwaliko wa kuhudhuria mbele ya Tume ya Jaji
Chande kwa ajili ya majadiliano tarehe 31 Januari 2026 ,
Niliwajibu Tume kwa barua ya tarehe 30 Januari 2026 kuwa
sitaweza kuhudhuria kikao hicho kwa kuwa tume hiyo sio huru na
ripoti yake hai taaminika kitaifa na kimataifa. Msimamo huu pia
ndiyo ulikuwa msimamo wa Chama changu cha ACT Wazale ndo
na hata Vyama vingine kama CUF na CHADEMA. Muhtasari wa
ripoti ya Tume ya Jaji Chande umedhihirisha ukweli wa kile
tulichokiamini awali.
Tangu kuwasilishwa kwa ripoti ya Jaji Chande, nimekuwa
nikipokea simu nyingi za wananchi na Waandishi wa Habari
kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi wakitaka kujua
maoni na mapendekezo yangu kuhusu ripoti ya Tume ya Jaji
Chande ambapo pamoja na ukweli kwamba chama changu cha
ACT Wazalendo kimeshatoa matamko y a chama ya Tarehe 9
Novemba 2025, Tarehe 19 Januari 2026 na Tarehe 4 Mei
2026 ambapo matamko yote nayaunga mkono.
Lakini na mimi kama mwanachama niliyepewa dhamana ya
kupeperusha bendera ya Chama cha ACT Wazalendo kuwania
nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi yetu kuwa mgombea
Urais nikaona leo ni siku muafaka ya mimi kutoa Maoni yangu
kuhusiana na Ripoti ya Jaji Chande.
Pia natambua juhudi za wananchi na Taasisi mbalimbali
waliojitokeza hadharani kutoa Maoni yao kuhusu ripoti ya Jaji
Chande akiwemo Jaji Joseph Sinde Warioba, Prof. Anna Tibaijuka,

3

Mzee Samweli Kassori, Wakili Peter Madeleka, TLS, LHRC, Asasi
za Kiraia 14, UDASA na Chama cha CHADEMA.
Kabla sijaanza kuchambua kipengele kwa kipengele yako mambo
ya kiujumla kama ifuatavyo:-
(i) Muhtasari wa Ripoti ya Tume ya Jaji Chande kwa
sehemu kubwa umeja a simulizi badala ya ushahidi wa
vielelezo na uthibitisho wa kisayansi, u na takwimu na
taarifa zinazokinz ana na u meacha kuchambua na
kufanya utafiti wa masuala muhimu ambayo jamii
ilikuwa na shauku kubwa kuyafahamu.

(ii) Tume kwa kiasi kidogo imezingatia maoni ya wananchi
na imeyakubali maudhui ya tathmini ya uchaguzi
niliyoitoa mnamo tarehe 6 Disemba 2025 yenye kichwa
cha habari “Taarifa kwa Umma ya Ndugu Luhaga
Joelson Mpina kuhusu Shauri la kesi ya Rufaa, Uchaguzi
Mkuu na Maandamano ya tarehe 29 Oktoba 2025”
2. CHANZO NA VICHOCHEO VYA MAANDAMANO
Muhtasari wa Ripoti ya Jaji Chande umebainisha mambo 5 yenye
vipengele 20 kuwa ndiyo chanzo kikuu cha ghasia na machafuko
ya tarehe 29 Oktoba 2025 , katika hili nawapongeza Tume kubaini
kuwa utendaji dhaifu wa Serikali ya awamu ya 6 ndiyo chanzo
kikuu cha machafuko na vifo Oktoba 2025, asante sana Tume
kwa kuona na kuweka wazi ukweli huo ambao umefichwa kwa
gharama kubwa kwa kipindi miaka 5 kwa kampeni za u tapeli za
4Rs, “Mama Hana Deni, Mama hatukudai” . Hakika mwisho
wa ubaya ni aibu na lakuvunda halina ubani . Wakati
naipinga kampeni hii haramu hadharani ndani na nje ya Bunge

4

nilipigwa vita na kutengenezewa chuki kubwa na baadhi ya
Viongozi waandamizi wa Chama cha Mapinduzi na Serikali. Leo
Tume ya Jaji Chande imethibitisha na mmewasikia wabunge huko
Dodoma nao wanalia hawajui fedha za ujenzi wa barabara na
miradi mingine zimekwenda wapi.
Hivyo nami nakubaliana na Tume ya Jaji Chande kama ifuatavyo:-
2.1 Yapo masuala ya kisiasa yanayohusishwa na madai ya Katiba
Mpya, D emokrasia katika mfumo wa Vyama vingi vya Siasa,
malalamiko ya kuingiliwa ndani ya Vyama vya Siasa, madai ya
maboresho ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na mfumo mzima
wa uchaguzi. Kwa mfano:-
(i) Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Msaji li wa
Vyama vya Siasa (RPP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali
(AG) na Mahakama zinatumika na Chama cha
Mapinduzi na mtawala kuwaengua wagombea wa
upinzani wa nafasi za Rais, Wabunge na Madiwani kwa
mabavu na kinyume cha Sheria.

(ii) Katiba na Sheria za uchaguzi zinakandamiza Vyama vya
upinzani ikiwemo kuweka masharti ya kutoping wa
matokeo ya uchaguzi wa Rais m ahakamani na kuipa
nguvu Tume kuwa rufaa ya mwisho katika mapingamizi
ya nafasi ya Rais ili kufanikisha kuwaengua wapinzani.
Kifungu cha 37 (6) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais,
Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024. Kuandaa
kanuni za maadili zinazokinzana hadi na Katiba ya nchi.
2.2 Masuala ya Kiuchumi yanayojumuish a ugumu wa maisha,
ukosefu wa ajira na kukosekana kwa usawa katika fursa za ajira

5

na za Kiuchumi, mazingira ya biashar a na uwekezaji yasiyo r afiki,
utitiri wa kodi na tozo na mfumo usio rafiki wa utozaji na
ukusanyaji wa mapato.
Ni kweli kabisa wananchi wana hasira kubwa na Serikali ya
awamu ya 6 kwa sababu zifuatazo:-
(i) Kuhusu kupanda kiholela kwa bei za bidhaa na huduma
muhimu za wananchi kama nishati ya mafuta, umeme,
maji, gesi, mbolea, sukari, gharama za matibabu,
bidhaa za afya, vifaa vya ujenzi, pembejeo, mbegu,
Nauli nk. Kwa mfano hivi sasa licha ya kuwepo akiba ya
mafuta yanayotosheleza miezi 3 ijayo lakini Serika li
imeruhusu Dizeli na Petroli kupanda kiholela kwa zaidi
ya Tsh. 1,200 kwa lita kwa kisingizio cha kupanda bei
katika soko la dunia.

Kipindi bei ya mafuta ilipopan da kwenye soko la dunia
Serikali ilitoka hadharani kutangaza kupanda kwa bei za
bidhaa lakini leo bei ya mafuta imeshuka katika soko la
dunia kutoka Dola 112.9 hadi kufikia Dola 87.3 kwa
pipa takriban bei imeshuka kwa 22% leo ni siku ya 5
hakuna tamko kutoka serikalini kuhusu bei mpya ya
mafuta na bidhaa.

(ii) Ukosefu wa ajira, Vijana zaidi ya 800,000 sawa na 80%
ya vijana wanao ingia katika soko la ajira hukosa ajira
kila mwaka na kwamba ajira zao zimekuwa
zikihujumiwa kuhamishwa na kupewa raia wa kigeni.
Mifumo ya ajira haiko wazi na imejaa upendeleo wa kila
aina kwa misingi ya Ndugu, jamaa na mara fiki.

6

Changamoto nyingine ni pamoja na k ukosa mitaji,
mikopo yenye masharti nafuu, mikataba ya ajira,
huduma ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii , Bima, mipango
bora ya wastaafu na kukosekana kwa taasisi ya ajira
kwa vijana.

Viongozi wanapatikana kwa misingi ya upendeleo
uliopitiliza na unaweza kukuta mkoa mmoja una
Makatibu Wakuu zaidi ya 10, Mawaziri zaidi ya 5,
Mabalozi wengi huku mikoa mingine ikiwa haina hata
Katibu Mkuu wala Waziri mmoja. Mara nyingi kupata
ajira mpaka uwe na Godfather serikalini, kwa Serikali
ya aina hii Gen-Z hawawezi kuacha kuandamana kudai
haki.

(iii) Kiuchumi, wakulima kupunjwa bei ya mazao ya o kwa
maslahi binafsi ya baadhi ya Viongozi waandamizi
serikalini ikiwemo kusingizia anguko la soko la dunia,
ushuru na makato makubwa, stakabadhi ghalani, kuua
ushindani na kuwa na mnunuzi mmoja (Monopoly)
Katika msimu wa kilimo wa 2024/2025 zao la pamba
liliporomoka bei kutoka Tsh. 2,500 hadi Tsh. 1,200 na
makato makubwa ya Tsh. 300 kwa kilo.

Mazao mengine ya liyoporomoka bei ni pamoja na
choroko, dengu, mbaazi , ufuta kwa za idi ya 50% . Pia
mazao mengine kununuliwa kwa mkopo kama tumbaku
na kugeuzwa mtaji wa wafanyabi ashara bila ridhaa ya
wakulima. Kwa dhuluma hizi wakulima hawahitaji
kupewa pesa ili kuingia barabarani kudai haki yao.

7

(iv) Kuua masoko, a jira na viwanda vya ndani, baada ya
kuua mifumo ya udhibiti na kuruhusu kuingia kiholela
kwa bidhaa bandia, feki na zilizokwisha muda wa
matumizi. Pia kuruhusu kuingia mazao na bidhaa
zinazozalishwa kwa wingi nchini kama Sukari, Mafuta
ya Kupikia, Mchele, Mbolea, Mbegu, Chanjo , Dawa za
kuogesha mifugo nk. na hivyo kuua soko la ndani .
Bidhaa hizo kutoka nje ya nchi hu samehewa kodi
wakati bidhaa za ndani zinatozwa kodi kubwa na hivyo
kuua ushindani.

Hivi sasa soko la mchele nchini limeanguka kutokana na
kuingia kwa wingi mchele kutoka nje ya nchi, kashfa ya
uingizaji wa sukari kiholela ya mwaka 2024 ilipelekea
wakulima wa miwa na viwanda vya ndani vya sukari
kukosa soko na taifa kupata hasara ya zaidi Tsh. Trilioni
1.5.

Zabuni na kandarasi kupewa wageni hat a kwa kazi
ambazo wanaweza kufanya watanzania na mbaya zaidi
wazawa hawalipwi madeni ambayo yamefikia zaidi ya
Tsh. Trilioni 7 .8 hali iliyowafanya wafilisike na ajira
kupotea. Pia wazawa wamekuwa hawashirikishwi
kikamilifu katika miradi ya kimkakati inayot ekelezwa na
Serikali.

(v) Misamaha ya kodi inatolewa kwa upendeleo hasa kwa
Makampuni ya nje (Wawekezaji mahiri) huku adhabu za
ukwepaji kodi zikitolewa kwa wazawa pekee . Mfano
Makampuni makubwa ya kimataifa MNCs
yamesamehewa adhabu ya 100% kwa miamala ya

8

kukwepa kodi ya Transfer Pricing, Pia utitiri wa tozo,
ushuru, ada na kodi hutozwa kwa wazawa hali
inayopelekea kuelemewa na kufunga biashara na
kusababisha kuua ajira.

(vi) Kushamiri kwa uvuvi haramu, madawa ya kulevya,
maeneo ya wachimbaji wadogo kupewa wagen i,
utoroshaji mkubwa wa raslimali kama madini, mazao ya
uvuvi na mifugo nk.
2.3 Masuala ya Kijamii yanayojumuishwa mmomonyoko wa
maadili na kushuka kwa uzalendo, kutopatiwa ufumbuzi na
majibu stahiki ya mekuwa kero katika jamii kama vile, Rushwa,
Ubadhirifu wa mali za umma na madai ya utekaji na kupotea kwa
watu.
Rushwa na ubadhirifu wa mali za u mma, taarifa za CAG, PPRA,
FIU, PCCB, IAG zimekuwa zikiripoti upotevu mkubwa wa
matrilioni ya fedha za umma kila mwaka. Wabunge na wananchi
wamelalamikia ufisadi uliokithiri serikalini katika kipindi cha miaka
5 iliyopita bila mafanikio yoyote huku wezi wa fedha na raslimali
za umma wakir uhusiwa kula kwa urefu wa kamba, mara wezi
watajwe kwa majina waone aibu na wengine kupewa zawadi ya
teuzi katika vyombo vya maamu zi kama ubunge, uwaziri mpaka
uwaziri Mkuu badala ya kufikishwa m ahakamani. Ipo mifano
mingi:-
(a) Kuna tuhuma za wizi wa kutisha kwenye mikopo
ya Serikali ambapo kwa miaka 5 iliyopita deni la
Serikali limeongezeka kutoka Tsh Trilioni 60.9
Machi 2021 hadi Tsh. Trilioni 115.2 Februari 2026
sawa na ongezeko la Tsh. Trilioni 54.3 . Deni

9

limeongezeka kutoka ukuaji wa 7% hadi 19% hii
kasi ya onge zeko sio la kawaida (Skyrocket ting
debt).

Kwa sehemu kubwa mikopo imechukuliwa kwa siri
na nje ya bajeti, matumizi yake h ayafahamiki na
fedha nyingine zimepita kwenye akaunti za watu
binafsi badala ya mfuko mkuu wa Serikali kinyume
na Ibara ya 135 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Kifungu cha 12 cha
Sheria ya Fedha za Umma Sura ya 348 na
marekebisho yake ya mwaka 2020.

(b) Kuwepo kwa mianya na mifumo ya kodi
inayoruhusu fedha za umma kuingia kwenye
mifuko ya watu binafsi na kupoteza mapato ya
Serikali zaidi ya Tsh. Trilioni 40 kila mwaka.

(c) Tuhuma za wizi wa kutisha katika mradi wa SGR
ambapo Serikali ilikiuk a sheria ya Manunuzi na
kuongeza gharama za mradi kwa zaidi ya Tsh.
Trilioni 3.4 kwa lengo la kufuja fedha za umma
huku ujenzi wa SGR Lot 3, Lot 4, Lot 5 na Lot 6
ukiwa umetelekezwa.

(d) Tuhuma za wizi wa kutisha katika mikataba ya
kifisadi ya ujenzi wa bara bara z a lami kupitia
utaratibu wa EPC+F wa Tsh. Trilioni 3.75

(e) Tuhuma za malipo ya fidia hewa katika Mahakama
ya Kimataifa ya U suluhishi wa Migogoro ya
Uwekezaji na Biashara (ICSID) na kupoteza fedha

10

za umma zaidi ya Tsh. Trilioni 2 katika kipindi cha
miaka 5.

Kesi nyingi za mchongo za raslimali zinazidi
kufunguliwa na kuamuliwa ili kuhalalisha wizi wa
fedha za umma katika Mahakama za nje wakati
Kifungu cha 11 cha Sheria ya Natural Wealth and
Resources (Permarnent Sovereignty) Act 2017
ambayo inakataza k utumia Mahakama za nje ya
nchi (Foreign Courts) katika mashauri yote
yanayohusu raslimali za nchi. Fedha hizi zimekuwa
zikilipwa kwa siri na bila ridhaa ya wananchi
kinyume na misingi ya uwazi na uwajibikaji.

(f) Tuhuma za wizi wa kutisha katika M radi wa
Bwawa la kufua umeme ya Julius Nyerere (JNHPP-
2115) ambapo zaidi ya Tsh. Trilioni 2. 418
zimetafunwa na ubora wa mradi ni wa kutiliwa
mashaka. Gharama za mradi zimeongezeka kwa
Tsh. Bilioni 940 kutoka Tsh. Trilioni 6.5 hadi Tsh.
Trilioni 7.44 bila sababu za ms ingi, mashauri hewa
ya usuluhishi ISCID yamelipwa kiasi cha Tsh.
Bilioni 889.6, kutokutekelezwa miradi ya Kijamii
(CSR) ya Tsh. Bilioni 262 na kutokukata faini ya
ucheleweshaji wa mradi ya Tsh. Bilioni 327.

(g) Kashfa kubwa ya kuiba fedha za wastaafu katika
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF kwa
kisingizio cha kujenga uwanja wa ndege wa
Serengeti (Serengeti Airport) wenye gharama ya
Tsh. Bilioni 362.47.

11

Bodi ya PSSSF ilivunjwa baada ya kugoma
kuidhinisha fedha za ujenzi wa uwanja huo tarehe
24 Aprili 2026 na baada ya siku 20 ilipofika tarehe
14 Mei 2026 Bodi hiyo ilivunjwa lakini Mkurugenzi
Mkuu (DG) akiachwa aendelee na majukumu yake.

Ziko taarifa kuwa Bodi ya PSS SF ilibaini tathmini
ya mradi haikufanyika kikamilifu kwani mradi huo
hauwezi kurejesha fed ha kwa wakati na hivyo
kuathiri ukwasi wa mfuko kuhudumia wastaafu.
Sababu zingine ni mfuko kuwa na miradi mingi
ambayo hai fanyi vizuri na imeshindwa kurejesha
fedha za mfuko kwa wakati (Stalled and White
elephant projects).

Miradi mingi haijakamilika uk iwemo Mradi wa
kumbi za mikutano AICC Arusha wa zaidi ya Tsh.
Bilioni 350. Mfuko unadaiwa madeni makubwa ya
kodi na TRA ya takriban Tsh. Bilioni 800 hivyo kwa
namna yoyote mfuko unapaswa kuelekeza nguvu
katika kufufua na kukamilisha miradi inayoendelea
badala ya kuanzisha mradi mwingine mpya. Hata
hivyo nini lengo la kujenga uwanja wa Serengeti
wakati ujenzi wa u wanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Mwanza unasuasua na haujakamilika hadi leo
kwa zaidi ya miaka 5 sasa.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF anatuhumiwa
kuiondoa Menejimenti akiwemo Mkurugenzi wa
Uendeshaji ( DO), Meneja wa Uwekezaji (IM),

12

Meneja wa Sheria ( LM) na Mkurugenzi wa Fedha
(DF) bila idhini ya Bodi ya Wadhamini.

Wastaafu wa nchi yetu wanapitia kipindi kigumu
mara baada ya kustaafu kutokana na
kucheleweshewa mafao na makato makubwa
yasiyo na sababu za msingi ikiwemo kuanzisha
kikotoo kipya na kuwapunja wastaafu . Hii
inatokana na Serikali kushindwa kusimamia fedha
za mifuko ya hifadhi za jamii na kuruhusu wizi na
udanganyifu kutapanya fedha za wastaafu.

(h) Tuhuma ya kashfa ya uingizaji wa Sukari kiholela
ndani ya nchi ambapo nchi ilipoteza zaidi ya Tsh.
Trilioni 1.5 huku wakulima wa miwa na viwanda
vya ndani vikikosa soko.

(i) Tuhuma za wizi wa kutisha katika uagizaji na
usambazaji wa mafuta ya Dizeli na Petrol i
kutokana na kuruhusu upandishaji wa bei kiholela
na kuwaibia wananchi matrilioni ya fedha kila
mwezi.

(j) Tuhuma za wizi wa kutisha katika uagizaji kutoka
nje na usambazaji wa mbolea ya ruzuku ambapo
zaidi ya Tsh. Trilioni 1 katika kipindi cha miaka 5
zimepotea.

(k) Tuhuma za kukithiri kwa utakatishaji wa fedha
haramu hadi nchi yetu kuingia kwenye orodha ya
nchi oevu za utakatishaji wa fedha haramu
duniani, pia miamala shuku (suspicious

13

transaction) imeongezeka mara dufu kutoka Tsh.
Trilioni 122 mwaka 2022, T sh Trilioni 280 mwaka
2023 hadi kufikia Tsh. Trilioni 463 mwaka 2024
huku taarifa za miamala fiche (Hidden
Transaction) zikifichwa kwa nguvu kubwa.
Utoroshaji wa fedha nje ya nchi umeongezeka
(Illicit Financial Flows) na hakuna mtu
anayechukuliwa hatua wal a kuwajibika kwa kuwa
mtandao huo unahusisha baadhi ya Viongozi
waandamizi wa Serikali (Serious Organized Crime-
SOC).

Mnamo mwezi Februari 2026 tumeshuhudia meli
yenye shehena kubwa ya dawa za kulevya
iliyokuwa inapeperusha bendera ya Tanzania
ikikamatwa nchini El Salvado ikiwa na tani 6.6 za
dawa za kulevya aina ya Kokeini.

(l) Kashfa ya wizi wa kutisha katika Mkataba ya
Uendeshaji wa Bandari ya Dar es Saalaam ambapo
mkataba wa IGA ambao una kila aina ya
udanganyifu na harufu ya rushwa uliingiwa licha
ya k ukataliwa na watanzania walio wengi.
Mikataba 3 ya HGA‟s imeingiwa kwa siri na bila
ridhaa ya Bunge ambapo tarehe 15 Aprili 2024
Serikali ilikabidhi Uendeshaji wa Bandari katika
Gati namba 1 hadi Gati namba 7 kwa Kampuni ya
DP World ya Dubai kwa muda wa mi aka 30.
Nguvu kubwa iliyotumika ililenga kumilikisha mali

14

za umma kwa watu binafsi na kwa manufaa
binafsi.

Kampuni ya DP World licha ya kupewa kiwango
kidogo cha kuwekeza cha Tsh. Bilioni 675 tu kwa
kipindi cha miaka 5 lakini imeruhusiwa ku pata
40% ya mapato yote katika gati namba 1 hadi gati
namba 7.

Ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam ikiwemo
kupunguza siku za kutoa mzigo, kuongeza
mapato, kutia nanga meli kubwa na ndefu,
uboreshaji wa mifumo ya TEHAMA unatokana na
uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serik ali ya
awamu ya Tano kwa kushirikiana na Benki ya
Dunia kupitia Mradi wa DMGP wenye thamani ya
zaidi ya Tsh. Trilioni 1. 118 katika bandari ya Dar
es Salaam . Pia uboreshaji uliofanyika bandari ya
Tanga na siyo ujio wa DP World kama
inavyopotosha na Viongozi wa Serikali.

Aidha Serikali ya awamu ya 6 imeingia mikataba
mingi mibovu na ya siri, bila ushindani na bila
ridhaa ya Bunge ikiwemo mikataba ya raslimali 43
na ya Ubia 74 baadhi ya mikataba ni kama
ifuatavyo:- Mkataba wa TPA na Adani Group ,
Nguala Rare Earth Project, Uwanja wa Ndege wa
KIA, Ngorongoro, TFS, Vitalu vya Uwindaji,
Liganga na Mchuchuma, NHC, STAMICO, DART,

15

TANROADS (Barabara ya njia 8 ya kulipia kutoka
Kibaha hadi Chalinze), Makaa ya Mawe nk.

Serikali ya awamu ya 6 imevunja Kifungu cha 12
cha Sheria ya ulinzi wa raslimali (The Natural
Wealth and Resources Permanent Sovereignty) Act
No. 5 of 2017) Cap 449 inayotaka mikataba ya
raslimali kupelekwa Bungeni na kuridhiwa kabla ya
kuanza utekelezaji na Sheria ya TEITA inayotaka
uwazi katika micha kato ya Manun uzi katika miradi
ya raslimali. Pia kitendo hicho ni kinyume na UN
Economic Charted on Natural Wealth and
Sovereignty.
Baadhi ya Viongozi wa Umma (Political and business
elites) wamekuwa wakituhumiwa kuwa na utajiri
usioelezeka kumiliki akaun ti za fedha nyingi Ughaibuni,
kumiliki mabasi, Malori, vituo vya mafuta, mahoteli,
Maduka makubwa na S uper Market, viwanda, magorofa,
mahekalu katika maeneo mbalimbali nchini na nchi za
ughaibuni kama Dubai, South Africa, Uturuki, Ubelgiji nk.
huku wananchi wengi wakiwa kwenye lindi kubwa la umasikini.
Orodha ya watuhumiwa wa wizi, rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa
fedha na ras limali za umma ni ndefu sana lakini kwa mujibu wa
Katiba ya nchi yetu, Rais na aliyekuwa Waziri wa Fedha (Waziri
Mkuu wa sasa) ni watuhumiwa wa kwanza.
Nchi nyingine duniani ulimbikizaji wa mali za umma kwa watu
wachache binafsi hatua kali huchukuliwa dhidi yao ikiwemo
kutaifishwa mali na fedha , kufungwa gerezani na wengine

16

kunyongwa hadi kufa. Mfano wa hiv i karibuni Mahakama ya
kijeshi nchini China mnamo tarehe 7 Mei 2026 iliwahukumu
adhabu ya kifo Mawaziri wawili wa Ulinzi, Wei Fenghe na Li
Shangfu baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya kupokea
rushwa kubwa, kukiuka taratibu za manunuzi na matumizi
mabaya ya madaraka. Lakini kwa bahati mbaya hapa nchini
kwetu Viongozi wa aina hiyo hupewa kinga, heshima na
kuzawadiwa vyeo na teuzi. Wananchi wanaofanyiwa haya yote
hawawezi kuendelea kubaki kimya kwa kuhofia Mikwaju ya
mtawala.
Utekaji, kupotezwa na kuuawa ni tatizo lililoshamiri nchini mwetu,
watu wengi wamepotea na wengine kuuawa . Kwa mujibu wa
Ripoti ya Tume ya Jaji Chande, jumla ya watu waliotekwa na
kupotea ni 758 huku kati yao watu 245 waliopotea mwaka 2023
hadi 2025 hawajapatikana hadi leo. Pamoja na ukubwa wa tatizo
na wingi wa matukio hayo Serikali imekuwa haitoi taarifa
kikamilifu wala kufanya jitihada ya kudhibiti na kuwatafuta
waliopotea. Ni Wajibu wa Serikali kulinda usalama wa raia hivyo
matendo haya yanaifanya Serikali ikose sifa kikatiba.
Watu wengi wamekuwa wakikamatwa kwa kubambikiwa kesi na
baadae kuachiliwa bila maelezo, mfano watu zaidi 1,651
waliokamatwa kwenye machafuko ya tarehe 29 Oktoba 2025 kwa
makosa ya uhaini baadaye waliachiliwa huru kwa kile kilichoitwa
msamaha wa Rais jambo ambalo halipo kisheria na ni ushahidi wa
wazi kwamba walikamatwa na kushtakiwa kwa kuonewa. Jambo
hili limelalamikiwa kwa muda mrefu pamoja na mapendekezo ya
Tume ya Haki Jinai lakini limekuwa likiendelea.

17

Tunakumbuka Mzee Ali Kibao wa CHADEMA alishushwa k wenye
bus mchana kweupe Septemba 2024 na baadaye kwenda kuuawa
na mpaka leo hakuna aliyeshtakiwa kwa kifo hicho. Huku baadhi
ya wananchi na Viongozi wengine wa dini wakiamua ku kimbilia
uhamishoni nje ya nchi.
Kijana Shadrack Chaula aliyechora picha ya Ra is Samia na
baadaye kuichoma moto na watanzania kujitokeza kumlipia faini
mahakamani baadaye alitekwa na kupotea Agosti 2024 na
hajaonekana hadi leo.
Kama hiyo haitoshi, Padri Dk. Charles Kitima, Katibu Mkuu wa
Baraza la Maaskofu Katoliki ( TEC) alivamiwa na watu
wasiojulikana, alijeruhiwa vibaya na kunusurika kifo Mei 2025. Pia
tulishuhudia kundi la watu linalojiita Wakatoliki wakitangaza
kupeleka malalamiko kwa Baba Mtakatifu na kutishia kuitisha
maandamano nchi nzima kupinga Viongozi wa Kanisa jambo
ambalo lilionekana ni la kutengeneza na kuongeza uhasama lakini
baadaye tukawaona Viongozi waandamizi wa Serikali wakiwa
Vatican kwa Baba Mtakatifu Leo XIV.
Baadaye ikaelezwa na Rais hadharani Tarehe 2 Disemba 2025
alipokuwa anazungumza na aliowaita Wazee wa Dar es Salaam
kwamba Serikali yake haifurahishwi na matamko ya kila mara
yanayotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ,
ambapo matamko hayo 8 yalilaani matumizi mabaya ya raslimali
za umma (Mkataba wa Bandari), utekaji, upotezwaji na mauaji ya
raia wasio na hatia, machafuko ya Oktoba 2025 nk.
2.4 Utendaji usioridhisha wa baadhi ya watendaji na watumishi
wa umma hususan ngazi za chini (Mamlaka za Serikali za Mitaa)

18

ikiwa ni pamoja na kutosikiliza au kutatua kero za wananchi kwa
wakati na utekelezaji hafifu wa mapendekezo ya Tume
mbalimbali zinazoundwa.
(i) Kero za wananchi, wananchi kuwa na kero za muda
mrefu ambazo zimekosa ufumbuzi ikiwemo migogoro
ya ardhi kila kona ya nchi, madai ya mirathi, mahusiano
mabaya ya wananchi na wahifadhi, wananchi
kutaifishwa mifugo yao, majanga ya moto ya k ila mara,
bidhaa feki, uchafuzi wa mazingira unaopelekea kuenea
kwa magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) na
yanayoambukiza (CDs) na kusababisha taifa kuwa na
wagonjwa wengi na vifo . Ajali z a barabarani ambapo
kwa miaka 5 zaidi ya watu 7,636 wamekufa huku
majeruhi wakiwa zaidi ya watu 12,663 nk.

(ii) Mapendekezo ya Tume zinazoundwa na Rais yamekuwa
hayafanyiwi kazi, mfano Tume ya Haki Jinai, Tume ya
Maboresho ya Kodi, Tume za Ngorongoro na haya ya
Tume h ii ya Matukio ya Okt oba 29, 2025, Kikosi kazi
cha kukusanya Maoni ya wadau kuhusu uratibu Maoni
ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi, licha ya Taifa
kutumia fedha nyingi kuzihudumia tume hizo mambo
haya yanachochea hasira za wananchi.
2.5 Masuala yanayohusu uhusiano wa kima taifa katika dunia ya
leo na ijayo ambapo mataifa mengi yanatanguliza mbele maslahi
yao kama msingi wa mahusiano na kujaribu mbinu na mikakati
mbalimbali ya kujiweka katika nafasi nzuri kuendeleza maslahi
yao katika nchi nyingine, hasa zinazoendelea na zen ye raslimali
nyingi.

19

Nakubaliana na Tume kuwa mahusiano yetu na nchi nyingi
Duniani yako kwenye hatihati kutokana kushamiri kwa ukiukwaji
mkubwa wa haki za binadamu, kuminywa kwa demokrasia,
kukandamizwa Uhuru wa Maoni na Vyombo vya Habari, utawala
usiozingatia sheria na kuvunja itifaki na mikataba ya kimataifa.
Vile vile vikwazo vya uwekezaji ambapo kazi na miradi zinatolewa
kwa upendeleo na rushwa, miradi kutol ewa kwa usiri na bila
ushindani kwa baadhi ya nchi fulani, kuwekewa masharti ya ziada
yanayokinzana na Sheria za nchi. Pia mambo ya njoo kesho, njoo
kesho kutwa ambayo yanapoteza muda mwingi na kuwakatisha
tamaa na kushindwa kuwekeza nchini. Zipo ba adhi ya nchi kubwa
duniani kama Marekani zimeanza kufanya tathmini upya ya kina
ya uhusiano wake na nchi yetu.
3. UHALALI WA VITENDO VYA SERIKALI WAKATI WA
KUTULIZA GHASIA
3.1 Tume haikuchambua baadhi ya mambo muhimu ili
kujiridhisha kama nguvu iliyotumika kukabiliana na waandamanaji
ilikuwa sawa au laa!
(i) Tume ilipaswa kueleza kwa kina mazingira
yaliyopelekea Jeshi la Polisi kuua watu zaidi ya 518,
nani aliyetoa amri ya kuruhusu kuua na akina nani
walihusika na mauaji hayo, kwanini risasi nyingi
zilikuwa za kichwani, kifuani, tumboni na mgongoni.

(ii) Tume haijaonyesha uthibitisho wa Polisi kutumia
mabomu ya m achozi, maji ya washawasha, risasi za
plastiki kama njia mbadala ya kukabiliana na
waandamanaji.

20

(iii) Tume haijae leza juu ya taarifa ya kuwepo kontena l a
silaha lilil odaiwa kuingia nchini kupitia bandari ya Dar
es Salaam Agosti 2025 kipindi cha kuelekea uchag uzi
Mkuu Oktoba 29, 2025.

(iv) Tume haijaeleza juu ya madai yaliyotolewa ya kuwepo
askari kutoka nje ya nchi waliokuja kushiriki mauaji ya
raia wasio na hatia.

(v) Tume haijaeleza madai ya baadhi ya askari waliovaa
kininja na wengine kuvaa kiraia na kushirik i mauaji ya
raia wasio na hatia, wengine wakiwa kwenye magari ya
ya Polisi na ya kawaida.

(vi) Tume imeshindwa kueleza juu ya kauli ya aliyekuwa
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh George Boniface
Simbachawene aliyoitoa tarehe 8 Disemba 2025 baada
ghasia na machafuko ya uchaguzi mkuu kukemea na
kulaani kitendo cha baadhi ya askari kuvaa kininja na
kutumia nguvu kubwa kupitiliza katika udhibiti na
ukamataji wa watuhumiwa . Mwezi mmoja baadaye
Waziri Simbachawene alifuku zwa mnamo tarehe 8
Januari 2026 jambo ambalo lilipok elewa kwa hisia
tofauti na wananchi kuwa ukamataji wa kikatili una
baraka za mtawala angalia link hii

View: https://youtu.be/1l9eLTwbqGM?si=fXbYk17v0_xt6Gvw

Yaliyomkuta Waziri Simbachawene yanafan ana na
yaliyomkuta aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Prof.
Palamagamba Kabudi baada ya kukiri kuwa serikalini
kuna matatizo makubwa katika majadiliano na kuingia

21

mikataba, kuna usiri mkubwa na matokeo yake nchi
inaingia kwenye mikataba inayolinyonya ta ifa letu
yenye masharti hasi na mingine ni tegesha kwa ajili ya
kushtaki nchi kwenye Mahakama za Kimataifa za
Usuluhishi wa migogoro ya biashara na uwekezaji
(ICSID) na kuligharimu taifa letu kwa kiwango kikubwa.
Profesa Kabudi aliyasema hayo tarehe 6 Dise mba 2024
jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha
Mwanasheria Mkuu wa Serikali huku akitaka kiundwe
chombo cha kuratibu na kusimamia mikataba nchini ili
kukomesha michezo hiyo, katika hali ya kushangaza
siku 2 baadaye ilipofika tarehe 8 Disemba 2024 Profesa
Kabudi aliondolewa wizara hiyo. Angalia link

View: http://youtu.be/ZKAittcZjeQ?si=_LG3lwdD0w7qfXCl

Mfano mwingine wa hivi karibuni Bodi ya PSS SF
imevunjwa baada ya kukataa kuidhinisha fedha za
ujenzi wa uwanja wa ndege wa Serengeti mkoani Mara.

3.2 Tume imeshindwa kutoa taarifa sahihi ya watu waliopoteza
maisha katika ghasia na maandamano ya tarehe 29 Oktoba
2025.

(i) Tume imeegemea taarifa za vifo zilizotolewa na vituo
vya huduma za ya afya pekee na kuacha ma eneo
mengine muhimu ya Serikali za Mitaa na Vijiji na
wenyeviti vitongoji kwani si maiti zote zilipelekwa
hospitali ikizingatiwa kuwa kulikuwa na katazo la
kutotoka nje.

22

Tume imeshindwa ku toa idadi halisi ya vifo kwani
madai ya kuwa watu wal iouawa wanaweza kuwa
zaidi ya 518 ni sawa na kukubaliana na takwimu za
watu wengine wanaosema kuwa watu waliouawa ni
zaidi ya 10,000 katika mikoa na wilaya zilizokumbwa
na machafuko.

(ii) Mchanganuo wa Tume katika ripoti yake ya idadi ya
watu waliofariki kati ka Mkoa wa Dar es Salaam
(182), Mkoa wa Mbeya (80), Mkoa wa Mwanza (90)
na Mkoa wa Arusha (53) , mchanganuo huo unaleta
jumla ya watu 405 badala ya 518 hii ni tofauti ya
marehemu 113. Makosa haya ya kitakwimu yanaleta
mashaka kuwa takwimu hizo ni za kupika na
zimechakachuliwa.

(iii) Pia Tume bila aibu imeficha idadi ya vifo katika Mikoa
ya Shinyanga (Kahama), Geita (Geita na Katoro),
Songwe (Momba &Tunduma), Mara (Bunda, Tarime)
na Iringa ambapo taarifa zilizopo watu wengi
waliuawa katika maeneo hayo.

3.3 Tume imeshindwa kuthibitisha madai ya mali iliyoharibiwa ya
thamani ya Tsh. Bilioni 125 yakiwemo majengo ya CCM na
Mahakama.

(i) Tume imeshindwa kuueleza umma chombo kilichofanya
ukadiriaji na utha minishaji wa mali zilizoharibiwa na
kufikia hasara ya Tsh. Bi lioni 125, hivyo madai haya
hayana uthibitisho na pengine yamelenga kufuja fedha
za umma kwa kisingizio cha fidia.

23

(ii) Tume imeweza kupata gharama za mali zilizoharibiwa
lakini imeshindwa kukokotoa gharama za kifuta
machozi za marehemu zaidi ya 518 na fidia, gharama
za matibabu na vifaa saidizi kwa wananchi waliopata
ulemavu wa kudumu zaidi ya 2,390.

(iii) Tume kwa siku zaidi ya 153 imeshindwa kukotoa
madhara na hasara walizopata wananchi na taifa kwa
ujumla kutokana na kuzimwa kwa Mtandao wa Intaneti
na kuzuiwa watu kutoka ndani (Curfew na Lockdown)
ambapo shughuli za kijamii na kiuchumi zilisimama kwa
siku 6 mfululizo. Je zuio hilo lilikuwa na uhalali wa
kisheria?

Kwa tathmini niliyofanya nchi ilipoteza zaidi ya Tsh.
Trilioni 5 ambapo Tsh. Trilioni 1 ni kodi ya Se rikali na
Tsh. Trilioni 4 ni mapato ya wananchi kutokana na
shughuli zao za kiuchumi za kila siku kama biashara,
mawasiliano, Benki, mikataba, uwekezaji nk.

Aidha madhara mengine ni pamoja na wananchi wengi
walikosa huduma za afya na wengine kupoteza maisha
kwa kukosa matibabu . Pia huduma za elimu, maji,
chakula na huduma zingine muhimu ziliathiriwa na
kuleta adha kubwa kwa wananchi.
3.4 Tume kushindwa kuthibitisha kauli za Viongozi (Rais na Waziri
Mkuu) ambapo kwa nyakati tofauti walieleza umma kuwa w atu
walioshiriki maandamano hayo walitoka nje ya nchi, na wengi
walifuata mkumbo, walipewa fedha kwanza ili waandamane na
walifadhiliwa na taasisi za Nje na Ndani . Waziri Mkuu alidai kuwa

24

kuna mtu mmoja alipewa Tsh. Bilioni 5 ili azigawe kwa
waandamanaji na akapiga marufuku kutaja idadi ya marehemu
kwa kuwa kufanya hivyo ni sawa na kushangilia vifo.
(i) Tume imeshindwa kuthibitisha kama waandanamaji
waliotoka nje ya nchi , walitoka nchi gani na namna
walivyoingia nchini?

(ii) Tume imeshindwa kuweka wazi kuhusu na ni
aliyefadhili Tsh. Bilioni 5 na nani aliyezipokea, na
ziligawiwa kwa utaratibu gani kwa waandamanaji.

(iii) Tume imetoa taarifa ya idadi ya waliouawa na
kujeruhiwa kinyume na agizo la Waziri Mkuu
lililozuia.

(iv) Tume imeorodhesha vyanzo vikuu vya maandamano
na kupingana na Kauli ya Rais kuwa waandamanaji
hawakuwa na ajenda mahsusi bali walilipwa na
walifuata mkumbo.
Kushindwa kwa Tume ya Jaji Chande kuthibitisha ukweli wa kauli
hizo au kubaini kinyume chake inaleta utata mkubwa kwa
Viongozi hao kwenye jamii.

4. VITENDO VYA SERIKALI BAADA YA MATUKIO YA MAUAJI YA
OKTOBA 2025

4.1 Vitendo vya Serikali baada ya matukio ya mauaji ya Oktoba
2025 vinadhihirisha wazi kuwa Serikali ina mgongano mkubwa wa
maslahi kama ifuatavyo:-
(i) Serikali kuacha kutenga muda wa kuomboleza w ala
kupeperusha bendera nusu ml ingoti katika kipindi cha

25

maombolezo kinyume na utaratibu wa siku zote nchi
inapopata majanga ya kupoteza maisha ya watu wengi.

(ii) Madai ya baadhi ya majeruhi kuzuiwa kupewa huduma
za matibabu na wengine kupelekwa mochwari wak iwa
hai kwa amri ya polisi.

(iii) Madai ya Ndugu wa marehemu ku nyimwa miili na hata
walioruhusiwa kuchukua miili waliandikiwa kwenye
vyeti vya kifo sababu nyingine na sio kuuawa kwa
risasi.

(iv) Maeneo mengi yaliyokuwa makazi ya ombaomba na
watu wenye matatizo ya akili hawapo huenda nao
waliuawa wakati wa machafuko.

(v) Serikali kushindwa kufanyia kazi taarifa za kiusalama
kutoka TCRA za terehe 17 -26 Oktoba 2025 kuwa
kulikuwa na mijadala katika moja ya mitandao ya
Kijamii kuhusu namna watakavyotekeleza ghasia siku
ya uchaguzi na kwamba kuna makundi yamejipanga
kuharibu uchaguzi na yalikuwa yakiendesha mafunzo
kwa vijana. Baadaye Tume ilibaini kuwepo nyumba
waliyokuwa wakifanya mafunzo ambayo ilikuwa mita 10
kutoka kituo cha Polisi.

(vi) Tume imeshindwa kuchunguza sababu za kukamatwa
na kushtakiwa kwa makosa ya uhaini, ugaidi na
ujambazi kwa vijana 1,651 na baadae kuachiliwa huru
kwa kile kilichoitwa msamaha wa Rais.

26

4.2 Tume kushindwa kuchunguza matukio ya watu kutekwa,
kupotea na kuuawa:
(i) Tume imepokea taarifa za Polisi pekee badala ya
kuwahoji pia inaodai waliotekwa na baadaye
wakapatikana watu 513. Pia Tume haijaeleza hatma ya
watu 245 waliopotea ambao hawajapatikana hadi leo.

(ii) Tume imeamini taarifa ilizopewa na Polisi kuwa watu
wengi wamepotea kwa sababu za mapenzi, ushirikana,
madeni, kukwepa mkono sheria, huku ikijua wazi kuwa
wapo wanasiasa wengi waliotekwa,kupotezwa kutokana
na kuwa wakosoaji wakubwa wa Serikali , mfano Balozi
Humphrey Polepole, Mchungaji Dk t. Godfrey Malisa,
Mdude Nyagali, Deus Soka.

Baadhi yao kukimbilia uhamishoni kutokana na vitisho
ili kunusuru maisha wakiweno Rose Mayemba, Sativa,
Twaha Mwaipaya , Hilda Newton , Mchungaji Mbarikiwa
Mwakipesile, Pastor Dickson Kabigumila na wengine
wengi. Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Agosti
2024 ilitoa orodha ya watu 83 waliotekwa na ku potea
kutokana na misimamo yao ya kisiasa.

(iii) Tume imeshindwa kuhoji sababu za Polisi kushindwa
kutangaza na kuchukua hatua dhidi ya watu au kikosi
cha watu kinachohusika na utekaji, kupoteza na kuua
raia wasio na hatia lakini badala yake imepokea simulizi
kutoka Polisi y a idadi ya watu 758 waliote kwa na
kupotea.

27

4.3 Tume kushindwa kutangaza gharama ilizotumia kufanya
uchunguzi na Uhalali wa kuongezewa mu da kutoka siku 90 hadi
siku 153, hii ikiwa ni ziada ya siku 63 saw a na ongezeko la muda
la 70%.
(i) Gharama zilizotumiwa na Tume hazikutangazwa
hadharani kinyume na misingi ya utawala bora ya uwazi
na uwajibikaji inavyotaka. Eneo hili lisipotazamwa kwa
umakini linaweza kutumika kama uchochoro wa kufuja
fedha na mali za umma.

(ii) Ongezeko la muda la ziku za ziada 63 z a Tume
kukamilisha kazi yake ni nyingi na Tume imeshindwa
kuthibitisha Uhalali wa ongezeko hilo. Aidha Tangazo la
Gazeti la Serikali (GN) la ongezeko la muda lilitolewa
mwishoni na nje ya muda uliopa swa kuwasilisha ripoti
ya Tume.

Tume ilipaswa kukamilisha kazi na kuwasilisha r ipoti
tarehe 20 Februari 2026 lakini GN ya ongezeko la muda
ilitolewa siku hiyo hiyo iliyotakiwa kuwasilisha ripoti .
Tume iliongezewa muda hadi tarehe 3 Aprili 2026 lakini
GN ya kuongeza muda ilitolewa tarehe 4 Aprili 2026 nje
ya muda wa kuwasilisha ripoti. Suala la kuongezewa
muda haliwezi kufanywa kwa dharura ilipaswa walau
siku 7 kabla ya siku ya kuwasilisha ripoti hivyo
nyongeza ya muda wa siku 63 iliyoongezewa Tume
haikuwa na sababu za msingi.

(iii) Ongezeko la muda lilitangazwa na Mwenyekiti wa Tume
kupitia Press Release na GN badala ya Mamlaka ya

28

uteuzi hivyo kuleta mkanganyiko mkubwa kuhusu
uhalali wa nyongeza ya muda wa kukamilisha kazi ya
Tume.
Kutokana na mkanganyiko huo ni dhahiri kuw a Uhalali wa
ongezeko la muda umeshindwa kuthibitika na pengine u lilenga
kuwazubaisha wananchi na kuchakachua ripoti ili kuuficha ukweli
na kufuja fedha za Umma.
4.4 Kupendekeza kuanzisha Tume nyingine ya jinai kuchunguza
kwa kina na kubaini waliohusika k atika matukio hayo ya mauaji
ya Oktoba 29, 2025.
(i) Haitokei kuunda tume mbili kwa madhila
yanayotokana na tukio moja au mnyororo wa
matukio ambayo chimbuko lake ni moja tena chini ya
mamlaka hiyo hiyo. Aidha jukumu kuu la Tume
lilikuwa kubaini ukweli (Fact Findings) kuhusu
matukio ya ghasia za wakati na baada ya uchaguzi
Mkuu Oktoba 2025 na kwamba Tume iliundwa
ikapewa Sekretarieti i takayoweza kufikia malengo
hayo.

(ii) Pendekezo la kuunda tume n yingine chini ya
Mamlaka hiyo hiyo ya Rais ni kuwapotezea muda
wananchi, kufuja fedha za umma na ni ujanja wa
kukwepa mchakato wa Mahakam a ya Kimataifa ya
Uhalifu (ICC) na mamlaka zingine za kimataifa.

29

4.5 Kuzuia Ripoti ya Tume ku pelekwa kwa wananchi na kudai ni
mali ya Rais na isidaiwe na mtu yoyote.
(i) Awali wakati Mtawala anaunda Tume aliwaomba
watanzania kuwa na subira wakati Tume
inakamilisha kazi yake ili kulitoa Taifa hapa lilipo,
baada ya ripoti kuwasilishwa nini kilibadilika hadi
kuficha ripoti.

(ii) Kusoma muhtasari na kuzuia ripoti ya Tume
kutodaiwa na mtu yoyote wala kwenda kwa Umma ni
ishara kuwa maudhui yaliyowasilishwa kupitia
muhtasari huenda yanakinzana na ripoti yenyewe na
kwamba kuna mambo mengi yasiyo ya kawaida
yanafichwa.

(iii) Ripoti ya Rais sio ya Siri hivyo kitendo cha Rais
kukataa isiende kwenye Umma ni mwendelezo wa
kuuficha ukweli ulioanishwa kwenye ripoti hiyo na
kuthibitisha kwa uwazi mgongano mkubwa wa
maslahi (Conflict of Interest)

(iv) Pia kuna mgongano wa ndani (Contradictions)
ambapo Tume inaahidi wadau kusoma mapendekezo
na Maoni ndani ya Ripoti k amili nanukuu “Nimetaja
baadhi tu ya mapendekezo yaliyomo kwenye
Ripoti, bila shaka wadau mbalimbali watapata
fursa ya kuyasoma kwa kina ndani ya Ripoti”
Mwisho wa kunukuu (Uk.58 wa Hotuba ya
Mwenyekiti wa Tume) lakini Rais baada ya kupokea

30

ripoti hiyo ali sema ni Ripoti yake na haipaswi
kudaiwa na yeyote.

Jambo la kushangaza zaidi Tu me ya Jaji Chande
ilipopata fursa ya kutoa Ufafanuzi kwa waandishi wa
habari Tarehe 28 Aprili 2026, Dar es Salaam
kuhusiana na Ripoti yao waliyokabidhi kwa Rais
walisema“ripoti isingeweza kuwekwa hadharani
kwa kuwa inajumuisha taarifa za siri” Kauli hii
ni kinyume na tamko lao la kwanza siku wanakabidhi
ripoti. Huu ni ushahidi wa wazi kuwa Tume hii
haikuwa na msimamo kwenye jambo lolote na
ilitegemea uelekeo wa mtawala pekee.

Kitendo cha kutoa ufafanuzi kwa umma hakikuwa na
mantiki yoyote kwa kuwa Rais alishasema Ripoti hiyo
ni yake na kwamba hata tume yenyewe ilikuwa
imeshatamatika kisheria mnamo tarehe 23 Aprili
2026 baada ya kukabidhi Ripoti kwa Rais.

(v) Rais anadai kuwa rip oti ni mali yake binafsi na kama
ni mali yake binafsi kwanini ametumia m ali na fedha
za umma kuhudumia tume hiyo kwa siku 153.

Marais waliotangulia tangu enzi ya Mwalimu Julius
Nyerere ripoti zilitolewa na hata pale zilipowasilishwa
kwa muhtasari taarifa zote muhimu ziliwekwa wazi ili
umma uujue ukweli mfano Tume ya Jaji Kipenka
(Mauaji ya Wafanyabiashara wa Madini Mahenge) ,
Tume ya Jaji Warioba (Katiba Mpya), Tume ya
Profesa Mruma (Makinikia) nk ambapo wahusika

31

walitajwa kwa majina na vyeo vyao na kuchukuliwa
hatua za kiutawala na wengine kuburuzwa
Mahakamani na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa.
(vi) Tume imepata hofu na kuogopa ku ishutumu Serikali
(Inferiority Complex) kutokana na uhusika wake
katika machafuko ya Oktoba 29, 2025. Tume
imeshindwa kutafiti na k ufanya uchunguzi wa
mambo muhimu, imekuwa na kigugumizi kueleza
ukweli lakini pia imekiuka kwa makusudi Sheria na
Kanuni za kufanya uchunguzi na utafiti na kubakiza
simulizi.

(vii) Serikali kutoa taarifa kwa umma ni jambo la lazima
na siyo hiari, Raia wa Tanza nia wanayo haki ya
kupewa taarifa wakati wote kuhus u matukio
mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu
kwa maisha na shughuli za wananchi na pia juu ya
masuala muhimu kwa jamii na kudai uwazi na
uwajibikaji. Hii pia ni kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Kifungu cha 4 cha Sheria ya upatikanaji wa taarifa
kwa umma (Access to Information Act).

5. UHALALI WA MAANDAMANO YA OKTOBA 2025
Tume katika hitimisho lake kuhusu uhalali wa maandamano ya
Oktoba 2025 ilidai kuw a hayakuwa maandamano ya amani bali
yalikuwa ni matukio ya ghasia zilizoambatana na matukio ya
uvunjifu wa amani, Tume ilibainisha kwamba waandamanaji
walikuwa nje ya kinga iliyowekwa kitaifa na kimataifa na hivyo
uvunjifu huo ulisababisha S erikali kutumi a nguvu kubwa
32

kukabiliana na waandamanaji hao. Hitimisho hilo la Tume
halitendi haki kwa waandamanaji kwa uchambuzi ufuatao:-
(I) Madai ya kuwa Waandamanaji hawakutoa
taarifa polisi
Ukweli ni kwamba k abla ya siku ya uchaguzi, vuguvugu la
maandamano lilienea kila kona ya nchi ambapo Rais, Waziri wa
Mambo ya ndani na Jeshi la Polisi walionya na ku piga marufuku
maandamano kuelekea siku ya uchaguzi mkuu badala ya kujipa
muda wa kusikiliza madai ya wananchi. Wahusika hao mara kwa
mara walitoa vitisho na hivyo isingekuwa rahisi kupelekewa notisi.
Imani ya wananchi kwa Jeshi la Polisi imepungua kutokana na
jeshi hilo kushindwa kudhibiti matukio ya uhalifu kama utekaji,
upotezwaji na mauaji yanayofanyika kila kona ya nchi na hivyo
wasingeona kama ni chombo halali cha kukimbilia.
(II) Madai ya kwamba eti Waandamanaji walizuia
haki ya mpiga kura
Kwa kifupi hapakuwa na uchaguzi Oktoba 29, 2025 bali kulikuwa
na mapinduzi ya Kiraia (Civil ian coup) kujiweka kwenye uongozi
kwa njia ya udanganyifu na mtutu wa bunduki badala ya
kuchaguliwa na wananchi, kujiweka madarakani kwa udikteta
badala ya njia ya kidemokrasia na hi vyo Rais, Wabunge na
Madiwani wame patikana kwa njia zisizo halali, kinyume cha
Sheria na Katiba ya Nchi. Hivyo maandamano yalilenga kudhibiti
uharamia huo uliolenga kupoka haki ya raia kuchagua v iongozi
wanaowataka.
Uchaguzi wa mwaka 2025 hata w aangalizi wa Jumuiya za SADC,
AU waliukataa kwamba haukuwa huru, haki wala wa kuaminika

33

na kwamba ulikuwa na dosari nyingi kiasi cha kut okukidhi
viwango vya demokrasia na hata baadhi ya Jumuiya za Kimataifa
zimetaka uchaguzi urudiwe kwa kuwa uchaguzi uliofanyika
haukuwa huru, haki wala wa kuaminika. Baadhi ya changamoto ni
kama ifuatavyo:-
Upande wa CCM.
(a) Uteuzi wa mgombea wa urais wa CCM, Ndg. Samia Suluhu
Hassan ulip ingwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na
mwanachama mwenzake wa CCM kutoka Kwimba, Mwanza,
Ndugu Devidlevi Nestory Nkindikwa. Pia mwanachama mwingine
wa CCM wa Moshi, Kilimanjaro Mchungaji Dk t. God frey Malisa
alipinga uteuzi huo Mahakama Kuu ya Tanzania kwa madai kuwa
mgombea huyo hakuwa amechukua fomu, Mkutano uliompitisha
haukuwa na ajenda ya uchaguzi, hakujaza fomu, jina lake
halikupita kwenye vikao vya mchujo huku mgombea huyo
akiendesha yeye mwenyewe vikao vya uteuzi wake jambo ambalo
ni kinyume na Kanu ni na Katiba za CCM na Sheria ya Vyama vya
Siasa kifungu cha 4 (5) (b), 6 A (2) Sura ya 258 RE 2019.
(b) Tarehe 26 Agosti 2025, Msajili wa Vyama vya Siasa alitoa
uamuzi wa malalamiko ya Ndugu Nkindikwa kwamba hawezi
kushughulikia malalamiko hayo kwa kuwa suala la uteuzi wa
mgombea wa CCM liko Mahakama Kuu jambo ambalo lilik uwa ni
la uongo kwani Mahakama K uu ilikuwa im eshaifuta kesi hiyo
tangu tarehe 22 Agosti 2025. Uamuzi wa Msajili ulilenga kumlinda
mgombea wa CCM asienguliwe kugombea na Tume ya Uchaguzi.
(c) Mchungaji Dkt. Malisa baada ya kesi yake ya kupinga uteuzi
wa Samia kutupwa na Mahakama Kuu alikata rufaa Maha kama ya

34

Rufaa Tanzania Oktoba 6, 2025 ambapo kesi yake ili pakiwa hadi
uchaguzi kupita na bado mpaka leo haijasikilizwa na kibaya zaidi
alitekwa na watu wasiojulikana na baadaye kufunguliwa kesi ya
Uhaini Januari 2026 na kusota gerezani hadi tarehe 19 Mei 2026
alipoachiwa huru na kufutiwa mashtaka.
(d) Balozi Polepole ambaye naye alipinga mchakato wa
kumpitisha mgombea wa CCM kwa kueleza kuw a kikao hicho
hakikuwa na ajenda ya uchaguzi na kusisitiza kuwa „Samia Must
Go‟ ambapo muda mfupi baada ya kauli hizo alitekwa na watu
wasiojulikana na hadi sasa ni miezi zaidi ya 8 hajulikani alipo.
Pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa
Kawe, Askofu Josephat Gwajima alipoibua hoja ya watu kutekwa
na kupotezwa na kudai uwajibikaji, vikao vya uchujaji majina
ngazi zote vilielekezwa kutopendekeza majina ya watu ain a ya
Gwajima (Magwajimanization) na baadae aka poteza nafasi ya
kugombea huku Kanisa lake la Ufufuo na Uzima lenye matawi
zaidi 2000 kote nchini likafungiwa na kuwazuia waumini kuabudu
kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Pia idadi kubwa ya Madiwani na W abunge wa Chama cha
Mapinduzi waliokuwa wakidai uwazi na uwajibikaji wa Serika li
walikatwa majina katika hatua za awali ili wasipate fursa ya
kugombea na kuchaguliwa na wananchi jambo hili lilileta
manung‟uiko makubwa kwa wanachama wa CCM na wananchi
nchi nzima.
Upande wa ACT Wazalendo
(i) Baada ya mimi Luhaga Joelson Mpina kuchaguliw a
kihalali na Mkutano Mkuu wa Chama cha ACT

35

Wazalendo kupeperusha bendera kwa nafasi ya Rais
Nilizuiwa kurejesha fomu wala kufika ofisi za INEC
Agosti 27, 2025 kwa madai kuwa Msajili wa Vyama vya
siasa amefuta uteuzi wangu, hii ni mara ya kwanza
katika his toria ya nchi yetu, Mgombea wa nafasi ya
Urais aliyezunguka nchi nzima kutafuta wadhamini, kula
kiapo Mahakama Kuu na kulipia Tsh. Milioni 1 ya fomu
kuzuiliwa kurejesha fomu na bila hata kupewa nafasi ya
kusikilizwa jambo ambalo lilikuwa kinyume cha Sheria
ya uchaguzi na Katiba ya Nchi.

(ii) Hata pale Mahakama Kuu iliponipa ushindi na kuamua
nirejeshe fomu na uteuzi uendelee bado Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Ndg. Hamza Said Johari aliniwekea
pingamizi akirejea maamuzi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa, pamoja na kutoa utetezi kuwa kwamba uamuzi
wa Msajili wa Vyama vya Siasa nimeupinga Mahakama
Kuu kwa shauri Na. 23438 ya mwaka 2025 chini
Mheshimiwa Jaji Wilbert Chuma hivyo maamuzi hayo
hayawezi kutumika tena kwenye pingamizi hadi hapo
Mahakama itakapoamua vinginevyo. Pamoja na utetezi
huo wa kisheria na kikatiba bado INEC ilikubaliana na
pingamizi la AG na kuniondoa kwenye orodha ya
wagombea.

(iii) Hata baada ya kufungua shauri lingine Mahakama Kuu
na baadaye Mahakama ya Rufaa tarehe 22 Oktoba
2025 kwa shauri Na. 2122 la mwaka 2025 shauri hilo
halikusikilizwa hadi uchaguzi kufanyika na mpaka leo
licha ya kufanyika Kikao cha kiutawala kilihusisha pande

36

mbili za waleta rufaa (Mimi na Chama cha ACT
Wazalendo) na Wajibu rufaa (Hamza Said Johari (AG)
na Dkt Ally Possi (SG) n a Wakili wa Serikali Mark
Mulwambo chini ya Uenyekiti wa Jaji Mkuu wa
Tanzania, Mheshimiwa George Masaju. Isingetarajiwa
kwa nchi inayofuata misingi ya Sheria na demokrasia
kuendelea na uchaguzi huku mmoja wa mgombea ana
kesi Mahakamani ya kupinga kuenguliwa kwake.

Kushindwa kuamuliwa kwa kesi hiyo kulipelekea Chama
cha ACT Wazalendo kukosa Mgombea Urais na Makamu
wa Rais Bi Fatma Abdulhabib Ferej , Hata hivyo
nichukue fursa hii kuwapongeza sana Mawakili
waliosimamia kesi zangu za uchaguzi katika hatua zo te
Wakili Msomi Omar Said Shaaban (Mwanasheria Mkuu
wa Chama), Wakili Msomi John Seka, Wakili Msomi
Edson Kilatu na Wakili Msomi Jasper Sabuni na kwamba
mapambano bado yanaendelea.

(iv) Vyombo vya Serikali vya INEC, RPP na AG vinatumika
kama silaha ya kuwaeng ua wagombea wa upinzani ili
kuua ushindani na kuwafanya wagombea wa CCM wa
nafasi ya Rais, Ubunge na Udiwani kupita bila
kupingwa.

Mfano Kesi ya Mwana CCM, Nkindikwa kwa Msajili wa
Vyama vya Siasa alijibiwa kuwa Msajili hatashughulikia
suala ambalo liko Mahakamani na anabanwa na Ibara
ya 107A (1 ) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania lakini upande wangu nilienguliwa na INEC
licha ya kueleza kuwa pingamizi l a Mwanasheria Mkuu

37

wa Serikali limepingwa Mahakamani. Hii ni double
standard na upendeleo uliopitiliza.
(v) Chama cha ACT Wazalendo kunyimwa nafasi ya Viti
Maalum katika nafasi za ubunge na udiwani licha ya
kupata 6.677% ya kura zote za wabunge ambapo
ilistahili kupata viti zaidi ya 6 vya ubunge huku chama
cha Chauma kikipewa viti 2 kinyume na Ibara ya 78 (1)
ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Upande wa CHADEMA
(i) Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA alikamatwa na
kufunguliwa kesi ya uhai ni Aprili 2025 na chama chake
kilifungiwa kufanya shughuli za kisiasa kwa kupitia
Msajili wa Vyama vya Sias a, Jaji Mstaafu Fransis
Mutungi na baadaye Mahakama Kuu hivyo chama hicho
kilizuiwa kufanya shughuli za kisiasa kwa mwaka mzima
na kimekuja kufunguliwa tena Aprili 2026 baada ya
uchaguzi kumalizika.

Nakumbuka siku nilipokwenda Mahakamani
kuhudhuria kesi yake alifurahi sana huku
akisema Mpina kaza, kaza kabisa be strong,
nami nilimwambia najua uko jela kwa tuhuma za
uongo lakini yana mwisho haya.

(ii) Uamuzi wa zuio la kukifungia chama cha CHADEMA
uliotolewa chini ya Jaji Hamidu Mwanga umekuja
kufutwa na Maha kama ya Rufaa Aprili 16, 2026 huu ni
ushahidi wa wazi kuwa chama hicho kilionewa ili

38

kisishiriki katika kinyang‟anyiro cha uchaguzi mkuu wa
2025.

(iii) Pia viongozi wengi wa CHADEMA walikamatwa kwa
kusingiziwa makosa mbalimbali na wengine kulazimika
kukimbilia nje ya nchi.
Mazingira ya Uchaguzi
Zilijitokeza dosari nyingi katika zoezi la uandikishaji wapiga kura,
kupiga kura, kuhesabu kura na kutangaza matokeo na hata
Uhalali wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Tume ya uchaguzi iliteuliwa na Rais ambapo ameteua wajumbe
bila ushindani na kwa upendeleo wa hali ya juu kwa misingi ya
Ndugu, jamaa na marafiki kama ifuatavyo: - Jaji Jacobs
Mwambegele (Mwenyekiti), Jaji Mbarouk Salim Mbarouk
(Makamu), Wajumbe wengine ni Jaji Asina A. Omari, Balozi
Omary Ramadhani Mapur i, Dkt. Zakia Mohamed Aboubakar,
Magdalena Kamugisha, na Ramadhani Kailima (Katibu na
Mkurugenzi wa Uchaguzi).
Tume hii iliteuliwa mwaka 2023 wakati huo ikiitwa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) na hivyo muda wake kisheria ulitamatishwa
mara baada ya Sheria na jina la Tume kubadilishwa mwaka 2024
na kuwa Tume Huru ya Uchaguzi (IN EC) waliruhusiwa kusimamia
uchaguzi wakiwa hawana sifa kisheria na kinyume na Kifungu cha
5 (1) (2) (a) na (b) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi ya Mwaka 2024 ambayo inata ka wajumbe wa Tume
Huru ya Uchaguzi wapatikane kwa njia ya ushindani kwa kuomba
nafasi hizo na kufanyiwa usaili.

39

Hivyo uchaguzi wa mwaka 2025 ulisimamiwa na Tume batili
ambayo haina mamlaka kisheria ni sawa na kusema uchaguzi huo
ulisimamiwa na genge la m tu binafsi. Dosari zingine ni kama
ifuatavyo:-
(i) Mawakala wengi wa ACT Wazalendo walizuiwa kuingia
katika vituo vya kupigia kura na hivyo kushindwa
kushiriki zoezi la upigaji kura, kuhesabu, majumuisho
ya kura na kutangaza matokeo.

(ii) Baadhi ya masanduku ya k ura yaliondoka na magari ya
polisi na kwenda kusikojulikana , baadhi ya wasimamizi
wa uchaguzi walionekana wakitiki karatasi za kupigia
kura na baadhi ya vituo walionekana watu
wakitumbukiza lundo la karatasi za kura za Rais,
Wabunge na Madiwani.

(iii) Mawakala wengi hawakupewa fomu za majumuisho ya
kura wala kusaini, wagombea na mawakala wengi wa
ACT Wazalendo walikamatwa na kufunguliwa kesi za
ugaidi, uhaini na ujambazi wakati zoezi la kupiga kura
likiendelea. Wengine walipigwa hadi kuuawa mfano
mgombea udiwan i Kata ya Sirari, Tarime Mkoa Mara
Dafroza K. Jacob.

(iv) Baadhi ya mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma,
Arusha, Mbeya, Ruvuma, Iringa, Songwe, Geita,
Shinyanga na Mara jumla ya mikoa 11 na wilaya 21
kuliibuka machafuko makubwa ambapo baadhi ya vituo
na ma boksi ya kura yalichomwa moto, vurugu za
maandamano na watu kuuawa lakini INEC iliwatangaza

40

wagombea wa CCM kwamba wameshinda kwa zaidi ya
95% maeneo hayo.
(v) Licha ya vituo vingi vya kura kuonyesha mwitikio
mdogo wa wapiga kura kuwa kati ya 10% -23% lakini
INEC ilitangaza mwitikio wa wapiga kura wa 87% na
mgombea wa urais wa CCM kutangazwa mshindi
97.6%. Kwa maoni yangu , m atokeo haya ni ya
kughushi na hayana uhalisia.

(vi) Upande wa Zanzibar hali ilikuwa vilevile ya uingizaji wa
karatasi za kura kwenye masanduku , karatasi za kura
za kuzagaa mitaani, mawakala kutolewa vituoni na
baadhi ya wagombea kuwekwa kuzuizini na kupigwa na
kuumizwa vibaya na huku vyombo vya dola vikitoa
vitisho vingi, kura hazikuhesa biwa wala kufanyiwa
majumuisho. Hata kura za Rais wa Zanzib ar
hazikuhesabiwa wala kufanyiwa majumuisho ambapo
hadi leo Mgombea wa Urais wa ACT Wazalendo, Ndg.
Othman Masoud Othman hajapewa hati rasmi ya
matokeo baada ya kunyang‟anywa ushindi.

(vii) Licha ya takwa la kisheria la kuitaka INEC kutangaza
kwenye Gazeti la Serikali ndani ya siku 7 baada ya
kutangaza matokeo leo ni zaidi ya miezi 7 imeshindwa
kutangaza matokeo hayo.

(viii) Pia Jumuiya na Taasisi za Kimataifa wakiwemo
waangalizi wa SADC, AU (AUEMO), Bunge la Ulaya
(EU), Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Haki za
Binadamu (UNCHR), walitoa taarifa zao kupinga

41

matokeo ya uchaguzi huo kwa kuwa unakinzana na
Kanuni za uchaguzi wa kidemokrasia, huru, haki na wa
kuaminika lakini pia ukiukwaji mkubwa wa haki za
binadamu na kutaka uchunguzi huru ufanyike.
Tume Huru ya Uchagu zi kwa sehemu kubwa ndiy o lilipiga kura
badala ya wananchi na kutangaza matokeo feki, h ivyo
kuandamana kwa wananchi walikuwa na sababu za msingi kwa
kuwa huo haukuwa uchaguzi bali genge lililoamua kupindua
mchakato wa kidemokrasia wa wananchi na kujiweka madarakani
kwa nguvu (kidikteta).
(III) Madai ya kwamba Waandamanaji walikuwa na
silaha (Bunduki)

(a) Tume i meibua tuhuma za kiujumla kwani siyo kweli
kwamba waandamanaji wote walikuwa na silaha, pia
imeshindwa kuweka ushahidi wa kuaminika . Mfano
waandamanaji walik uwa na bunduki ngapi na za aina
gani? Na je bunduki hizo zinamilikiwa kihalali au laa, na je
walikamatwa waandamanaji wangapi wenye bunduki?
Badala yake Tume imepiga simulizi tu. Hii sio sawa na ni
dhihaka kubwa kwa taifa na kutowatendea haki
marehemu kwa kuwa hawana uwezo wa kujitetea.

(b) Tume inaeleza kuwa walioshiriki maandamano ni
wananchi wa kawaida na wengi wafuat a mkumbo sasa
kama ndivyo hivyo, wananchi hao walipata wa pi silaha za
bunduki hadi kutishia usalama wa nchi?

(c) Watu wote waliokamatwa kwenye vuguvugu la
maandamano na kufikishwa Mahakamani kwa makosa ya

42

uhaini walisamehewa na haikuripotiwa kama baadhi yao
walikutwa na silaha aina ya bunduki.
(IV) Madai ya kwamba Maandamano yalihatarisha
usalama wa Taifa
Kwa kuwa Tume imeshindwa kuthibitisha kama w aandamanaji
walitumia silaha za moto na kuhatarisha usalama wa nchi ni
dhahiri kuwa kilichoonekana kwa jamii ndio ukweli wenyewe
kuwa waandamanaji hawakuwa na silaha (Unarmed protestors)
na wengi wao waliuawa wakiwa wanakimbia kujisalimisha
majumbani na wengine walikuwa barabarani, maeneo ya kahawa,
kwenye vibanda vya kuangalia Mpira, vi simani wakichota maji,
madukani na sehemu zao za biashara (Picha na Video Clips zote
zinaonyesha waandamanaji hawakuwa na bunduki). Hakuna
picha wala video inayoonesha kuwe po majibizano ya risasi baina
ya waandamanaji na Polisi. Zaidi askari walionekana wakiua
kikatili watu wakubwa kwa wadogo waliokuwa wanakimbia ili
kujiokoa.
Hapakuwa na vita wala hali ya hatari iliyokuwa imetangazwa na
Rais kwa mujibu wa Ibara ya 32 (1) na (2) ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania hivyo maelezo ya tume kuwa
waandamanaji walihatarisha usalama wa taifa hayana ukweli na
msimamo wa Serikali kuwa ilibidi kutumia nguvu kubwa kupitiliza
kuwadhibiti waandamanaji kurejesha a mani na usalama w a nchi
siyo ya kweli na hayana uthibitisho wowote.
Serikali imeki uka Sheria na mikataba ya kimataifa inayoweka
ukomo wa kutumia nguvu kupitiliza (Necessary, Proportional and
Reasonable force) kwani nguvu iliyotumika si ya busara haina

43

uwiano na kosa wala haikuwa na ulazima hii ni kinyume na Ibara
ya 31 (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, PGO
na Sheria ya Matumizi ya Silaha na Risasi pamoja na mkataba wa
African Charter on Human and People‟s Rights.
Haki za binadamu hazitekelezwi kwa utashi w a mtawala bali
zinalindwa kisheria na mikataba ya kimataifa (International
Human Rights Law, The United Nations Conventional on Civil and
Political Rights of 1966 and The Universal Declaration on H uman
Rights 1948).
Mwandishi wa vitabu huko India, Radhakrishnan Pillai katika
kitabu chake cha Corporate C hanakya alisema ni mwiko kwa
kiongozi kutoa adhabu inayovuka mipaka ya sheria. Nanukuu
“never ever try to do any serious injury that goes beyond
the law” mwisho wa kunukuu.
Serikali ilivuka mipaka ya Katiba na Sheria kwa kutumia nguvu
kupitiliza na kusababisha mauaji na ulemavu wa kudumu kwa raia
wasio na hatia.
(V) Madai ya Waandamanaji walikuwa wafuata
mkumbo
Maelezo ya Tume hayaeleweki na hayaaminiki kwa kuwa yana
mkanganyiko mkubwa, awali Tume ilieleza kuwa wananchi
wanazo sababu kuu 5 zilizopelekea kuwepo maandamano
ambazo ndani yake kuna vipengele 20 na kwa kweli kwa uzito
wa hoja hizo waandamanaji walikuwa na sababu za msingi za
kuandamana na hivyo kitendo cha kuwatuhumu kuwa walifuata
mkumbo ni madai ya uongo. Mashujaa hao walielewa fika
wanachokifanya kuwa ni kulikomboa upya taifa lao.

44

5. MASUALA YA KIUCHUMI
Serikali ya awamu ya 6 iliruhusu rasmi wizi wa fedha na mali za
umma ambapo watumishi wa umma waliambiwa wale kwa urefu
wa kamba, watuhumiwa wa u fisadi kutangazwa kwa majina ili
waone aibu badala ya kuchukuliwa hatua za kutumb uliwa na
kufikishwa mahakamani, huku uzembe kwa watumishi wa umma
nao ukapewa baraka hadi kufikia 40%.
Kama nchi tulipitisha Sheria mbili mwaka 2017 za kulinda raslimali
za T aifa “The Natural Wealth and Resources (Permanent
Sovereignty) Act No. 5 of 2017 na The Natural Wealth and
Resources Contracts (Review and Re -Negotiation of
Unconscionable Terms) Act No. 6 of 2017 ‟” Maamuzi na Mageuzi
haya yalisisimua Afrika na dunia nzima kwa nchi ya Tanzania
kuongeza uwazi na uwajibikaji na kuzidisha mapambano ya ulinzi
wa raslimali na fedha za Umma. Lakini leo hii Serikali ya awamu
ya 6 inavunja sheria hizi kila uchao na hazisimamiwi tena.
Wizi huu mkubwa kupindukia u nachelewesha mageuz i ya
Kiuchumi na maendeleo, Taifa kuingia kwenye orodha ya nchi
zenye mzigo mkubwa wa madeni (Heavily Indebted poor Country-
HIPC).
Huku tofauti ya kipato kati ya wenye nacho na wasionacho ikizidi
kuongezeka (Gini coefficient) takriban sehemu kubwa ya uchu mi
mkubwa wa nchi yetu unashikiliwa kundi la watu wachache na
raia wa kigeni (Mafisadi wachache). Huku watumishi wa umma
wakilipwa ujira mdogo usioendana na hali halisi ya ugumu wa
maisha na hivi majuzi kwenye sherehe za Mei Mosi 2026
watumishi wa umma wam enyimwa kuongezewa mshahara kwa

45

kisingizio cha fedha nyingi kutumika kwenye uchaguzi wa mwaka
2025 jambo ambalo haliwahusu na uchaguzi sio suala la dharura.
Katika uchaguzi wa mwaka 2025 tumeshuhudia ufuajaji mkubwa
wa fedha za umma uli opitiliza ikiwemo T ume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi kuwanunulia na kuwagawia wagombea wa urais magari
mapya ya kifahari 19 kwa ajili ya kuendesha kampeni ya siku 60
kwa madai kuwa ni kuweka usawa katika kampeni (level playing
field).
Huwezi kutumia fedha za umma zaidi ya Tsh. Bilioni 10 kununua
magari 19 kwa kampeni za siku 60 wakati ungeweza kukodi
magari kwa wagombea wote kwa fedha zisizozidi Tsh. Milioni 500
tu. Kama hiyo haitoshi hadi leo hakuna uthibitisho kama magari
hayo yamerejeshwa serikalini, pia tulishuhudia Rais aki badilisha
magari kwa sababu ya awamu yake ya kwanza imekwisha na sio
magari hayo kuwa yamechakaa haya ni matumizi mabaya
yaliyopitiliza ya fedha za umma.
Nikiwa mgombea wa Urais nilikataa gari hilo kwa kuwa niilijua ni
matumizi mabaya ya fedha za umma, chanzo cha fedha
hakikuwekwa wazi na kwamba kasma hiyo haikuwemo katika
bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026. Madai ya kuwa na uwanja
sawa haikuwa na mantiki yoyote kwa kuwa INEC ilikuwa
imeengua wagombea wengi wa upinzani kwa nafasi za Udiwani,
Ubunge na Urais. Lakini pia suala la malipo ya mawakala liliachwa
mikononi mwa wagombea na Vyama vyao hivyo suala la gari
pekee haliwezi kuwa kigezo cha kuleta usawa katika uchaguzi bali
ilikuwa ni mambo binafsi yaliyojificha nyuma ya pazia.

46

Hata kilichoelezwa na Tume ya Jaji Chande kuhusu kiwango cha
nchi kuaminika katika kukopa kutokana na tathmini iliyofanywa na
Kampuni ya Moody‟s na nchi yetu kupewa kiwango cha B1,
watanzania tusiaminishwe na vigezo vya kampuni hiyo pekee
kwani ukweli tunaujua kuhusu deni la Serikal i ambapo vigezo vya
uhimilivu vilivyowekwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) vya
deni la Serikali vinakaribia kufikia ukomo uliowekwa (Thresholds
or Borrowing ceilling limit).
Hadi kufikia Februari 2026 Deni la Serikali limeongezeka kwa Tsh.
Trilioni 54.3 kiasi ambacho ni karibia sawa na Deni lote la nchi
yetu la tangu Uhuru miaka 65 iliyopita lakini pia uwiano wa Deni
la Serikali kwa pato la taifa ( Debt-to GDP Ratio) umefikia 44 %
wakati ukomo ni 55% imebaki 11 % tu kufikia ukomo. Uwiano wa
ulipaji wa deni la Serikali kwa mau zo ya huduma na bidhaa nje
(Debt Service to Export Ratio) umefikia ni 17% wakati ukomo ni
15-20%, hivyo tumeshavuka ukomo na ukomo wa mwisho
tumebakiza 3%, uwiano wa ulipaji wa deni kwa mapato (Debt
Service to Revenue Ratio) ni 14.5% wakati ukomo ni 18% hivyo
tumebakiza 3.5% tu kufikia ukomo.
Pia Wafadhili wengi wamepunguza misaada na mikopo ya
masharti nafuu na hivi sasa taifa limebebeshwa mzigo mkubwa
wa riba kutokana na mikopo mikubwa ya Kibiashara ( Commercial
Debt Share) ambayo imefikia 35.8% kiwango hiki ni kikubwa
kwani inatakiwa iwe chini ya 20%. H atari nyingine ni kwamba
takriban 70% ya deni hili liko kwenye Dola za Marekani na hivyo
mtikisiko wowote wa kushuka thamani kwa Tanzania Shilingi dhidi
ya Dola kunapelekea kuongezeka kwa deni la Serikali (High Forex
and Currency Risks).

47

Tulipofanyiwa tathmini ya uhimilivu (Debt Sustainability Analysis)
na IMF, World Bank, Tanzania Investment Centre and
Consultant Group Limited -TICGL pamoja na maelezo kuwa
deni ni himilivu lakini ta asisi hizo zimetahadharisha kuwa nchi
yetu iko kwenye hatari kubwa ya kuvuka viwango vya ukomo wa
mikopo vilivyowekwa (High Vulnerability).
Huku deni la Serikali likiripotiwa kuongezeka kwa kasi isiyokuwa
ya kawaida na fedha kutengwa kila mwaka lakini ni dhahiri kuwa
zimekuwa bajeti hewa na fedha kutafunwa. Mfano ujenzi wa Reli
ya SGR wa Lot 3 (Makutupora -Tabora) umefikia 14.53% na Lot 4
(Tabora-Isaka) umefikia 6.65% wakati mkataba hii yote ilipaswa
kukamilika Disemba 2025. Mradi wa Lot 6 (Tabora -Kigoma) uko
umefikia 7.88% wakati mkataba ulitakiwa kuwa umemalizika
ifikapo Juni 2026, Lot 5 (Mwanza -Isaka) mradi umefikia 68.77%
wakati mradi ulipaswa kumalizika Disemba 2024.
Kwa kifupi miradi ya SGR imetelekezwa katika kipindi chote cha
miaka 5 licha ya Serika li kuripotiwa kukopa zaidi ya kiwango
kilichoidhinishwa kwenye bajeti na sasa inadai tena kupata mkopo
mpya ya zaidi ya Trilioni 3.32 kwa ajili ya SGR. Swali la kujiuliza
mikopo ya nyuma imeenda wapi iliyokuwa ikichukuliwa kwa zaidi
ya 100% kila mwaka wa fedha?
Ujenzi na ukarabati wa barabara unasuasua, Mtandao wa
Barabara za Lami na changarawe tulionao kwa sehemu kubwa
umechakaa na barabara maeneo mbalimbali nchini zimejaa
mashimo matupu na kusababisha ajali na usumbufu mkubwa kwa
mabasi ya abiria, magar i ya mizigo na magari madogo (Fully -
Fledged Crisis).

48

6. JUMUIYA ZA KIMATAIFA
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Shirley Ayokor Botchwey
alituma ujumbe maalum mwezi Aprili mwaka 2026 ukiongozwa na
Rais Mstaafu wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera , kufanya
uchunguzi wa awali. Asante sana Dkt. Chakwera na ujumbe wako
kwa kukutana na kufanya mahojiano na wadau wengi muhimu.
Mimi binafsi nashukuru kwa kunipatia nafasi ya zaidi ya saa 3 na
kuwasilisha maoni na mapendekezo yangu yenye Kurasa 70.
Pia itakumbukwa kuwa Bu nge la Ulaya mnamo Novemba 27,
2025 na EU na Balozi za Nchi 16 mnamo Disemba 5, 2025 walitoa
tamko la kutaka Serikali ikabidhi miili ya marehemu kwa Ndugu ili
wakazikwe kwa heshma na kutaka wafungwa wa kisiasa
waachiliwe mara moja bila masharti. Leo ni zaidi ya miezi 6
imepita hakuna utekelezaji wowote uliofanywa na Serikali na kwa
mantiki hiyo maagizo hayo yamepuuzwa.
Sambamba na hilo Bunge la Ulaya Novemba 2025 lilipitisha
maazimio kuitaka Kamisheni ya EU kusitisha mpango wa ufadhili
kwa Tanzania wa Euro Milioni 156 (takribani Tsh. Bilioni 438)
kutokana na ghasia za uchaguzi na ukandamizaji wa kisiasa na
uonevu kwa viongozi wa upinzani.
Licha ya jumuiya za kimataifa kuchukua hatua mbalimbali
kutokana na machafuko yaliyotokea Tanzania lakini Jumuiya za
Afrika AU, SADC na EAC ziko kimya kana kwamba hakuna
kilichotokea. Hadi sasa hakuna kikao chochote kilichoitishwa kwa
ajili ya kujadili hali ya kisiasa nchini Tanzania.
Baadhi ya Jumuiya za Kimataifa kama Wabunge wa Kamati Ndogo
ya Haki za Binadamu ya Bunge la Ulaya walizuiliwa kuja nchini

49

kufuatilia machafuko ya Oktoba 2025 jambo ambalo linazidi
kuiweka mahala pabaya nchi yetu kidiplomasia.
Muswada wa Sheria ume wasilishwa katika Bunge la Seneti la
Marekani na Maseneta wawili Bi. Jeanne Shaheen
(Democratic Party) na Bw. Ted Cruz (Republican Party)
kuhusu ukandamizaji wa demokrasia na mauaji ya Oktoba 2025
nchini Tanzania ambapo Bunge hilo limeombwa kutoa uamuzi
kuiwekea vikwazo nchini yetu katika nyanja mbalimbali jambo
ambalo nchi yetu haijawahi kufikia mahusiano mabaya kiasi hicho
tangu Uhuru kwani na imekuwa ikitambulika kama kisiwa cha
amani.
Maelezo ya Waziri wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ,
Balozi Mahmoud Thabit Kombo kuwa alipeleka barua 25 za
Mheshimiwa Rais kwa mataifa mbalimbali duniani za maelezo
kuhusu machafuko na mauaji ya Oktoba 2025 ambapo naamini
kuwa utetezi huo hauwezi kukubalika mahala popote duniani.
Rais na Serikali yake alishindwa kutoa taarifa rasmi ndani ya nchi
ya kilichotokea Oktoba 2025 akidai mpaka iundwe Tume ya
Uchunguzi ndiyo ije na majibu lakini pia alitoa msimamo na kauli
zinazokinzana na Katiba na Sheria za nchi.
7. UWAZI NA UWAJIBIKAJI KUHUSIANA NA MAUAJI YA
OKTOBA 2025
Kutokana na kudhibitiwa kwa vyombo vya habari vya ndani na
kuwepo kwa makatazo ya wananchi kutokuto ka nje pamoja na
kuzimwa mawasiliano ya Intaneti , taarifa za mauaji ziliibuliwa na
vyombo vya Kimataifa ikiwemo CNN, DW, BBC, AL JAZEERA, VOA
na vyombo vya habari vya nchi jirani hususan nchi ya Kenya.

50

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, s uala la usalama na ulinzi wa
Raia na mali zao ni jukumu kuu la msingi la Serikali hivyo mauaji
ya watu zaidi ya 518 na majeruhi zaidi ya 2,390 kipindi cha
uchaguzi wa Oktoba 2025, Serikali haiwezi kukwepa lawama na
kuwajibika, ilipaswa Rais na watu wengine wanaohusika wawe
wameshawajibika kwa kashfa nzito ya kukatisha maisha ya watu
wasio na hatia wakiwemo walemavu, ombaomba, waandishi wa
habari, Viongozi wa Dini, wagonjwa, watoto, wajawazito, watu
wazima na wazee.
Ni Tanzania pekee katika dunia ya leo ambapo kiongozi mweny e
kashfa nzito kiasi hicho anaweza kuendelea kubaki madarakani na
kuona ni kawaida tu. Kwa mfano, huko nchini Nepal Kiongozi wa
nchi hiyo, KP Sharma Oli amejiuzulu kutokana na kash fa ya vifo
vya watu 22 walioua wa katika maandamano ya kupinga ufisadi
nchini humo.
Taasisi nyingine ambazo haziwezi kukwepa lawama ya
kusababisha machafuko hayo ni pamoja na Msajili wa Vyama vya
Siasa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi na Mahakama ambazo kwa namna moja au nyingine
zilishirikiana kwa pam oja kufanya upendeleo na kuharibu
uchaguzi kwa kuzuia Vyama na wagombea wa Vyama vya
upinzani (ACT WAZALENDO na CHADEMA) kushiriki uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2025 hususan katika nafasi ya Rais na hivyo
kuwanyima wananchi nafasi ya machaguo na hivyo kuamua
kuandamana.
Pia Tume ya Uchunguzi ya Jaji Chande haiwezi kukwepa lawama
kwa kuliingiza taifa kwenye mzozo mkubwa zaidi kwa kutoa

51

taarifa kinzani na kuuficha ukweli iliyoufahamu kutokana na
ushahidi na vielelezo ilivyopokea kutoka kwa wananchi na
Serikali.
Rais na Waziri Mkuu kwa kutoa taarifa zisizoweza kuthibitika na
kusababisha hofu, na mkanganyiko mkubwa kwenye jamii. Dhana
ya uwajibikaji sio mpya nchini kwetu Viongozi mbalimbali
wamewahi kujiuzul u mfano Mzee Ali Hassan Mwinyi na Dkt.
Emmanuel Nchimbi ( wakiwa Mawaziri wa Mambo ya Ndani), Pia
Mheshimiwa Hayati Edward Ngoyai Lowassa (Waziri Mkuu).
Tulimsikia Mtawala anajutia na kusema kungekuwa na uwezekano
angetamani siku zirudi nyuma ili yaliyotokea Oktoba 2025 yawe
hayakutokea na hi storia ijiandike upya i li kufuta doa aliloingia,
hakika majuto ni mjukuu.
Hakuna uwezekano wa siku kurudi nyuma, wala kurejesha uhai
wa watu na viungo vya miili ya binadamu vilivyopotea. Mioyo ya
watanzania na familia za wafiwa zinazovuja damu haziwezi
kupata faraja kwa maneno ya aina yoyote ya kuomba msamaha
isipokuwa Rais mwenyewe kuwajibika.
Rais alikataa ushauri wote uliotolewa na wawakilishi wa wananchi
hadi wengine akawafukuza bungeni , Wazee, Viongozi wa Di ni,
Asasi za Kiraia na S erikali yake ikashindwa kuheshimu hata
Mahakama akiamini anaweza kila kitu matokeo yake ndiyo haya
wahenga walisema Asiyesikia la mkuu, huvunjika guu.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo, Ndg.
Masoud Othman Masoud ambaye pia alikuwa mgombea wa
urais Zanzibar mwaka 2025 alichukua uongo zi na kumfuata Rais
Samia Suluhu Hassan pamoja na Viongozi kadhaa kuwaeleza

52

juu ya viashiria vya kutokea kwa maafa makubwa nchini lakini
hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa hadi kutokea mauaji
makubwa ya Oktoba 2025.
Mzee Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye a lihangaika
kumtafuta Rais na Tume Huru ya Taifa Uchaguzi ili kurekebisha
kasoro za mifumo ya uchaguzi nchini na kanuni za maadili ya
uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ambazo zilikuwa zinakinzana na
Sheria na Kanuni za uchaguzi na kwa kufanya hivyo kungeleta
maelewano ya pamoja kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025
lakini kwa bahati mbaya sana Mzee huyu hakupewa nafasi ya
kikao na ushauri wake ulipuuzwa.
Ushauri mwingine uliotolewa na Wazee mashuhuri kama Mzee
Samweli H. Kassori, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, Mzee
Freeman Aikaeli Mbowe, Marehemu Suleiman Said Bungara
Maarufu Bwege , Mungu amlaze mahala pema peponi, Mungu
ampe kauli thabiti Mzee wetu Ameen. kwa nyakati tofauti tofauti,
walishauri namna bora ya kuendesha uchaguzi huru na wa amani
ambao nao pia waliishia kudharauliwa.
Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi
kusema nanukuu “Chama kitakachopuuza maoni ya
wananchi, kinaweza kikalia kilio asipatikane mtu wa
kukisaidia kupangusa machozi, ninachowaambia CCM na
waambia Vilevile Vyama v ingine, lazima msikilize
wananchi wanasema nini” mwisho wa kunukuu.
CCM inawajibika kwa kuondolewa madarakani kwani hakuna
uwezekano tena wa kuendelea kuwa Chama tawala kwa kuwa

53

Serikali ya awamu ya 6 imekifikisha tamati chama hicho kufuatia
machafuko na mauaji ya Oktoba 2025.

8. HITIMISHO
Pamoja na Tume ya Jaji Chande kupata kigugumizi na
kushindwa kusema ukweli kuwa Rais akiwa Amiri Jeshi Mkuu
na kwa kauli zake zimeacha maswali mengi kuwa huenda yeye
ndiye aliyetoa amri ya kuua waandamanaji na raia wengi ne
ambapo ni matumizi mabaya ya mamlaka aliyopewa na Ibara
ya 148 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
mfano alikiri hadharani kuwa:-
(i) Mtawala ali tamka hadharani kuwa n guvu kubwa
iliyotumika ndiyo nguvu iliyotakiwa kuwadhibiti
waandamanaji kw ani walilenga kupindua Serikali yake
na wale wanaolia watoto wao kufa walitakiwa kuwazuia
kuandamana.

(ii) Mtawala alisema hadharani kuwa k ama isingetumika
nguvu kubwa kuwadhibiti waandamanaji hao hali
ingekuwa mbaya zaidi ya tuliyoyaona na usalama wa
nchi ungekuwa hatarini.

(iii) Serikali ilikataa kutenga muda wa kushiriki mazishi,
kuhani misiba, kushiriki Misa za kuwaombea marehemu
na majeruhi wala kupeperusha bendera nusu mlingoti
kama sehemu ya kuwakumbuka na kuwaenzi mashujaa
hao kama ilivyo mila na desturi y a nchi yetu, mfano
Rais wa awamu ya 3, Hayati Benjamin William
Mkapa alitangaza siku 3 za maombolezo na bendera

54

ya taifa kupepea nusu mlingoti kutokana na ajali ya
kuzama kwa Meli ya Mv Bukoba mwaka 1997.

(iv) Wananchi kuzuiwa kutoka nje na kuzima kwa mtanda o
wa Intaneti kwa siku 6 mfululizo na baadaye
kufunguliwa bila kuelezwa sababu za kufungwa.
Matukio hayo ya uvunjifu wa Sheria na Katiba ya nchi huendana
na kunyamazishwa kwa vyombo vya habari kwa kufungiwa mfano
Jambo Tv, Jamii Forums , Mitandao ya Tiktok , X (Twitter) nk
vingine kupigwa faini na waandishi wa habari kupewa misukosuko
huku nguvu kubwa zikifanyika kuhamisha wananchi kwenye
kujadili ajenda muhimu za kitaifa ili kufunika maovu ya Serikali
yasijadiliwe wala kujulikana kwa umma huku kampeni za
machawa ndani na nje ya nchi zikishika kasi (Sportswashing)
Serikali haijali ukuu wa Katiba wala Sheria za nchi na inafika
mahala hadi Rais kudiriki kusema kuwa „Katiba ya nchi ni
Kijitabu Tu‟ (Crisis of Consitutional Order and Lawlessness)
kinyume na ibara ya 26 (1) na (2) ya Katiba ya nchi mifano
michache inayothibisha kwamba Serikali imekuwa ikivunja Sheria
na Katiba ya nchi kwa kiwango kikubwa kama ifuatavyo:-
(i) Serikali k uingia mikataba ya siri ya raslimali kinyume
cha kifungu cha 12 cha Sheria ya kulinda raslimali na
Ibara ya 9 (c), (d), (j), Ibara ya 27 (1), (2) na Ibara ya
63 (3) (e) ya Katiba Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.

(ii) Kuchukua mikopo nje ya Bajeti na fedha kutokupitia
mfuko mkuu wa Serikali na badala yake kuingia kwenye

55

mifuko ya watu binafsi kinyume na kifungu cha 12 cha
Sheria ya Fedha za Umma Sura ya 348 na marekebisho
yake ya mwaka 2020 na Ibara ya 9 (d), (i), (j) na Ibara
ya 135 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.

(iii) Kutapanya fedha za umma na kuruhusu ziliwe kwa
urefu wa kamb a, Ripoti za CAG kutofanyiwa kazi
kikamilifu kinyume na Kifungu cha 38 cha Sheria ya
Ukaguzi wa Umma Sura ya 418 na Ibara ya 9 (c), (d)
(i), (j) na Ibara ya 27 (1) na (2) ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.

(iv) Kuvuruga uchaguzi kwa kuruhusu kusimam iwa na
Tume ya Uchaguzi batili na kuminya demokrasia kwa
Vyama vya upinzani kinyume na Ibara ya 3, 5 (1), 8 (1)
(a), 13 (1), 15 (1) (2) na Ibara ya 74 ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(v) Kushindwa kulinda raia na mali zao na kunyimwa haki
za kuabudu kinyume na Ibara ya 9 na 19 (1) na (2) ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vyombo vya uwakilishi wa wananchi kama Bunge na Mabaraza ya
Madiwani kudhibitiwa na hata wachache wanaojitokeza kuhoji
mambo ya msingi hudhibitiwa kupitia vikao vya Caucus, kupewa
taarifa nyingi zisizo na kichwa wala miguu wakati wa uchangiaji ili
kupotezewa muda, kunyimwa kuchangia na kusimamishwa vikao
na baad aye kufukuzwa rasmi kwenye vyombo hivyo vya
uwakilishi wa wananchi. Bunge limekuwa sehemu ya kubariki
dhuluma na ufisadi badala ya kuwa chombo cha kulinda maslahi
ya umma.

56

Upande wa Mahakama k uingiliwa na kufanya maa muzi kwa
maelekezo ya Serikali na hili Jaji Mkuu amekuwa akilithibitisha
mara kwa mara huku mamlaka ya uteuzi wa majaji ikitumika
vibaya kufanya up endeleo ili kulinda maslahi binafsi kupitia
mhimili huo.
Msajili wa Vyama vya Siasa hajaishia kuingilia utendaji wa Vyama
vya upinzani bali pia amekuwa akikataa kusajili Vyama vipya vya
Siasa bila sababu za msingi. Mfano Chama cha Independent
People‟s Par ty (IPP) ambapo waanzilishi wa chama hicho
wameamua kufungua shauri Mahakamani dhidi ya Msajili wa
Vyama vya Siasa baada ya kupigwa danadana kwa miaka 4
wakimlalamikia kunyimwa usajili wa chama hicho licha ya
kukamilisha taratibu zote za msingi na hata kul ipia ada ya usajili
wa muda ya Tsh. Milioni 1.
Pendekezo la kuundwa tume nyingine halikubaliki na hatuwezi
kuwa na Tume juu ya Tume tena zinazoundwa na mamlaka ile ile
leo Rais ameteua tena tume ya mrengo mmoja anayooita „Tume
ya Uchunguzi wa Kijinai wa Ma tukio ya Ghasia ya wakati
na baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025‟.
Tume ya uchunguzi wa kijinai imechelewa na haiwezi kupewa
nafasi tena. Mwanadiplomasia mashuhuri nchini Profesa Anna
Tibaijuka alishauri mapema kupitia andiko lake tarehe 15
Novemba 2025 katika mtandao wa X akisisitiza kuundwa kwa
Tume ya K ijaji „Judicial Enquiry ‟ lakini ushauri wake ulipuuzwa.
Leo Serikali inarejea mawazo yake kwa kuchelewa, haitasaidia.
Watanzania na jumuiya za kimataifa haziwezi kusubiri tena.

57

Katika kipindi cha hivi k aribuni Serikali imekuwa na mahusiano
mabaya na viongozi wengi wa kisiasa, Viongozi wa Dini, wazee,
wanaharakati, Wanahabari hasa wakosoaji ambao wamekuwa
wakitungiwa kesi za kubambikwa mara kwa mara ikiwemo Ugaidi
na Uhaini na wengine kuzuiwa kugombea kwa nguvu.
Hatujasahau kesi za Tundu Lisu, Dk t. Malisa, Heche, Mbowe,
Mpina na migogoro kwenye makanisa.
Kama nilivyosema awali Serikali ilishauriwa kikamilifu kabla ya
uchaguzi ili isije kusababisha vurugu lakini m fumo mzima wa
Serikali ulikaidi na kuendelea na zoezi hilo.
Rais Mstaafu wa awamu ya 4, Mzee Jakaya Mrisho Kikwete
kwa kipindi chote cha matatizo yaliyolikumba taifa letu
amechagua kukaa kimya licha ya Viongozi wa nchi na jumuiya
mbalimbali za kimataifa kuja nc hini kufuatilia mauaji ya kika tili
yaliyofanyika Oktoba 2025 . Ukimya wa Mheshimiwa Rais Mstaafu
Kikwete umeleta sintofahamu kubwa kwenye jamii na watu
kujiuliza kulikoni? huku akionekana mataifa mbalimbali duniani
akitafuta suluhu ya migogoro ya kisiasa.
Baada ya kufanya uchambuzi wa muhtsari wa Ripoti ya Tume ya
Uchunguzi ya Jaji Chande nimebaini kuwa:-
(i) Muhtasari wa Ripoti ya Tume ya Jaji Chande
uliowasilishwa kwa umma ulihaririwa (edited) hadi
ukawa skrepa kwa madhumuni ya kuuficha ukweli na
kukwepa uwajibikaji, badala yake Tume ikakimbilia
kutangaza tuhuma bandia kwa marehemu na watu
wengine wasiohusika.

58

(ii) Waandamanaji waliuawa kwa chuki ya Serikali ya
awamu ya 6 kwani walikuwa wanazo haki na kinga
kikatiba na kisheria kitaifa na Kimataifa na siyo kweli
kwamba walitishia usalama wa nchi na vy ombo vya
dola kulazimika kutumia nguvu kubwa kama
ilivyoelezwa na Tume ya Jaji Chande.

(iii) Serikali ina mgongano mkubwa wa maslahi katika
machafuko ya Oktoba 2025 na hivyo ni lazima kitafutwe
chombo huru cha nje ya nchi kitakacho tafuta ukweli,
kushinikiza u wajibikaji na kusimamia mazungumzo ya
amani ili kufikia muafaka wa kitaifa.

(iv) Idadi ya watu waliouawa ni kubwa zaidi ya 518 na watu
waliojeruhiwa ni zaidi ya 2,390 tofauti na ilivyoelezwa
na Tume ya Jaji Chande kwani Tume hiyo imetoa
takwimu zinazokinzana na kuegemea maeneo ya
huduma za afya pekee na pia imeacha maeneo
mengine muhimu kama Katoro, Geita, Kahama,
Tunduma, Bunda, Tarime na Iringa ambayo yaliripotiwa
kutokea vifo vingi pia Tume haikuchukua takwimu
katika maeneo ya mitaa, vitongoji na vijiji.

(v) Pamoja na Tume ya Jaji Chande kupata kigugumizi
kumtaja aliyetoa amri n inaamini mtawala akiwa Amiri
Jeshi Mkuu ndiye aliyetoa amri ya kuua na yey e
mwenyewe amethibitisha hilo mara kadh aa (The White
Elephant in the room is the head of state).

(vi) Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ulisimamiwa na Tume
batili na isiyo halali kwani haikuwa inatambulika
kisheria baada ya kutungwa kwa Sheria mpya ya Tume

59

Huru ya Uchaguzi ya mwaka 2024. Hivyo iliyojiita Tume
Huru ya Uchaguzi ilikuwa ni genge la watu binafsi
lililojitwika m ajukumu ya umma na kusababisha
machafuko na mauaji makubwa nchini.
Matokeo hayo ya uchaguzi yalikuwa batili kwani kwa
sehemu kubwa kura zilipigwa na maafisa wa Tume
Huru ya Uchaguzi badala ya wananchi, kutokana na
udanganyifu huo, Tume imeshindwa ku Gazze tte
matokeo kwenye gazeti la Serikali na hata kwenye
tovuti rasmi ya INEC.

(vii) Mahakama ilichangia kwa kiwango kikubwa machafuko
ya Oktoba 2025 kwa kuruhusu kufungiwa chama cha
Siasa cha CHADEMA kufanya shughuli zake mwaka wa
uchaguzi na kuruhusu uchaguzi ku endelea wakati mimi
mgombea wa Urais wa ACT Wazalendo nikiwa
nimeweka zuio m ahakamani la kuzuia uchaguzi
kufanyika hadi kesi ya msingi ya kupinga kuenguliwa
kwangu itakaposikiliwa na kuamuliwa.

(viii) Waandamanaji walikuwa na sababu za msingi 5 zenye
vipengele 20 kama zilivyoanishwa na Tume ya Jaji
Chande na sio kweli kwamba walifuata mkumbo kama
inavyoelezwa na watawala.

(ix) Bila kudhibiti na kutokomeza kabisa mtandao wa
utakatishaji wa fedha haramu, wizi, rushwa, ufisadi,
ubadhirifu wa fedha na raslimali za umma , amani na
utulivu haiwezi kurejea nchini mwetu.

60

(x) Uhimilivu wa Deni la Serikali uko kwenye hatari kubwa
kwa kuwa deni limeongezeka kwa kasi kubwa na vigezo
vilivyowekwa na IMF kwa sehemu kubwa vinakaribia
kufikia ukomo na taifa kutokopesheka tena kinyume n a
taarifa ya Tume ya Jaji Chande inayotuaminisha kuwa
taifa liko kwenye kiwango cha kuaminika katika ukopaji
kutokana na tathmini ya Moody‟s.

(xi) Mfumko wa bei za bidhaa na huduma, ugumu wa
maisha pamoja na changamoto nyingine zilizopo ni za
kutengeneza kwa m aslahi ya mafisadi wachache
zitakomeshwa muda mfupi baada ya kupata Viongozi
bora katika taifa.

(xii) Madai ya Tume ya Jaji Chande kuwa mali zilizoharibiwa
na kufikia hasara ya Tsh Bilioni 125 hayana uhalali
kwani hakuna uthibitisho wa kuhakikiwa na chombo
chochote chenye mamlaka kisheria kama RITA na
Mthamini Mkuu wa Serikali

(xiii) Tume ya Jaji Chande kwa siku 153 imeshindwa
kukokotoa na kubainisha fidia kwa marehemu na watu
waliojeruhiwa, hasara waliyopata wananchi kutokana
na kuzuiwa kutoka nje na kuzimwa kwa mta ndao wa
intaneti kwa siku 6 mfululizo.

(xiv) Maelezo ya Tume ya Jaji Chande ya mekinzana na Kauli
nyingi za Rais na Waziri Mkuu lakini pia k auli zingine
zimeshindwa kuthibitika kama ambavyo viongozi hao
waliibua tuhuma mbalimbali dhidi ya waandamanaji.

61

(xv) Ninaungana na pendekezo la Tume kuwa ni lazima
kuwepo Baraza la wazee (Fuddy-duddy depo sitory)
katika uendeshaji wa nchi ingawa hata waze e
wachache wanaojitokeza hadharani kutoa m aoni yao
wanapuuzwa na Serikali ya awamu ya 6.

(xvi) Tume imeu kingia kifua mtandao w a utekaji, upotezaji
na mauaji ya wananchi wasio na hatia kwa kushindwa
kusema ukweli sababu za kutekwa na kuuawa na hatua
zinazochukuliwa licha ya kuripoti idadi kubwa ya watu
758 waliotekwa na kupotea katika kipindi cha miaka 3
kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na kati ya
hao watu 245 hawajulikani walipo hadi sasa.

(xvii) Ongezeko la muda wa siku 63 ya Tume ya Jaji Chande
kufanya kazi hali kuwa na uhalali kisheria na pengine
lililenga kupoteza muda, kuchakachua ripoti na kufuja
fedha za umma.

(xviii) Nilienguliwa kugombea nafasi ya Rais katika uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2025 kwa mabavu na kinyume cha
sheria na Msajili wa V yama vya Siasa, INEC na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kumfanya mgombea
wa CCM Samia kukosa ushindani.

(xix) Tundu Antipas Lissu, Mwenyekiti wa Taifa w a
CHADEMA kufunguliwa kesi ya mchongo ya uhaini na
Chama chake kufungiwa kufanya shughuli za kisiasa
ililenga kumdhibiti yeye na Chama chake asishiriki
uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ili kuipa ahueni CCM.

62

(xx) Ninapinga kuanzishwa kwa Tume nyingine chini ya
mamlaka hiyo hiyo ya Rais kwani haitokei kuunda tume
mbili kwa madhila yanayotokana na tuk io moja, hii ni
kuwapotezea muda wananchi, kufuja fedha za umma
na ni ujanja wa kukwepa mchakato wa Mahakama ya

Rais amekimbia na Ripoti ya awali na Tume imeshindwa
kuweka wazi gharama ilizotumia kufanya kazi zake
lakini bila aibu imependekeza kuundwa tena kwa Tume
nyingine.

(xxi) Mtawala hataki Viongozi na watumishi wanaotekeleza
vyema majukumu yao kwa mujibu wa Katiba na Sheri a
za nchi na ndio maana amekuwa na utamaduni wa
kubadilisha watendaji na viongozi waandamizi serikalini
kama nguo , lakini pia wazembe na mafisadi
wanazawadiwa vyeo kila uchao. Hii inaleta hisia kuwa
mtawala huyu hu enda halitakii mema taifa letu la
Tanzania.

(xxii) Licha ya wezi wa fedha za umma kufahamika kwa
majina na vyeo vyao ndani ya Serikali, mamlaka za
mashtaka,upelelezi na uchunguzi za DPP, DCI na
TAKUKURU zimeshindwa kuwakamata na kuwafungulia
mashtaka na inapobidi kutaifisha mali zao.

(xxiii) Taifa limepata an guko kubwa kutokana na Taasisi
nyingi za umma na Kijamii kushindwa kutekeleza
majukumu yake kikamilifu na kwa uhuru kutokana na
taasisi hizo kujaa machawa na makachero mfano

63

Bunge, Mahakama, INEC, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa, Vyama vya Siasa, Vyama vya Wafanyakazi ,
Serikali za Wanafunzi wa Vyuo vikuu, Jumuiya za
Wafanyabishara, Vyama vya Wakulima na Wafugaji nk.

(xxiv) Rais hana mamlaka kikatiba na kisheria kuzuia ripoti ya
umma na hivyo kitendo cha Rais kudai ripoti ya Tume
ni mali yake na isidaiwe na mtu yoyote ni uvunjaji
mkubwa wa Sheria na Katiba ya nchi na kukwepa uwazi
na uwajibikaji.

(xxv) Haitawezekana kuwepo kwa maridhiano bila ya ukweli
kuwekwa wazi (Fact Findings) na Uwajibikaji kwa
yaliyotokea Oktoba 2025 tofauti na m apendekezo
yanayotolewa na Tume ya Jaji Chande ya kuundwa
Tume ya Maridhiano.

(xxvi) Hadi sasa zaidi ya miezi 7 imepita hakuna aliyewajibika
ni danadana tu na kuundiwa tume juu ya tume.
Imekuwa ni jambo rahisi zaidi kwa nchi yetu
kushtakiwa katika Mahakama za Kimataifa ICSID ili
kuhalalisha uuzaji wa raslimali za nchi lakini imekuwa
vigumu Viongozi kuwajibika ICC.

(xxvii) Tume za Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola
iliyoongozwa na Dkt. Lazarus Chakwera, Rais Mstaafu
wa Malawi, ripoti yake inasubiriwa kwa hamu kubwa na
watanzania na tunaamini kuw a itakuwa rejea muhimu
kwa hatua za uwazi na Uwajibikaji.

(xxviii) Jumuiya za Afrika AU, SADC na EAC kushindwa
kushughulikia migogoro na machafuko kiasi kwamba

64

matatizo ya Afrika yanashughulikiwa zaidi na Jumuiya
za Kimataifa badala ya Afrika yenyewe. Kutoa adhab u
ya kuondolewa kwenye jumuiya nchi ambazo
zimepinduliwa kijeshi (Military Coup) , lakini kwa
viongozi walioingia madarakani kwa kumwaga damu za
watu, wizi wa kura na uk andamizaji mkubwa wa
demokrasia jumuiya hizo hazijishughulishi kabisa na
matatizo hayo.
Sababu kuu 5 zenye vipengele 20 zilizoanishwa na Tume ya Jaji
Chande kuwa chanzo cha maandamano zinauzito mkubwa na ni
dhahiri kuwa waandamanaji walikuwa na sababu za msingi za
kuandamana na hawakufuata mkumbo kama ambavyo Tume
inajaribu kutoposha, honger a sana Gen -Z, hongera sana
waandamanaji wote mmejitoa bila kujibakiza kwa taifa lenu,
wengine mmepoteza maisha, wengine mmepoteza viungo vya
mwili na kuwa na ulemavu wa kudumu, historia ya nchi yetu
haitawasahau orodha yenu ipatikane na iunganishwe na
mashujaa wengine waliolipigania taifa letu.
Watanzania wanahitaji Viongozi wenye weledi na uwezo wa ziada
(Will-power) kuwapeleka kwenye mafanikio ya kweli,
Maandamano ya Oktoba 2025 ni ishara ya watanzania kuchoshwa
na S erikali hii iliyoshindwa kuwajibika kik amilifu na ndio maana
walisikika wakiimba na kusema hatumtaki mama Samia,
hatuitaki CCM na tume choshwa na ufisadi nchini ,
tunataka nchi yetu, wengine walisikika wakisema, Ndugu zetu
wametekwa sana, wameuawa sana na wengi hawana
familia, tukaona watanzania kwa pamoja tuungane,
tushirikiane hatumtaki Rais Samia, tunataka nchi yetu

65

Watanzania wamechoka kudhulumiwa, kuibiwa fedha na raslimali
za umma, maisha magumu, kutekwa, kupotezwa na kuuawa,
ndiyo maana walisimama kulipigania taifa lao na ili kurejesha
hesma palipojaa dharau . Mungu azilale roho za mashujaa hawa
na uwakumbuke siku ya mwisho angalia link
- YouTube na

View: https://youtu.be/m4hWpd-kFM?si=JYbbA0CLDl43c7MM
Raha ya Milele, Uwape eeh Bwana na Mwanga wa Milele
uwaangazie, Wapumzike kwa amani. Amina,
Ina Lillahi wa inna Ilayhi Raji‟un.
9. MAONI NA MAPENDEKEZO
Baada ya kufanya uchambuzi hapo juu ninatoa Maoni na
mapendekezo kama ifuatavyo:-
(i) Kuundwa Tume Huru chini ya Umoja wa M ataifa (UN),
Jumuiya ya Madola (Commonwealth) na Umoja wa
Ulaya (EU) itakayohusisha makundi yote muhimu ya
ndani na ya nje ya nchi kufanya uchunguzi kwa uwazi
na bila upendeleo wa upande wowote.

(ii) Kulipa kifuta machozi kwa familia zote za marehemu na
fidia na vifaa saidizi kwa watu wote waliopoteza viungo
vya mwili. Pia kuwarejesha watu 245 ambao
hawajulikani walipo hadi sasa.

(iii) Rais, Msajili wa Vyama vya Siasa, INEC , AG, Mahakama
na wengine waliohusika wawajibike kwa kashfa ya
kusababisha vifo vya watu zaidi ya 518 na majeruhi
zaidi ya 2,390 wasio na hatia il i kuliponya taifa na

66

kudumisha Uwajibikaji (naungana na Maoni ya Tume
kuwa asiwepo mtu wa kutolewa kafara -Sacrificial
Lamb)

(iv) Vyombo vya Dola vikiongozwa na Afande CDF vimtake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
aliyekuwa Waziri wa Fedha (Waziri Mkuu wa sasa)
waeleze yalipo matrilioni ya fedha za um ma yaliyoibwa
na kufujwa, pia vyombo hivyo vi watake Viongozi hao
kuweka wazi jedwali la mikopo na mikataba y ote ya
raslimali iliyoingiwa kwa siri katika kipindi cha uongozi
wao wa miaka 5 iliyopita.

Aidha na ifahamike kuwa jukumu la kwanza la msingi la
Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni
kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.

(v) Tume huru ya kimataifa itakayoundwa pamoja na
mambo mengine ichunguze ukwasi wa baadhi ya
Viongozi wanaotuhumiwa kuiba na kuficha fedha za
umma nje ya n chi na kusaidia kutaifisha mali na fedha
hizo na kuzirejesha nchini na hii ifanyike kwa kuhusisha
Taasisi zinazoaminika kimataifa za uchunguzi wa fedha
(Accredited Financial Investigators-AFI).

(vi) Watanzania wote wazalendo na wenye mapenzi mema
na nchi yetu walioko ndani na nje ya nchi wanaombwa
kufichua mitandao ya wizi na kuweka wazi nyaraka
zinazohusu ufisadi ili umma uweze kuchukua hatua
stahiki za uwajibikaji.

67

(vii) Uchaguzi wa tarehe 29 Oktoba 2025 ufutwe na
kutangazwa uchaguzi mpya ili kuwapa nafasi wananchi
kuchagua Viongozi wanaowataka katika ngazi ya Rais,
Wabunge na Madiwani ili kurejesha umoja,
mshkamano, amani na utulivu nchini.

(viii) Kesi ya kupinga kuenguliwa kugombea Urais iliyopo
Mahakama ya Rufaa kati yangu mimi Luhaga Joelson
Mpina na ACT Wazalendo dhidi ya INEC na AG . Pia kesi
kati yangu mimi Luhaga Joel son Mpina na ACT
Wazalendo dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (RPP)
na AG.

Aidha kesi nyingine ni kati ya ACT Wazalendo dhidi ya
INEC na AG kuhusu uteuzi wa wabunge wa Viti Maalum
zisikilizwe na kuamuliwa haraka ili kutenda haki na
kuwa rejea muhimu kat ika safari ya ujenzi wa
demokrasia nchini.

(ix) Wakati shauri likiwa Mahakama ya Rufaa kusubiri
kusikilizwa na kuamuliwa C hief Justice, Mheshimiwa
Masaju ajitokeze hadharani kuueleza umma wa
watanzania na dunia kwa ujumla status yangu ni ipi
kwa sasa kwani nimekaa kwenye ugombea wa Urais wa
kudumu na endelevu muda mrefu, kwa kuwa yeye
ndiye aliye na kesi yangu na yeye ndiye aliyeshuhudia
kiapo cha Mtawala katika Kambi ya Kijeshi badala ya
Uwanja wa Jamhuri Dodoma kama ilivyozoeleka miaka
yote.

68

(x) Mahakama iache kutumika kisiasa na kuwa sehemu ya
kutakatisha uhalifu na kuwanyima haki wenye haki na
badala yake ijijenge upya kama ilivyokuwa enzi za Jaji
Mkuu, Hayati Fransis Lucas Nyalali.

(xi) Liundwe Baraza la Taifa la Katiba ambalo litateuliwa na
wananchi wenyewe ba dala ya Bunge la Katiba
linaloteuliwa na Rais , Katiba ya Wananchi haiwezi
kuandikwa na wateule wa Rais na Viongozi wa Chama
cha Mapinduzi. Ripoti ya Tume ya Jaji Warioba itumike
kama rejea na funzo kubwa. Katiba mpya ipatikane
mapema mwaka 2027 badala ya m waka 2028
ilivyopendekezwa na Tume ya Jaji Chande.

(xii) Vyuo vikuu vya nchi yetu viruhusu midahalo ya Wasomi
ambayo italiokoa taifa kama tulivyoshuhudia hivi
karibuni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais
Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Chuo Kikuu ch a
Havard Ma rekani anatoa mhadhara kwenye mdahalo
lakini chuo chake midahalo haifanyiki kama
ilivyozoeleka miaka ya nyuma katika u kumbi wa
Nkrumah (Nkrumah Hall) ambao ndio uliokuwa
chemchem ya mageuzi ya kifikra nchini.
Mwisho nimalizie kwa kutoa masikiti ko yangu juu ya Raslimali za
taifa letu ambazo tumezilinda kwa machozi, jasho na damu na
wivu mkubwa tangu Uhuru mwaka 1961, leo zinauzwa na
kumilikiwa na watu binafsi tena kwa siri. Fedha za umma
zinatapanywa na kupelekea huduma za Kijamii na Kiuchumi kwa
wananchi kudorora. Kwa mwendo huu watoto na wajukuu wetu
watakuja kurithi nini?

69

Kwa nchi yetu ilipofikia kwa sasa lawama hizi tunapaswa tuzibebe
watanzania wote kwa kutotimiza Wajibu wetu kikamilifu tuliopewa
na Katiba na kuingia kwenye mtego wa ushabiki uliopitiliza wa
Vyama vya Siasa na michezo, Vyama vya upinzani kukosa umoja
na mshikamano na mambo ya kung‟ata na kupuliza hivyo
kushindwa kutimiza w ajibu wao kikamilifu katika kuisimamia
Serikali.
Wazee ni mizizi na shina la ustawi wa taifa letu. Nchi yetu imebaki
yatima hasa baada ya Wazee wengi na wenye uzoefu mkubwa
waliowahi kushika nyadhifa za juu kwenye Utumishi wa umma
kuchagua kunyamaza hata pale mambo yanapoharibika hii ni
kutokana na Viongozi hao kukosa uzalendo na kutegemea fadhila
ya teuzi za mtawala na kuliacha taifa linaangamia.
Pia nashindwa kujizuia kuwapongeza sana Viongozi wetu wa Dini
ya Kiislamu na Kikristo kwa kuwa na msimamo thabiti na k ukataa
kuyumba wala kuyumbishwa katika kipindi hiki kigumu nchi y etu
inapitia. Aidha nawapongeza wazee wetu Jaji Joseph Sinde
Warioba, Profesa Anna Tibaijuka, Mzee Samweli Kasori kwa
msimamo thabiti. Pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika
(TLS) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Aidha pamoja na yote tunayopitia kwa sasa kama taifa niwaombe
Ndugu watanzania wenzangu tujipe moyo ushindi unakuja na
kwamba YANA MWISHO HAYA.
Asanteni kwa kunisikiliza,
Luhaga Joelson Mpina
Aliyekuwa Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT
Wazalendo mwaka 2025
 
Attachments

BURIANI MASHUJAA WETU

YANA MWISHO HAYA

TAARIFA KWA UMMA YA NDG. LUHAGA JOELSON MPINA, KUHUSU UCHAMBUZI WA MUHTASARI WA RIPOTI YA TUME YA RAIS YA KUCHU NGUZA MATUKIO YA GHASIA
NA UVUNJIFU WA AMANI YALIYOTOKEA WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2025 , LEO TAREHE
1 JUNI 2026, DAR ES SALAAM.

JUNI, 2026

ii

YALIYOMO

hizi ni poroja tu za kupotezea watu muda :1Head:
 
BURIANI MASHUJAA WETU

YANA MWISHO HAYA

TAARIFA KWA UMMA YA NDG. LUHAGA JOELSON MPINA, KUHUSU UCHAMBUZI WA MUHTASARI WA RIPOTI YA TUME YA RAIS YA KUCHU NGUZA MATUKIO YA GHASIA
NA UVUNJIFU WA AMANI YALIYOTOKEA WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2025 , LEO TAREHE
1 JUNI 2026, DAR ES SALAAM.

Bonyeza HAPA kupakua Hotuba yake

View attachment 3599993

Duuh tunakazi sana
 
Sasa hapa wale vidampa na wazee wa buku saba mkija humu mje na factors za kupinga hoja za mpina, na sio kumtukana sababu ya hizo buku saba mnazopewa!!
 
Sikumuelewa Mpina, kumbe Tanzania kama Nchi tuna watu wazuri wa Akili,Kuna Haja ya katiba mpya!Tutakula mbele kuliko Nchi zote za Afrika, Maana madini tunayo,ardhi yenye rutuba tunayo,Bandari tunayo,Mifugo tunayo.Tunapokwqma ni watu Wachache kumiliki maamuzi na uchumi.Tlaahtlaah, Mwashambwa na wengineo,acheni ushabiki wa vyama.
 
Ingesindikizwa na ule wimbo wa @& '?%,,.. Mzee Chande......
 
Taarifa imeshiba kwelikweli.
Mungu ambariki sana ndugu Luhaga J. Mpina kwa kazi njema hii iliyotukuka.
 
Ni jambo la kutia moyo kwamba bado watu wenye akili wamo nchi hii
 
Back
Top Bottom