Full Time: 4 Yanga Vs 0 Njombe Mji uwanja wa Uhuru Dar, Ligi kuu Tanzania bara

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Mpira tayari umeanza, tuwe pamoja kwa updates..

Kikosi cha Yanga SC: #VPL Ramadhan Kabwili, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Said Juma, Kelvin Yondani, Maka Edward, Raphael Daud, Papy Tshishimbi, Pius Buswita, Obrey Chirwa, Emmanuel Martin.

SUB: Kakolanya, Mhilu, Mahadhi, Matheo, Said Musa, Baruan Akilimali.

Kikosi cha Njombe Mji: #VPL Rajab Mbululu, Agathon Mapunda, Harerimana, Ahmed Adewale, Raban Kambole, Aden Chepa, Willy Mgaya, Juma Mpakala, Ettienne Ngiladjoe, Ditram Nchimbi, Claide Wigenge.

SUB: Kissu, Sagala, Mwambungulu, Mwasondola, Siame, Obash, Kibabage.


Kipyenga tayari kishapulizwa na mpira umeanza

Timu zote zinashambuliana wa zamu..

Yanga wamefunga goli ila likakataliwa maana mchezaji Pius Buswita alikuwa offside

16' Yanga wanafanya shambulizi hapa kwenye lango la Njombe mji kupitia kwa shishimbi ila Njombe mji wanakataa

18' Njombe mji wanapata kona ya pili

20' Hakuna goli kwa pande zote

21' Ditram Nchimbi anafanyiwa faul na anagangwagangwa uwanjani, faulu inapigwa kuelekea lango la Yanga

Njombe Mji wanaonekana kucheza kwa umakini wakijilinda na kwenda mbele kwa kushtukiza

29' Fauli inapigwa kwenye lango la Njombe Mji

29' Faulu nyngine kuelekea lango la Yanga, ila anaondosha Juma Makapo

31' Njombe mji wanashambulia lango la Yanga kwa shuti kali lakini, golikipa wa Yanga Ramadhani Kabwil anaipangua na inakuwa ni kona

35' Yanga wanapata kona ya tatu lakini shishimbi anapiga shuti ambalo halijazaa matunda

38' Yanga wanafanya shambulizi matata baadaya Gadiel Michael kupokea pasi na kudribo mpira lakini mabeki wa Njombe Mji wanamdhibiti.

40' Yanga wanafanya shambulizi kupitia kwa Emmanuel Mrtini lakini anajikuta anatoa mwenyewe na inakuwa ni goal kick

42' Yanga wanapata kona ya nne

43' Yanga wanapata kona ya tano, Yanga wanajitahidi kujipanga kupata goli lakini Njombe Mji wanawadhibiti kwa umakini

45' Yanga wanapanga shambulizi hapa lakini Shishimbi anapiga nje inakuwa ni goal kick

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimemalizika kwa matokeo ya 0 Yanga na 0 Njombe Mji


Kipindi cha pili kinaanza

Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

47' Obrey Chirwa afunga goli kwa upande wa Yanga baada ya kupokea pasi safi toka Pius Buswita

48' Njombe mji wanapata ya tano, lakini kipa anaidaka

51' Njombe Mji wanafanya shambulizi kwenye lango la Yanga lakini haijazaa matunda

52' Faul inapigwa na Yondani kuelekea na lango la Njombe

53' Njombe mji wanapiga kona lakini haijazaa matunda

54' Kipa wa Njombe Mji Rajab Mbululu anaonyeshwa kadi nyekundu kwa kudakia nje ya uwanja na kujifanya kujirusha ndani ya eneo la kudakia

58' Yanga wanapiga faul lakini inambabatiza mchezaji wa Njombe Mji

63' Yanga wanapata penati

64' Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

Yanga wanapata goli la pili kupitia mkwaju wa penati ulioingizwa kimiani na Obrei Chirwa.

68' Goooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

Emmanuel Martini anaipatia Yanga goli la tatu baada ya kupiga shuti kali golini na golikipa hajaweza kulidaka.

71' Yanga wanapata kona lakini haijazaa matunda, mashambulizi mengi sasa yanamiminika kwenye lango la Njombe Mji

75' Yanga wanapata kona, kona inapigwa lakini Shishimbi anapiga nje

Emmanuel Martini yuko chini anaugulia maumivu ya mguu

78' Njombe Mji wanafanya mashambulizi kupitia kwa Agatoni lakini hayajazaa matunda

80' Yanga wanapata kona, kona inapigwa ila golikipa wa Njombe Mji anaidaka

83' Yanga wanamtoa Emmanuel Martin anaingia Yahaya Akilimali

87' Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

Obrey Chirwa anaifungia Yanga goli la 4 na kufanya hat-trik yake ya kwanza kwa msimu huu.

90+1' Njombe Mji nao wanajaribu mara kwa mara kwenda kwenye lango la Yanga lakini mipango inagonga mwamba.

90+3' Njombe mji wanapanga mashambulizi ndani ya lango la Yanga lakini mashambulizi hayazai matunda.

Na mpira umekwisha; 4 Yanga, 0 Njombe Mji.
 
36' Hakuna goli pande zote mbili kwa Yanga na Njombe Mji
 
Ila hawa yanga tuache ushabiki hamna mpira wowot wanaocheza yaan team kubwa kama hii iko nyumban dhidi ya njombe mji ila inashindwa hat kupiga pass NNE mfululizo za uhakika yaana njombe mji wanacheza kama wapo sabasaba
 
44' Sasa ni zamu ya Njombe Mji kulishambulia lango la Yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…