Kikosi cha Yanga SC: #VPL Ramadhan Kabwili, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Said Juma, Kelvin Yondani, Maka Edward, Raphael Daud, Papy Tshishimbi, Pius Buswita, Obrey Chirwa, Emmanuel Martin.
SUB: Kakolanya, Mhilu, Mahadhi, Matheo, Said Musa, Baruan Akilimali.
Kikosi cha Njombe Mji: #VPL Rajab Mbululu, Agathon Mapunda, Harerimana, Ahmed Adewale, Raban Kambole, Aden Chepa, Willy Mgaya, Juma Mpakala, Ettienne Ngiladjoe, Ditram Nchimbi, Claide Wigenge.
SUB: Kissu, Sagala, Mwambungulu, Mwasondola, Siame, Obash, Kibabage.
Kipyenga tayari kishapulizwa na mpira umeanza
Timu zote zinashambuliana wa zamu..
Yanga wamefunga goli ila likakataliwa maana mchezaji Pius Buswita alikuwa offside
16' Yanga wanafanya shambulizi hapa kwenye lango la Njombe mji kupitia kwa shishimbi ila Njombe mji wanakataa
18' Njombe mji wanapata kona ya pili
20' Hakuna goli kwa pande zote
21' Ditram Nchimbi anafanyiwa faul na anagangwagangwa uwanjani, faulu inapigwa kuelekea lango la Yanga
Njombe Mji wanaonekana kucheza kwa umakini wakijilinda na kwenda mbele kwa kushtukiza
29' Fauli inapigwa kwenye lango la Njombe Mji
29' Faulu nyngine kuelekea lango la Yanga, ila anaondosha Juma Makapo
31' Njombe mji wanashambulia lango la Yanga kwa shuti kali lakini, golikipa wa Yanga Ramadhani Kabwil anaipangua na inakuwa ni kona
35' Yanga wanapata kona ya tatu lakini shishimbi anapiga shuti ambalo halijazaa matunda
38' Yanga wanafanya shambulizi matata baadaya Gadiel Michael kupokea pasi na kudribo mpira lakini mabeki wa Njombe Mji wanamdhibiti.
40' Yanga wanafanya shambulizi kupitia kwa Emmanuel Mrtini lakini anajikuta anatoa mwenyewe na inakuwa ni goal kick
42' Yanga wanapata kona ya nne
43' Yanga wanapata kona ya tano, Yanga wanajitahidi kujipanga kupata goli lakini Njombe Mji wanawadhibiti kwa umakini
45' Yanga wanapanga shambulizi hapa lakini Shishimbi anapiga nje inakuwa ni goal kick
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimemalizika kwa matokeo ya 0 Yanga na 0 Njombe Mji
Kipindi cha pili kinaanza
Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
47' Obrey Chirwa afunga goli kwa upande wa Yanga baada ya kupokea pasi safi toka Pius Buswita
48' Njombe mji wanapata ya tano, lakini kipa anaidaka
51' Njombe Mji wanafanya shambulizi kwenye lango la Yanga lakini haijazaa matunda
52' Faul inapigwa na Yondani kuelekea na lango la Njombe
53' Njombe mji wanapiga kona lakini haijazaa matunda
54' Kipa wa Njombe Mji Rajab Mbululu anaonyeshwa kadi nyekundu kwa kudakia nje ya uwanja na kujifanya kujirusha ndani ya eneo la kudakia
58' Yanga wanapiga faul lakini inambabatiza mchezaji wa Njombe Mji
63' Yanga wanapata penati
64' Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Yanga wanapata goli la pili kupitia mkwaju wa penati ulioingizwa kimiani na Obrei Chirwa.
68' Goooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Emmanuel Martini anaipatia Yanga goli la tatu baada ya kupiga shuti kali golini na golikipa hajaweza kulidaka.
71' Yanga wanapata kona lakini haijazaa matunda, mashambulizi mengi sasa yanamiminika kwenye lango la Njombe Mji
75' Yanga wanapata kona, kona inapigwa lakini Shishimbi anapiga nje
Emmanuel Martini yuko chini anaugulia maumivu ya mguu
78' Njombe Mji wanafanya mashambulizi kupitia kwa Agatoni lakini hayajazaa matunda
80' Yanga wanapata kona, kona inapigwa ila golikipa wa Njombe Mji anaidaka
83' Yanga wanamtoa Emmanuel Martin anaingia Yahaya Akilimali
87' Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Obrey Chirwa anaifungia Yanga goli la 4 na kufanya hat-trik yake ya kwanza kwa msimu huu.
90+1' Njombe Mji nao wanajaribu mara kwa mara kwenda kwenye lango la Yanga lakini mipango inagonga mwamba.
90+3' Njombe mji wanapanga mashambulizi ndani ya lango la Yanga lakini mashambulizi hayazai matunda.
Na mpira umekwisha; 4 Yanga, 0 Njombe Mji.