kiwatengu
Platinum Member
- Apr 6, 2012
- 18,585
- 16,780
⚽ Azam FC vs Yanga SC
🏟️ Benjamin Mkapa Stadium
🛡️ Community Shield.
📅 11.08.2024
⏰ 7:00pm
#Daimambelenyumamwiko#
Tukutane saa Moja kwa Updates...
Mwanzo mwisho!!
Kikosi Cha Yanga Kinachoanza.
KIKOSI CHA AZAM
Timu zote sasa zinaingia uwanjani ili mchezo uanze kutoka kwa Miamba miwili Yanga SC dhidi Azam FC
Mchezo umeanza sasa.
Dakika 2, Yanga wameaza kwa kasi.
Dakika 4, Max Mpia anakosa nafasi ya kufunga goli.
Dakika 8, Yanga wanajenga shambulizi ila Azam wanaokoa.
Dakika 13, Goooooool Feisal anawapa goli la kuongoza Azam FC.
Dakika 18, goooooooool Dube anawazawashia Yanga.
Dakika 25, Mpira umekuwa wa kasi sana na Diarra anapata kadi ya njano
Dakika 27, Gooooooool Azam wanajifunga na Yanga wanapata goli ya pili.
Dakika 29, Diabi anapata kadi ya njano.
Dakika 30 Goooooool Aziz Ki anapiga msumari wa tatu.
Dakika 35, Azam wanafanya mabadiliko Diabi anatoka.
Dakika 40, Azam wametengeneza nafasi nzuri ya kufunga goli lakini wamekosa kuitumia.
Dakika 2, zimeongezwa kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Dakika 45, za kipindi cha kwanza zimetamatika Yanga SC 3- 1 Azam FC.
Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi sana.
Dakika 50, Bado timu zote zinacheza kwa tahadhari sana hadi sasa.
Dakika 52, Blanco anapiga shuti kali sana Diarra anaisaidia Yanga kwa kuudaka mpira kwa uzuri kabisa.
Dakika 56 , Mudathir anapata kadi ya njano.
Dakika 59, Adam Adam anaingia
Dakika 71, Mzize anachukua nafasi ya Dube na Bakari Nondo anachukua nafasi Mudathir
Dakika 75, Chilambo na Eva Meza wanachukua nafasi Lusajo na Chama anachukua nafasi ya Aziz Ki kwa upande wa Yanga.
Dakika 85, Yanga wanafanya mabadiliko anatoka Pacome anaingia Musonda na Aucho nafasi yake anachukua ya Andambwile.
Dakika 5 zimeongezwa kumaliza mchezo wa leo .
Dakika 92, Goooooool Mzize anapiga msumari wa nne
Naam Dakika 90 zinatamatika katika Dimba la Benjamini Mkapa Yanga SC ni Bingwa wa Ngao ya Jamii.
Full Time: Yanga SC 4 -1 Azam FC.
Nyie Hamuogopi!