Full Time: Bravos do Maquis 3 - 2 Constantine | CAF Confederation

Full Time: Bravos do Maquis 3 - 2 Constantine | CAF Confederation

Mechi hii imechezwa 90+ 7minutes ila ubao ulionesha added minutes ni 4 lakini waarabu wa Algeria(Cs Constantine) wamefurahi tu na refa katoka bila escort kwa kuwa wao walikuwa nyuma kwa 3-2 na waarabu wa kuchovya pale dimbwini Tanzania wapo kimya
 
Hivi sheria ya head to head siku hizi haipo? Au ina apply katika mazingira gani, mbona Simba kapelekwa nafasi ya 3 wakati alimfunga huyu Bravo?
Ipo na inaapply pale wanapokuwa wamecheza game zote mbili( home and away) hivo Simba akimalizana na hawa jamaa itaapply, kwa sasa before second match wanacheki goals scored and goal difference.
 
Head to head haiwezi kutumika hapa kwavile hawajacheza second leg. Wakishacheza second leg wanataangalia kwanza head to head kabla ya magoli. Hapo kilichombeba Bravo ni kuwa kafunga magoli mengi
Seth saint simba ana Magoli machache ya kufunga hivyo lazima akae hiyo nafasi

1. Bavo ana point 6, magoli 6
2. Constantin ana point 6, Magoli 5
3. Simba ana point 6, magoli 4

Wangefungana au lingana magoli ya kufunga na kufungwa wangeangalia H2H nk...
 
Mechi hii imechezwa 90+ 7minutes ila ubao ulionesha added minutes ni 4 lakini waarabu wa Algeria(Cs Constantine) wamefurahi tu na refa katoka bila escort kwa kuwa wao walikuwa nyuma kwa 3-2 na waarabu wa kuchovya pale dimbwini Tanzania wapo kimya
Hapo wa kulalamika alikuwa ni Bravo wala sio Constantine. Dakika ziliongezwa ni 4 lakini wakati inafika dakika 3 na sekunde zake Bravo akapata goli la 3. Kuendelea mpira hadi kufikia dakika 7 ilikuwa ni favor kwa aliyefungwa ili kutafuta goli la kusawazisha huku Bravo wao walitamani kipyenga kililie dakika 4 ilipogotea ili wapate point 3
 
Soma vizuri uelewe nilichoandika usikimbilie kujibu.

Nimeandika kuwa waarabu ikiwa favor kwa wenzao( ambayo essentially siyo favor bali ni haki) wao walalamishi na fujo juu ila hii mechi wameona raha tu kwa kuwa ilikuwa favor kwao
 
Hiyo mentality haipo kwa waarabu peke yake bali kwa timu yeyote ile ambayo inahitaji matokeo positive. Ukiwa una hitaji ushindi na umeshinda basi unatamani mpira uishe, na ukiwa umefungwa huwa ni kinyume chake utatamani mpira usiishe. CS Sfaxien wao walitamani wapate point 1 hivyo htaji lao ni mpira uishe haraka na refa anapoongeza dakika hutamani zile dakika ziende haraka ili refa apulize kipyenga bahati mbaya kwao refa alinogewa na mashambulizi ya Simba, na inaweza moyoni alikuwa anasema "come on Simba bado kidogo tu mnapata goli komaeni" Simba walikuwa na njaa ya kupata goli kwavile wanaona wapo nyumbani na goli moja tu linaweza kubadilisha sura ya kundi. Ni sawasawa na jana Yanga kwa Tp Mazembe, Mazembe walitamani mpira uishe huku Yanga walitamani usiishe wapate kitu. Ndivyo akili ya mchezo huwa hivyo sio swala la waarabu wala wazungu wala waswahili
 
Back
Top Bottom