Huyu Selemani Mwalimu ameshokosa kujiamini sasa hivi hata hajui majukumu yake uwanjani kuwa yeye ni mshambuliaji wa mwisho. Haiwezekani wewe namba tisa nyuma yako yupo fundi Chama (japo si yule OG) pembeni wapo mafundi Libase na Oura sasa we Sele unahangaika nini kurudi mpaka katikati ya uwanja kutafuta mipira au unakimbilia pembeni matokeo yake unapishana na mipira ya mwisho.
Kwa namna Simba inavyocheza sasa hivi huyo Sele alitakiwa awe na kazi tatu tu:-
1. Kupress mabeki wa kati na kipa wa timu pinzani ili wasianze kutengeneza mashambulizi kuanzia nyuma. Hili kafeli kabisa.
2. Kuzunguka ndani ya boksi la 18 tu na kufunga magoli. Hili nalo kafeli pakubwa.
3. Kuruka sambamba na mabeki wa kati wa kwenye mipira yote ya juu. Hapo napo sifuri kabisa.
Ushauri wangu tena kwenye benchi la ufundi la Simba. Pigeni hesabu kujua dakika Sele aliocheza kama namba tisa asili amefunga goli ngapi kulinganisha na magoli yaliyopatikana kwenye mechi mlizotumia "false number nine". Then baada ya hapo mtachagua wenyewe kusuka au kunyoa.