π—™π—¨π—Ÿπ—Ÿ π—§π—œπ— π—˜: Mapinduzi cup: Yanga 1-0 KMKM SC

π—™π—¨π—Ÿπ—Ÿ π—§π—œπ— π—˜: Mapinduzi cup: Yanga 1-0 KMKM SC

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Mechi ngumu sana lakini Wananchi wamepambana mpaka mwisho, KMKM ni wazuri sana chini ya Kocha Hemed Morocco lakini hawakuweza kuwa wababe mbele ya Wananchi, alama tatu kwao.

Sio timu tu kutoka Zanzibar, Ni KMKM, mabingwa wa ligi ya Zanzibar tuliowashinda tena kwa kikosi cha pili, hii ndio maana halisi ya kikosi kipana.

1. Yacouba Sogne anatia matumaini ya kurudi kwenye kiwango chake. Hivyo kwa faida pia ya Azizi Kii, angebakishwa

2. Mudathir...aisee, kaifanya timu iwe kwenye form kwa dakika chache alizocheza, pongezi kwa usajili wake.

3. Ambundo aongeze bidii, kakosa nafasi nyingi za wazi, kwa kifupi kazingua ila tumeamua kumvumilia baada ya kutupooza hasira kwa goli pekee alilofunga.

4. Kambole apewe tu mkono wa kwa heri, ni mzito kupitiliza huenda pia umri umemtupa! Kiufupi hawezi kuwa na msaada wowote ule kwenye timu, katika hili, siwezi kuwa mnafiki.

Boss hukawiaga kula ila halalag na njaaa.

324377853_202284495707105_5572421252049030267_n.jpg
 
uzi umeanzishwa baada ya mechi kuisha..

Haya tujimwambafai Wana WA jangwani tuwazodoe wekundu maana ushindi si ushapatikana πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸƒπŸƒπŸƒπŸƒ
sijui kwanini ma mods hawakuweka uli ule wa kutupa updates, yawezekana nao ni ,,,,,,,,,,,,
 
Angalizo: Kmkm siyo Mlandege. Na utopolo haikuchezesha wakaa benchi kwa asilimia 100
 
Mbumbumbu kwenye ubora wake unateseka ukiwa wapi, mmepeleka kina kibu denis na mmegongeshwa wenzenu wakajaza U20 na wakampiga bingwa mtetezi wa zanzibar
Manyani fc, nashukuru Mungu sikushabikia utopolo
 
Naona uzi umeanzishwa baada ya wachezaji kurudi hotelini...
 
Uzi unaanzishwa saa tisa usiku duhh mlikuwa kwenye mambo yenu yake ya video[emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089]
 
1. Yacouba namuona akirudi kikosini.

2. Mudathir...aisee, kaifanya timu kutulia kwa dakika chache alizocheza.

3. Kambole, hakuwa na games nyingi, bado mapema kum-Judge. Bado ana kitu miguuni.

4. Ambundo kakichafua kinoma noma
Kwa dakika 90 zote nilizomuangalia Kambole; aisee kama kuna uwezekano uongozi ungempa tu mkono wa kwa heri.
Anaonekana bado mzito kupitiliza! Na pia anaonekana umri umemtupa! Kiufupi hawezi kuwa na msaada wowote ule kwenye timu. Na katika hili, siwezi kuwa mnafiki.

Yacouba Sogne anatia matumaini ya kurudi kwenye kiwango chake. Hivyo kwa faida pia ya Azizi Kii, angebakishwa. Na achukue nafasi ya Gael Bihirimana.

Ila siyo Kambole. Timu itafute mshambuliaji wa kumletea ushindani wa kweli Fiston Mayele, kwenye kuzifumania nyavu. Narudia tena baada ya kumuona Lazarus Kambole kwenye mechi ya jana dhidi ya KMKM; nasema BIG NO ❌
 
Hebu tuambie Mlandege yuko nafasi ya ngapi kwenye ligi ya Zanzibar na kmkm yuko nafasi ya ngapi ili tuendelee
Msimu uliopita mlandege alipowafunga alikuwa nafasi ya ngapi? Tuanzie hapo
 
Back
Top Bottom