ipo siku utakufa
Senior Member
- Dec 8, 2016
- 146
- 530
Paul nongaaaaaaaaa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] fursa
Mmmmmh!!Vipiii bado umefurahi
Ndo ivo tena.Leo Vipiiii Jamani Mbona Iviiii.
Inmaana Pengo La Kwasi Linaonekana Ama!!!!
Siku Ovyooo Kabisaa Leo.
Ivi Awa Maaduhi Wanajifanya Kukaza Ivi Alafu Wako Mkiaani kule ndo Nini!!!!!
Kwakweli wamekupa Raha[emoji23] [emoji23] [emoji23]Simba punguzeni kunipa raha
Daaah!!! Okay Not Bad Ila!!!Ndo ivo tena.
[emoji23] [emoji23] [emoji125]Kwakweli wamekupa Raha[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Kafunga kwa msaada wa refaWalisema Okwi hajawahi kufunga nje ya dar...haya sasa
Matokeo mazuri kwa Mwaduni kwani anakwea hadi nafasi ya 8Niko hapa uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga ambapo leo timu ya Mwadui FC inamkaribisha mnyama mkali wa mwituni, Simba SC na nitakuwa nakuletea mubashara yale yanayojiri mpaka pale mchuano huu utapoenda kuisha.
Tuwe pamoja kwa updates: Mwadui VS Simba
Kikosi cha Mwadui FC: Anold Massawe, Revocatus Richard, David Luhende, Joram Mgeveke, Iddy Mfaume, Awesu Awesu, Jean-Marie Girukwishaka, Paul Nonga, Evarigestus Mjwahuki, Miraji Athuman.
SUB: Dionis, Malaki, Salum, Matogolo, Rajabu, Mathias, Salvatory.
Kikosi cha Simba SC: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Juuko Murshid, Yusuph Mlipili, Erasto Nyoni, Shiza Kichuya, Said Ndemla, Emmanuel Okwi, John Bocco, James Kotei.
SUB: Mseja, Ally Shomary, Mavugo, Gyan, Kazimoto, Yassin, Bukaba.
View attachment 696007
Muonekano wa dimba la CCM Kambarage
01' Mpira umeanza
02' Simba wanaendelea kupandisha mashambulizi kwenye lango la Mwadui
03' Timu zote zina uchu wa kufunga magoli lakini mara nyingi wanajikuta ktk kuotea
04'Mwadui wanashambulia lango la simba kupitia kwa Awesu.
05' Mpaka sasa hakuna shambulizi kali kwani timu zinacheza kwa umakini mkubwa hasa safu za ulinzi.
08'Beki wa Mwadui anatoa boko kwa kumpasia John Bocco mpira anadhibitiwa hapa.
09' Faul inapigwa kwenye lango la Mwadui
Goooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
John Bocco anaipatia simba goli la kwanza baada ya faul iliyopigwa na Shiza Ramadhani Kichuya na Bocco akaiunganisha kwa kichwa ikajaa moja kwa moja golini.
10'Mpira unachangamka hapa baada ya simba kupata goli la kuongoza, okwi amekuwa naingia ndani lakini anadhibitiwa inakuwa ni kona, kona imepigwa lakini haijakuwa na madhara.
15'Mwadui wanafanya shambulizi lakini wanatoa nje
17'Okwi anambabatiza beki wa mwadui inakuwa ni kona, Kichuya anapiga kona fupi lakini haina madhara.
20' Kona inapigwa kwa mwadui, inatoka nje na inapigwa tena lakini haina madhara
23'Ndemla anapiga krosi lakini inawapita wenzake na kutoka nje.
25' Bocco kaumia na anagangwagangwa
26'Ndemla anapiga faul, kipa anadaka.
27'Mohamed Hussein anaoneshwa kadi ya njano kwa kuchelewesha mpira
28'Aweso amechezewa faul, faul inapigwa kuelekea lango la Simba.
29'John Bocco anatoka anaingia Mavugo.
31'Faul inapigwa kwenye lango la simba lakini inakuwa haina madhara
32'Miraji athumani anapata nafasi ya wazi baada ya kubakia na kipa lakini anashindwa kufunga.
33'Bocco anapokea shuti lilipigwa kama faul lakini anashindwa kufunga na kujikuta yupo offside.
36' Okwi anapga shuti moja kali lakini kipa analitema.
37'Simba wanaendelea kulisakama lango la Mwadui.
38'Okwi anamchezea beki wa Mwadui faul. Faul inapigwa kwenda lango la simba.
41'Awadhi Juma anapiga shuti kali kuelekea lango la Simba lakini linatoka nje.
44'Simba wanaanzisha tena mashambulizi kwenda lango la Mwadui
45'Kichuya anapiga shuti lakini kipa anaidaka.
45+1' Mwadui wanafanya shambulizi ila wanadhibitiwa
45+3' Mpira ni Mapumziko
Kipindi cha pili45'Kipinidi cha pili kinaanza.
46' Kapombe anarusha mpira kuelekea Mwadui
50'Mwadui wanaongeza mashambulizi, na sasa wanapiga kona lakini inakuwa haina madadhara.
51'Mwadui wanashambulia lakini wanajikuta wapo offside.
55' Miraji Athumani anafanya shambulizi lakini mabeki wa Simba wanamdhibiti.
56'Paul Nonga ameitoa nje baada ya kupigiwa pasi ndeefu
57'Faul inapigwa lango la simba ni karibu kabisa na 18.
59' Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
David Luhende anaipatia Mwadui bao la kusawazisha, baada ya kupiga faul iliyomshinda golikipa Aishi Manula na kuingia moja kwa moja golini.
62' Faul nyingine inapigwa na awesu lakini inakuwa haina madhara
63'Kipa wa Mwadui, Massawe anaoneshwa kadi ya njano baada kudakia nje ya eneo lake.Faulu inapigwa lakini kipa anaipangua na inakuwa kona.
64'Kona inapigwa na inakuwa ni piga nikuge golini na Mwadui wanaokoa, kipa wa Mwadui anagangwa lakini anaamka.
68'Okwi anaangushwa ndani ya 18 na inakuwa ni penalt
70'Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Emmanuel Arnold Okwi anaifungia Simba goli la pili baada kupiga kwa mkwaju wa penat.
75' Awesu Ali anaonyeshwa kadi ya njano na anatolewa nje baada ya kujiangusha ndani ya 18.
76'Aishi Manula anaanzisha.
77'Mavugo anafanya shambulizi kali baada ya kupokea pasi kutoka kwa kichuya lakini anakuwa sehemu mbaya.
78'Okwi anafanya shambulizi moja kwa shuti moja kali ambalo halijalenga goli.
79'Awesu Ali anapiga kona moja nzuri inawapita mabeki wa Simba lakini mwadui wenyewe wanaitoa nje.
81'Faul inapigwa kuelekea simba, anaipiga Joram lakini inaondoshwa.
83'Faul inapigwa kwenda Mwadui na kichuya lakini anadaka Anold Massawe.
84'Juuco Mushi anaonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuwa na kadi mbili za njano.Faul inapigwa lakini haina madhara.
87'Mavugo anatoka na anaingia Paul Bukaba
89'Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo.
Paul Nonga anasawazisha baada ya kupiga kichwa kilichotokana na faul iliyopigwa na kuingia golini.
90+5'Mwamuzi anaudaka mpira na anamaliza.
Mwadui 2, Simba 2
ngapi ngapiKujifariji imo.