Full Time: Simba 0-2 Yanga Taifa 26/9/2015

Full Time: Simba 0-2 Yanga Taifa 26/9/2015

Mods ebu toeni huu uzi, ushapitwa na wakati, kama taifa tuna mambo ya msingi ya kufanya sio watu wako bize kupoteza muda humu!

Sheria ya JF inaruhusu kuomba ban upumzike ,wasiliana na mod watakusaidia
 
Kwa mpira upi? ile butua butua? Yanga hawana mpira, huo ndo ukweli! Mpira wao hauvutii HATA kidogo!

Mkuu usijitoe ufahamu, wenzako wameukubali mziki wa Yanga; Azam, Coastal Union, Prisons, JKT Ruvu na Simba wenyewe wote wanaujua mziki wa Yanga isipokuwa wewe tu! Kumbuka mchezo wa mpira ni magoli na siyo chenga wala pasi.
 
Dah! Anyway, tulokwazika leo tutafurahi trh 26 Oktoba, na tulofurahi leo tatakwazika trh 26 Oktoba. Ole wenu mtaokwazika leo na trh 26 Oktoba.
 

Attachments

  • Malimi for Change.jpg
    Malimi for Change.jpg
    9.8 KB · Views: 329
Last edited by a moderator:
Wamchangani FC
 

Attachments

  • 1443349307263.jpg
    1443349307263.jpg
    39.4 KB · Views: 179
Hahahahaa. Ninafuraha ya ajabu. Simba walichongaaaa
 
Wakuu yamebaki masaa takribani 16 kipenga kipulizwe kuashiria mtanange mkubwa kuanza kati ya Simba na Yanga zote za Dar. Mbali na kuwa ni watani wa jadi timu hizi zina historia kubwa katika mpira wa Tanzania. Mashabiki wana hamasa kubwa wakitegemea mpira na ufundi wa hali ya juu. Kamanda wako ninaahidi kukuletea live updates hapahapa JF kila dakika itakayocheza. Tulia
========

00' Mpira umeanza hapa uwanja wa Taifa

06' Kipa wa Yanga, Mustapha anapiga mpira nje kuashiria kuumia baada ya kudaka mpira wa kona

28' Kiiza anakosa goli baada ya kupewa pasi nzuri na Mustapha kufanikiwa kuutoa

30' Bado milango yote migumu, faulo ya haraka baada ya Awadh wa Simba kuwekwa chini

35' Yanga wanafanya mabadiliko ya wachezaji na Msuva anatoka

39' Hamis Tabwe anaangushwa chini na kugaagaa lakini anaweza kuinuka na kuendelea na mtanange

41' Yanga wanakosa goli baada ya kipa kufanikiwa kuutoa na kuzaa kona ambayo hata hivyo haikuleta mafanikio.

44' :A S soccer:Hamis Tambwe anafanikiwa kuiandikia Yanga bao la kwanza

45+2' Mpira unaenda mapumziko

45' Mpira umerejea baada ya mapumziko

64' Mbuyu Twitte anapewa kadi ya manjano baada ya kucheza ndivyo sivyo

79' :A S soccer:Bao la pili kwa Yanga kupitia kwa Malimi Busungu, Simba 0-2 Yanga

90' Kipa wa Yanga, Mustapha yuko chini na anapewa kadi ya njano kwa kupoteza muda, dakika saba zinaongezwa.

90+8' Mbuyu anapewa kadi ya pili ya manjano na kuwa kadi nyekundu

90+9' Kipenga kinapuliza kuashiria mwisho wa mechi ya leo, Simba 0-2 Yanga.



Sio kwa video hiii...
 
Back
Top Bottom