Fumanizi la mama mwenye nyumba

Fumanizi la mama mwenye nyumba

Mkuu mkuu umri mdogo, ila matukio ndio mazito. Sometime unajiangalia alaf uamini kama ni wewe ndio umepitia yote hayo. Story ya Maza house sio ya kitambo sana, ilikuwa around 2017
kuna kitu kimoja hua unanichanganya unavosimulia ni kama upo umri flani ila ulivolaliza ile story ni kama mtu mzima flani hivi
 
Jambo la kujifunza tusiwape imani wanawake hata kidogo ona mke wa mtu mke wake anawekewa dau hadi la 150K aisee nitakuwa sioi mimi...dadadeq
 
6th Portion:

.... Kama nilivyosema awali, chumba changu na cha jamaa mwingine vimejitenga, kwa hiyo mtu yeyote atakayekuja uelekeo ule, either atakuwa anaenda kwa jamaa au kwangu, maana hakuna njia inayopitia kule zaidi ya ukuta.

Nilivyozama gheto, nikalock mlango na kuzima taa, alaf nikakausha. Faza house kufika pale,alipitiliza mpaka kwenye ukuta kule, Kisha akarudi na kugonga sana mlango, alivyoona kimya akaamsha huku anafoka kwa jazba. Kama nilivyowaambia awali, wapangaji tulikuwa watano, japo alikuja kuongezeka wa sita baadae. Kati ya hao watano, wawili ni Mimi na yule jamaa ambae vyumba vyetu vimejitenga, alaf na hao wengine wanne waliopo upande mwingine. Moja kati ya hao wapangaji wengine, ni jamaa mmoja anafanya kazi tanesco ( mke wake ndiye niliyekuwa namuuliza lile varangati linahusu nini, kabla hatuja sambaratika baada ya kumuona faza house na panga). Huyu jamaa visenti Senti vya hapa na pale alikuwa navyo vingi tu.

Baada ya faza house kufoka sana, mwishowe akaenda kugonga kwenye chumba cha yule jamaa wa tanesco ambae mke wake tulisambaratishwa wote. Gonga sana mlango huku akiamuru wafungue mlango. Mwanamke anaitikia anafungua, lakini afungui. Faza house akasema navunja mlango kama ufungui,alaf gharama utazilipa wewe. Yule mke wa tanesco akaamua kufungua.

Mpaka hapo nikawa sijaelewa mchezo unaendaje. Kwani huyu faza house imekuwaje kaniacha Mimi kaenda kwa jamaa wa tanesco? Nafsi ikaanza kuniambia "Jali usalama wako kwanza, toka humo ndani". Hisia zikakubaliana na huu ushauri, huenda faza house kaona nimekuwa trapped,Sina pa kukimbilia. Nikatoka taratibu mle ghetto, baada ya chumba changu unafatia ukuta, nikaruka ule ukuta japo ulikuwa mrefu, nikaangukia upande wa pili. Nilivyotua tu chini, nilitoka mbio sio za kawaida. Ila nilivyofika Mtaa wa pili, nikajiuliza kwani nakimbizwa? Nikaamua kusimama, nikapitisha wazo la kurudi karibu na home nikasome mchezo.

Kati ya wapangaji wa pale nilipokuwa naishi, kuna jamaa alikuwa bodaboda. Sasa mida ile jamaa ndio alikuwa anarudi ghetto kwake. Nilivyomuona karibia na home, nikajibanza sehemu. Jamaa alipofika home, akamkuta faza house yupo nje na panga lake mkononi. Yule boda alivyoona panga, akahisi faza house alikimbiza mwizi. Faza house analalamika "Haya maisha tu mwanangu, haya maisha tu", Akaendelee "nimemfuma baba nanii (tanesco) na mke wangu". Nilivyosikia hivyo, nikashangaa "Kumbe sikuwa peke yangu?" Baada ya kugundua msala sio wangu, nikajitokeza.

Faza house kuniona anashangaa "Jombaa siulikuwa chumbani kwako?" Nikakataa, akapotezea, ndo kuanza kutupa story. Alikuwa anataka kwenda chooni kujisaidia kabla ya kwenda kulala. Sasa alivyofika usawa wa bafu, akaona khanga ya mkewe ipo mlangoni, akachukulia kawaida kwavile alimuona mkewe wakati anajiandaa kwenda bafuni. Ila alivyofika usawa na dirisha la bafu, akaona kichwa cha baba nanii (tanesco), wakagonganisha macho, ile bafu kidirisha chake kilikuwa kidogo cha wastani, alaf hakina wavu wala nondo. Faza house ikabidi arudi mlangoni chapu, kufika pale mkewe akawa anatoka, hakumjali, akapitiliza moja kwa moja mpaka bafuni. Akamkuta baba nanii (tanesco) anamalizia kuvaa suruali. Yule jamaa wa tanesco alivyomuona faza house, fasta bila hata kujiuliza mara mbili, akaruka na kupita kwenye kile kidirisha, akaangukia upande wa pili kwenye mabati na mbao mbao.

Faza house nae chap akatoka bafuni na kumuwahi jamaa pale nje. Ubaya, kule alipoangukia jamaa, hawezi kutoka mpaka apite aliposimama faza house. Faza house anakwambia, akamvagaa yule jamaa na kumpush mpaka ukutani, jamaa anataka kurudi alipigwa kichwa cha uso. Faza house akawa anatuonesha nundu, maana baada ya kumpiga jamaa, na yeye alitoka nundu. Jamaa wa tanesco alifanikiwa kupata upenyo na kukimbilia nje (ndio muda ule niliosikia purukushani nje getini mpaka nikatoka). Muda huo anatusimulia, mke wa jamaa wa tanesco nae yupo. Ila yule mwanamke akawa hataki kuamini, maana mumewe alishamuaga kuwa anaenda kazini shift ya usiku, sasa iweje akutwe bafuni?. Faza house akamwambia mpigie simu umuulize,jamaa akapigiwa simu,ila akakataa kabisa. Mkewe ndo kumwambia kuwa faza house Yuko na panga anamsubiria.

Baada ya kama nusu saa jamaa akaja na sungu sungu. Faza house alivyomuona akaanzisha varangati. Ila sungu sungu wakamsihi apoe kwanza. Jamaa anaulizwa pale Bado anakataa, ila kumuangalia vizuri, nae ana bonge la nundu usoni. Mkewe anamuuliza, "Ilo nundu umelitoa wapi mume wangu maana wakati unaondoka hukuwa nalo?" Jamaa hatoi jibu la kueleweka. Faza house akamvamia tena, jamaa kuporonyoka akakimbia tena.

Tukabaki tunajadiliana pale. Faza house kushika simu ya mkewe , ndio anakuta msg za jamaa wa tanesco akitoa ofa ya 100k kwa Maza house. Maza house akawa Bado anamkatalia. Jamaa wa tanesco akaongeza mpaka 150k, mwanamke akawa anasita sita, jamaa wa tanesco akamwambia ukienda kuoga nakuja nayo huko huko bafuni 150k. Hapo ndio Maza house kumwambia " Sawa, ila ukikutwa shauri yako". Jamaa akajibu ni chap tu, hatuwezi kukutwa. Bahati mbaya kwao,wakakutwa.

Kimoyo moyo nikawa nawaza, huu msala hata Mimi unaweza kunikuta. Nikapitisha wazo kuhama hata kabla Kodi haijaisha, maana huwezi jua mbeleni yataibuka yapi. Nikaingia zangu gheto nikaangusha. Kesho yake asubuhi nikamwambia dalali anitafutie chumba maeneo fulani hivi, pale natoka.....
W
 
7th Portion:

.... Mida ya alfajir Maza house aliamua kurudi home. Alivyorudi alipewa sana kichapo na mumewe. Mpaka watoto wakaja kutuamsha wapangaji twende tukamsaidie Mama yao asije kuuliwa. Kimoyo moyo nikajisemea "Niende anitaje tupigwe wote?" Nikakausha. Ila baadae alikuja akaacha kumpiga. Siku nzima Maza house hakutoka nje. Mida ya jioni naenda kwa mama ntilie kula, nikakutana na K anatoka dukani. Nikampa pole kwa jinsi alivyopigwa siku ile, akaniambia nisijali yalishapita. Nikamuuliza Maza house anaendeleaje? Akajibu "Hajiskii poa, yupo ndani amelala tu maana ameumia sana miguu na mikono". Nikamwambia akampe pole, akasema sawa. Story zikaisha, tukabaki tumesimama tu. Kishetani kikaja upande wangu "Fanya kweli kabla hujahama"

Nikamuuliza K, "Vipi unaweza kuja leo?" Akajibu anaumwa hawezi kuja, labda baada ya siku mbili au tatu. Nikaelewa yupo period huyu. Nikamwambia basi sawa, tutachek baada ya hizo siku tatu. Tukaagana.

Kesho yake jioni wakaja ndugu wa faza house na Maza house,kwa ajili ya vikao vya upatanishi. Niko nje nachota maji, namsikia faza house anavyobwata, ndugu zake wakawa wanamtuliza. Sikutaka kuwafatilia, nikaendelea na mishe zangu. Nilivyomaliza kuchota maji, nikawagongea ili niwape hela ya maji. Aliyekuja kufungua mlango, mwanzoni sikumtambua ila nilikuja kujua ni mdogo ake na Maza house. Huyu hakuwa mweupe sana kama Maza house, yeye alikuwa kama brown Fulani hivi, ila anamwili mkubwa kuliko Maza house, nyama za kutosha. Nikaanza kujiuliza "Nini hiki naona Mimi? Mbona majaribu hayaishi?"

Yule mdogo ake Maza house (tumuite Mwahija), akaniuliza "nikusaidie Nini?. Nikamwambia nimeleta hela ya maji hii. Akaipokea, alafu akasema " Asante". Tabasamu lake na zile pozi wakati anaongea, zikanivuruga kimtindo. Nikaondoka.

Nafika gheto dalali akanipigia simu kuna chumba kimepatikana, kama Nina muda sasa hivi twende nikakiangalie ili kesho nihamie kama nitaridhika nacho. Nikamuuliza kipo mtaa gani? Akanielekeza, nikamjibu fasta kuwa sijakipenda. Dalali anauliza "Boss hata hujakiona ushasema hujakipenda?. Kama upo busy hata kesho sio mbaya uje ukiangalie.". Nikamwambia nitakuwa busy, aniambie kipoje hicho chumba. Akaanza kuniambia kipo ndani ya fensi, usalama mkubwa, kina tiles n.k. Nikamuuliza kimepigwa rangi? Akajibu ndio, kina ceiling board? Akajibu ndio. Kina tiles za aina gani? Akasema zile zenye urembo urembo kama michoro au maua maua. Nikamwambia sipendi maua hizo tiles sijazipenda, anitafutie chumba kingine. Dalali akawaka "Mkuu siulisema una haraka, mbona unaleta mambo sio?". Nikamwambia kama anaona namsumbua basi aache asitafute, sihami tena. Akawa mpole, akasema atanifutia kingine. Tukaagana.

Huyu Mwahija kwanini hakusubiria nihame ndio aje? Haya majaribu mpaka lini? Nikajaribu kuyapotezea mawazo juu yake, baadae nikalala, siku ikaisha.

Kesho yake sikumuona kabisa, japo nilifanya jitihada zote. Mida ya jioni nikakutana na K akiwa anatoka kununua mkaa. Story za hapa na pale, akaniambia amepona, aje baadae? Nikamwambia siko poa, najiskia vibaya. Akanipa pole. Wakati anataka kuondoka nikamuulizia Mwahija, akaniambia "Ma mdogo kuna sehemu alienda ila leo atarudi". Nikasema sawa .

Baadae kama zali, naenda nje kutafuta msosi, nakutana na Mwahija getini anataka kuingia. Nikamsalimia, akaitikia. Wakati anataka kuingia ndani nikamuuliza "Tokea tulivyoonana juzi, sijakuona tena, kama hauishi humu vile". Akacheka "Kuna mtu nilienda kumtembelea, siunajua nimekuja mjini mara moja tu". Kipindi ananijibu, akawa amefungua geti anataka kuingia ndani. Nikamwambia "Inaonekana una haraka sana, ila nilitamani sana tuendelee kuongea". Akaniuliza "Unataka tuongee kuhusu nini?" Nikamjibu "Vingi tu, ila vinahitaji muda". Akajibu, "Sawa ngoja niwaone kwanza huko ndani, alaf baadae tutaongea". Nikajibu sawa. Akaingia ndani. Nikaanza kujilaumu sijachukua namba.

Nilivyotoka kula, nikawa muda wote nimesimama mlangoni labda atatokeza nimfate, ila wapi. Mpaka inafika saa mbili na nusu sijamuona. Nikachukua ndoo zangu na kwenda kuchota maji. Kila nikichota ndoo moja nailipia, alaf nikifika kule ghetto kwa nyuma naimwaga chini, natulia dakika chache then naenda tena kuchota maji. Mara ya kwanza nilivyoilipia alitoka K, mara ya pili alitoka faza house, mara tatu ndo akatoka Mwahija.

Hakusimama mlangoni, alitoka nje kabisa. Anauliza "Mbona fujo nyingi dogo?" Nikamjibu "Tunamihadi ya kuongea ila hukunipa namba". Akajibu "Ningekupaje namba na hukuomba?". Nikamjibu "Yameshapita hayo, bahati nzuri tupo hapa sasa". Akaniambia "Haya sema unachotaka kusema". Sikujifikiria mara mbili wala sikutaka kujipanga maana ningeharibu, nikamwambia "Nimetokea kukuelewa ghafla, najikuta napenda tu uwe karibu tukiongea kama hivi". Akakunja sura, alaf akawa serious "We mtoto kumbe huna adabu? Unaelewa kweli unachokiongea, mbona kama unanivunjia heshima?". Nikamjibu "Sio wewe tu unayenishangaa, hata Mimi binafsi najishangaa. Sielewi nimekutwa na nini"

Akaniuliza "Unavuta bangi? Mbona huna adabu, Mimi ni kama dada yako au hata mama ako kabisa, maana Nina uhakika nimekuzidi miaka mingi". Nikamjibu " Upo sahihi kwenye kila unachosema, ila binafsi siamini kama nakukosea adabu. Ila pia sipo hapa kukwambia unielewe ninachosema, nilitaka tu usikie maneno yangu, maana kama ungeondoka bila kukwambia ningejilaumu sana". Tulijikuta tunaongea sana, na kwa muda mrefu. Mwisho wa siku akaniambia "Hapa nimekuja kusuluhisha ugomvi wa dada angu na shemeji, sitaki kutia aibu". Nikamwambia "Huwezi tia aibu, maana nitahama hapa ndani ya siku chache zijazo". Akanijibu " Nitakuwa hapa town kwa wiki mbili, hama hapa alaf nitafute. Nikamjibu hakuna shida. Akaniuliza, ila unauhakika na unachokitaka?. Nikamjibu ndio. Akaniuliza, "Na hako kamwili kako utauweza huu mwili?". Nikamjibu "Wewe ndio utaamua niuweze au nishindwe, ila kwa upande wangu maji nimeshayavulia nguo haya". Akacheka, nikamuuliza " Upo tayari niweze au nishindwe?". Akacheka tena "Unaongea sana, siumesema unahama? Haya hama, mengine hayafai kuongelea hapa.".

Nikachukua namba yake, then nikaenda ghetto. Kufika gheto nikamchek yule dalali kumuuliza kama kile chumba bado kipo wazi au kimechukuliwa. Dalali akawa mkali kidogo, ila nikamwambia nilikuwa stressed siku ile. Tukaelewana nikaenda kukiangalia. Process za kuhama zikaanza.

** ** ***** *****

Hellow guys, huwa napenda kuandika story kuhusu Mimi kwa kutegemea na tukio husika. Mlengwa wa kisa hiki alikuwa ni Maza house na lile fumanizi, hatimae tumefikia tamati, maana nilifanikiwa kuhama. Matukio mengine yaliyofatia au ambayo nimeshawahi kukutana nayo katika hii safari ya maisha, nitayaleta independently siku zijazo. Mwahija ni mtu aliyenifanya nikasema Mimi na mashangazi sasa basi, japo huwa nakili, kati ya mashangazi yote, hakuna kama Mwahija.

Nashkuru kwa tuliokuwa pamoja tokea mwanzo.

Until next time,

Wasalaam

Analyse
Aaaaah unakatisha utamu malizia hyo y mwahija
 
Mzee salute sana nimekukubali sana tafuta ntu wa scriot aisee iwe bonge la series
 
Back
Top Bottom