Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tumsaidie tu 😌😋🤤Mr tumezinguana hapokei simu hapa napambana mwenyewe usiku upite.
Dah! Hiyo ya mwahija itakua na heading gani7th Portion:
.... Mida ya alfajir Maza house aliamua kurudi home. Alivyorudi alipewa sana kichapo na mumewe. Mpaka watoto wakaja kutuamsha wapangaji twende tukamsaidie Mama yao asije kuuliwa. Kimoyo moyo nikajisemea "Niende anitaje tupigwe wote?" Nikakausha. Ila baadae alikuja akaacha kumpiga. Siku nzima Maza house hakutoka nje. Mida ya jioni naenda kwa mama ntilie kula, nikakutana na K anatoka dukani. Nikampa pole kwa jinsi alivyopigwa siku ile, akaniambia nisijali yalishapita. Nikamuuliza Maza house anaendeleaje? Akajibu "Hajiskii poa, yupo ndani amelala tu maana ameumia sana miguu na mikono". Nikamwambia akampe pole, akasema sawa. Story zikaisha, tukabaki tumesimama tu. Kishetani kikaja upande wangu "Fanya kweli kabla hujahama"
Nikamuuliza K, "Vipi unaweza kuja leo?" Akajibu anaumwa hawezi kuja, labda baada ya siku mbili au tatu. Nikaelewa yupo period huyu. Nikamwambia basi sawa, tutachek baada ya hizo siku tatu. Tukaagana.
Kesho yake jioni wakaja ndugu wa faza house na Maza house,kwa ajili ya vikao vya upatanishi. Niko nje nachota maji, namsikia faza house anavyobwata, ndugu zake wakawa wanamtuliza. Sikutaka kuwafatilia, nikaendelea na mishe zangu. Nilivyomaliza kuchota maji, nikawagongea ili niwape hela ya maji. Aliyekuja kufungua mlango, mwanzoni sikumtambua ila nilikuja kujua ni mdogo ake na Maza house. Huyu hakuwa mweupe sana kama Maza house, yeye alikuwa kama brown Fulani hivi, ila anamwili mkubwa kuliko Maza house, nyama za kutosha. Nikaanza kujiuliza "Nini hiki naona Mimi? Mbona majaribu hayaishi?"
Yule mdogo ake Maza house (tumuite Mwahija), akaniuliza "nikusaidie Nini?. Nikamwambia nimeleta hela ya maji hii. Akaipokea, alafu akasema " Asante". Tabasamu lake na zile pozi wakati anaongea, zikanivuruga kimtindo. Nikaondoka.
Nafika gheto dalali akanipigia simu kuna chumba kimepatikana, kama Nina muda sasa hivi twende nikakiangalie ili kesho nihamie kama nitaridhika nacho. Nikamuuliza kipo mtaa gani? Akanielekeza, nikamjibu fasta kuwa sijakipenda. Dalali anauliza "Boss hata hujakiona ushasema hujakipenda?. Kama upo busy hata kesho sio mbaya uje ukiangalie.". Nikamwambia nitakuwa busy, aniambie kipoje hicho chumba. Akaanza kuniambia kipo ndani ya fensi, usalama mkubwa, kina tiles n.k. Nikamuuliza kimepigwa rangi? Akajibu ndio, kina ceiling board? Akajibu ndio. Kina tiles za aina gani? Akasema zile zenye urembo urembo kama michoro au maua maua. Nikamwambia sipendi maua hizo tiles sijazipenda, anitafutie chumba kingine. Dalali akawaka "Mkuu siulisema una haraka, mbona unaleta mambo sio?". Nikamwambia kama anaona namsumbua basi aache asitafute, sihami tena. Akawa mpole, akasema atanifutia kingine. Tukaagana.
Huyu Mwahija kwanini hakusubiria nihame ndio aje? Haya majaribu mpaka lini? Nikajaribu kuyapotezea mawazo juu yake, baadae nikalala, siku ikaisha.
Kesho yake sikumuona kabisa, japo nilifanya jitihada zote. Mida ya jioni nikakutana na K akiwa anatoka kununua mkaa. Story za hapa na pale, akaniambia amepona, aje baadae? Nikamwambia siko poa, najiskia vibaya. Akanipa pole. Wakati anataka kuondoka nikamuulizia Mwahija, akaniambia "Ma mdogo kuna sehemu alienda ila leo atarudi". Nikasema sawa .
Baadae kama zali, naenda nje kutafuta msosi, nakutana na Mwahija getini anataka kuingia. Nikamsalimia, akaitikia. Wakati anataka kuingia ndani nikamuuliza "Tokea tulivyoonana juzi, sijakuona tena, kama hauishi humu vile". Akacheka "Kuna mtu nilienda kumtembelea, siunajua nimekuja mjini mara moja tu". Kipindi ananijibu, akawa amefungua geti anataka kuingia ndani. Nikamwambia "Inaonekana una haraka sana, ila nilitamani sana tuendelee kuongea". Akaniuliza "Unataka tuongee kuhusu nini?" Nikamjibu "Vingi tu, ila vinahitaji muda". Akajibu, "Sawa ngoja niwaone kwanza huko ndani, alaf baadae tutaongea". Nikajibu sawa. Akaingia ndani. Nikaanza kujilaumu sijachukua namba.
Nilivyotoka kula, nikawa muda wote nimesimama mlangoni labda atatokeza nimfate, ila wapi. Mpaka inafika saa mbili na nusu sijamuona. Nikachukua ndoo zangu na kwenda kuchota maji. Kila nikichota ndoo moja nailipia, alaf nikifika kule ghetto kwa nyuma naimwaga chini, natulia dakika chache then naenda tena kuchota maji. Mara ya kwanza nilivyoilipia alitoka K, mara ya pili alitoka faza house, mara tatu ndo akatoka Mwahija.
Hakusimama mlangoni, alitoka nje kabisa. Anauliza "Mbona fujo nyingi dogo?" Nikamjibu "Tunamihadi ya kuongea ila hukunipa namba". Akajibu "Ningekupaje namba na hukuomba?". Nikamjibu "Yameshapita hayo, bahati nzuri tupo hapa sasa". Akaniambia "Haya sema unachotaka kusema". Sikujifikiria mara mbili wala sikutaka kujipanga maana ningeharibu, nikamwambia "Nimetokea kukuelewa ghafla, najikuta napenda tu uwe karibu tukiongea kama hivi". Akakunja sura, alaf akawa serious "We mtoto kumbe huna adabu? Unaelewa kweli unachokiongea, mbona kama unanivunjia heshima?". Nikamjibu "Sio wewe tu unayenishangaa, hata Mimi binafsi najishangaa. Sielewi nimekutwa na nini"
Akaniuliza "Unavuta bangi? Mbona huna adabu, Mimi ni kama dada yako au hata mama ako kabisa, maana Nina uhakika nimekuzidi miaka mingi". Nikamjibu " Upo sahihi kwenye kila unachosema, ila binafsi siamini kama nakukosea adabu. Ila pia sipo hapa kukwambia unielewe ninachosema, nilitaka tu usikie maneno yangu, maana kama ungeondoka bila kukwambia ningejilaumu sana". Tulijikuta tunaongea sana, na kwa muda mrefu. Mwisho wa siku akaniambia "Hapa nimekuja kusuluhisha ugomvi wa dada angu na shemeji, sitaki kutia aibu". Nikamwambia "Huwezi tia aibu, maana nitahama hapa ndani ya siku chache zijazo". Akanijibu " Nitakuwa hapa town kwa wiki mbili, hama hapa alaf nitafute. Nikamjibu hakuna shida. Akaniuliza, ila unauhakika na unachokitaka?. Nikamjibu ndio. Akaniuliza, "Na hako kamwili kako utauweza huu mwili?". Nikamjibu "Wewe ndio utaamua niuweze au nishindwe, ila kwa upande wangu maji nimeshayavulia nguo haya". Akacheka, nikamuuliza " Upo tayari niweze au nishindwe?". Akacheka tena "Unaongea sana, siumesema unahama? Haya hama, mengine hayafai kuongelea hapa.".
Nikachukua namba yake, then nikaenda ghetto. Kufika gheto nikamchek yule dalali kumuuliza kama kile chumba bado kipo wazi au kimechukuliwa. Dalali akawa mkali kidogo, ila nikamwambia nilikuwa stressed siku ile. Tukaelewana nikaenda kukiangalia. Process za kuhama zikaanza.
** *** *****
Hellow guys, huwa napenda kuandika story kuhusu Mimi kwa kutegemea na tukio husika. Mlengwa wa kisa hiki alikuwa ni Maza house na lile fumanizi, hatimae tumefikia tamati, maana nilifanikiwa kuhama. Matukio mengine yaliyofatia au ambayo nimeshawahi kukutana nayo katika hii safari ya maisha, nitayaleta independently siku zijazo. Mwahija ni mtu aliyenifanya nikasema Mimi na mashangazi sasa basi, japo huwa nakili, kati ya mashangazi yote, hakuna kama Mwahija.
Nashkuru kwa tuliokuwa pamoja tokea mwanzo.
Until next time,
Wasalaam
Analyse
Tatizo la bongo movie sio script, Bali ni budget. Hiyo ndio inaharibu movieComrade tengeneza tamthilia ya muendelezo (series) tafuta na director, hii ni fursa... siku hizi Africa magic swahili kuna tamthilia kedekede zinazovutia za kibongo... Hii inaweza ikawa ni mojawapo au ikawa nzuri zaidi, imejaa mafunzo na burudisho la aina yake.
Nashauri Usiendelee na hicho kisa cha "Mwahija" bali uunganishe na kisa cha kwanza utengeneze tamthilia, hawa waliomo humu watakuwa wafuatiliaji, watazamaji na mashabiki wako wakuu wa kuanza nao.
Kwa Mwahija nitarudi [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]Dah! Hiyo ya mwahija itakua na heading gani
View attachment 2422495
Noma na nusu mzee! Ila pale kati kale katoto kamezima nahisi hata mishipa ya genye ilisinyaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kwa Mwahija nitarudi [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Tatizo la bongo movie sio script, Bali ni budget. Hiyo ndio inaharibu
Exactly! As i said watu ndo mtaji na kama kweli una nia Comrade bakuli linapita na unatoa kitu saaaafi! Wananchi wanaburudika na ujumbe unaufikia hadhira.Tatizo la bongo movie sio script, Bali ni budget. Hiyo ndio inaharibu movie
Mwahija anamkasa wake. Tukijaaliwa, nitauleta
Moyo ulikuwa unadunda hadi nikawa nahisi mtu akipita nje anaweza kuusikia. Nilikuwa natoka jasho balaa[emoji28][emoji28][emoji28]Noma na nusu mzee! Ila pale kati kale katoto kamezima nahisi hata mishipa ya genye ilisinyaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hawa wamama wenye nyumba haswa mishangazi kuna siku watatufanya vibaya, kuna mahala nilipanga zamani kidogo, mama mwenye nyumba alinipenda sana kiasi kwamba alikua anagombana na wapangaji wengine kwa sababu ndogo ndogo zilizokua zinanipa kero na akawaambia kabisa, atakae 7bbisha huyu kuhama atahama nae[emoji1787][emoji1787] mf, usafi alikua hataki kabisa kusikia nimehusishwa kwenye zamu za usafi na ishu ya umeme ilikua mtihani wapangaji kama sita mita moja inafikia mnanunua umeme wa mia5, usiku kucha mtu ana saga majuice, mwingine dobi ni kupasi mtindo mmoja alafu wanataka tuchangiane umeme sawa, ilikua kimbembe, yule mama akanihamishia kwenye mita yake[emoji23][emoji23] mumewe hana la kusema yupo kama mdoli jioni nikirudi ni tungi tuu mimi na bimkubwa kibarazani, mumewe hanywi, siku ya siku mumewe kawahi kulala saa4 mapema sisi tunapombeka tu, kaja kushtuka saa 9 anatukuta hata akili hatuna mkewe hawezi kusimama na kajikojolea hafai[emoji28][emoji28][emoji1787][emoji1787] ulikua mziki, nikajichekecha mbio ndani nikamuacha wanaendelea na makelele na kukokotana. Utoto_ujana ni mtihani sana!Moyo ulikuwa unadunda hadi nikawa nahisi mtu akipita nje anaweza kuusikia. Nilikuwa natoka jasho balaa[emoji28][emoji28][emoji28]
Ukisoma story za kunyanduana mnara unasoma clear eeh? 😀Unganisha hapa hapa nime subscribe kabisa siku hizi naingia jf kwa kunusa ili ukiendelea niukute hapa
Haujala mzigo ?[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hawa wamama wenye nyumba haswa mishangazi kuna siku watatufanya vibaya, kuna mahala nilipanga zamani kidogo, mama mwenye nyumba alinipenda sana kiasi kwamba alikua anagombana na wapangaji wengine kwa sababu ndogo ndogo zilizokua zinanipa kero na akawaambia kabisa, atakae 7bbisha huyu kuhama atahama nae[emoji1787][emoji1787] mf, usafi alikua hataki kabisa kusikia nimehusishwa kwenye zamu za usafi na ishu ya umeme ilikua mtihani wapangaji kama sita mita moja inafikia mnanunua umeme wa mia5, usiku kucha mtu ana saga majuice, mwingine dobi ni kupasi mtindo mmoja alafu wanataka tuchangiane umeme sawa, ilikua kimbembe, yule mama akanihamishia kwenye mita yake[emoji23][emoji23] mumewe hana la kusema yupo kama mdoli jioni nikirudi ni tungi tuu mimi na bimkubwa kibarazani, mumewe hanywi, siku ya siku mumewe kawahi kulala saa4 mapema sisi tunapombeka tu, kaja kushtuka saa 9 anatukuta hata akili hatuna mkewe hawezi kusimama na kajikojolea hafai[emoji28][emoji28][emoji1787][emoji1787] ulikua mziki, nikajichekecha mbio ndani nikamuacha wanaendelea na makelele na kukokotana. Utoto_ujana ni mtihani sana!