Kuna jamaa alimfumania mkewe akiwa anatoa penzi enje ya ndoa, chakushangaza jamaa hakumsemesha mkewe wala nini,
Ila alivyowakuta aliingiza mkono mfukoni na kutoa sarafu ya shilingi 200 na kuirusha juu na kuidaka na kuiingiza mfukoni,
haikuishia hapo alikua anarusha ile hela kila akimuaga mkewe wakati akienda kazini na wakati akirudi nyumbani.
Mke alishindwa kumwelewa mumewe maana alikuwa maana ilikua ni mara mbili anairusha juu ile sarafu
kila wakati anatoa 200 yake na kuirusha juu na baada ya hapo huiingiza mfukoni.
Ilifika kipindi mpaka mke akawa anamwogopa mkewe yaani ikafikia hatua ambapo mke aliamua kuondoka na kumwacha mume mwenyew, huku akijiuliza kwanini mumewe anafanya kitendo kile.
Jamaa aliamua kumfuata mkewe nyumbani kwao na kumuomba warudi nyumbani ila alipofika hapo nyumbani hakusahau kuirudia ile style yake ya kurusha hela ndipo mke alipoendelea kukataa kuondoka na mumewe huku akiropoka aliyomfanyia mumewe. Ndipo wazazi walipoyajua yote.
Muda mchache baadae walirudiana na kuishi pamoja, huku mwanamke akiwa mtiifu na mwaminifu katika ndoa yake.
Hapo tunaona jinsi gani fumanizi lilivyoimarisha ndoa.
CC:
Mtambuzi, Speaker,
SnowBall,
snowhite,
Kaunga,
Mamndenyi,
gfsonwin,
Bujibuji,
asigwa.