Fumbo la hii ndoto ni lipi?

Fumbo la hii ndoto ni lipi?

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Sikumbuki ilianzaje ila tulikuwa kwenye gari kama zile za kutembeza watali na watu zaidi ya watatu akiwemo na mke wangu na mtoto

Tulikuwa tunasafiri tukafika kwenye mji una maghorofa mazuri sana lakini tulipofika tu kwenye jengo moja la ghorofa refu tukaona watu wanauwawa kwa kupigwa kwa risasi na mabomu,

Ikabidi tupitilize kukimbia na gari kwa kasi kujiokoa

Tulipofika mbele tulikutana na njia mbovu sana yaani ilikuwa ni matope na makorongo ikabidi tuendelee tu kusonga mbele tukiamini tutakutana na njia nzuri au mji. Huko mbele

Lakini kunawakati tulikutana na njia zuri kabisa au sehu ambayo inaonyesha Kuna nyayo za matairi ya magari tukifuatilia kidogo tu inapotea na kukuta kanjia chembamba mno yaani kiuju jala njia zilikuwa ni nyingi mno kiasi kwamba ukipotea huwezi kurudi nyuma

Basi baada ya kufika sehemu tukawa kama tumeshuka hivi kama kusukuma gari ipite sehemu ya matope ilikwama

Sasa ilipotoka na Mimi nikateremka, Ohoo!

Kurudi ikawa kimbembe yaani ile gari ikawa ni kama toi kiasi kwamba ikawa haiwezekani tena kurudi humo ndani nikaibeba na kuanza kutembea kwa miguu tu,

Lakini wakati tunaanza matatizo kwenye huo mji na kuanza kukimbia dereva alikuwa mwingine hivo Mimi nilipopewa niendeshe walikuwa wananielekeza namna ya kuingiza gia na Kuna sehem ilikuwa inanasa kwenye matope na wakanielekeza nikanyage tu mafuta na kweli ilikuwa inatoka yaani hiyo ardhi ilikuwa ni kama mbuga halafu imeloana na mvua

Nawasilisha
 
Kuna suala la control ya familia yako na ndoa yako pia. Fanya kitu au waweza kushangaa yatakayotokea na inaweza kuwa too late. Usipuuze ushauri wa watu juu ya hili.
 
  • Thanks
Reactions: LA7
Back
Top Bottom