SoC02 Fumbo lililomshinda Abighaeli

SoC02 Fumbo lililomshinda Abighaeli

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 30, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Kuipitia hadithi hii n wazi kuwa jamii itabadilika na kutupilia mbali Imani zinazogubikwa na wimbi la udanganyifu.

Basi, binti mkurugenzi alikuwa na rafiki Yake aitwae Sikujua ambae alikuwa ni binti aliezitamani sana bahati za Abighael kufuatiliwa na wakaka wengi ili aitumie fursa ile. Kwa kweli Sikujua alikuwa ni mdada ambae hajapata bahati ya kutongozwa na mkaka yeyote mtaani tangu avunje ungo hali iliyokuwa inamfanya afikirie Zaidi nini sababu au tatizo la kuwa mweusi kama mkaa? Au pengne aliwaza kwa sababu ya kutokuwa na umbo lisilo na namba zinazotajwa na wanaume wengi, kwa sababu umbo la Sikujua hali kuwa namba sita, nane na wala hali kuwa namba tisa waliopata elimu ya kizungu waliliita umbo la Sikujua kuwa ni SHAPELESS.

sikumoja, Sikujua alimtembelea bibi yake kijijini.Alikaa kwa siku tatu,na akawa amepata habari za mganga mmoja alieaminiwa kuwa alitibumatatizo yakindoa,kukosa uzazi na kutokupata mpenzi kwa msichana na mvulana. Kitendo cha taarifa hizi kubisha hodi na kuingia kwenye masikio ya Sikujua, ikambidi aghaili safari yake ya kurudi mjini kwa siku iliyo fuata na badala yake nikuenda na kumtafta mganga Yule aliye julikana kwa jina la Ling’anyi.

Ilipofika mchana mida ya saa nane Sikujua alianza safari kuelekea Kwa Linganyi, mzee Linganyi alikuwa na wanawake wengi mmoja wapo alikuwa anaitwa Kabula ambae anawatoto kumi lakini mmewe alikuwa na utitili wa watoto kutoka kwa wanawake wanje. Alipofika pale alishangazwa na idadi kubwa ya watoto kama watoto wa bata kwani kila mtoto aliku wana shughulizake, mara huyu anakunywa maji machafu,maraYule anakula kiazi,mara hawa wanafukuzana kwasababu ya mmoja kakataza sufuria la ukoko.

Mganga ling’anyi alikua mganga ambaye alikuwa anaogopeka sana na hata kuheshimika sana katika kijiji kile. Kwa kipindi kile, alikuwa na wanawake watatu na wote walikuwa wasichana makamo ya mjukuu wake wakwanza, kwani ilikuwa ni kawaida yake kuoa na mara baada ya mke kumuona amechakaa alitumia uganga wake kumwambia kuwa mizimu inamtaka aoe mwanamke mwingne, mzee ling’anyi alikuwa akitaka mdada yeyote Yule anae mtaka katika jamii ile na kudai kuwa mizimu ina mtaka huyu dada ndipo dada hakupaswa kuwa na kauli ya kukataa kuolewa na mganga Yule.

Niukweli kuwa Sikujua alikuwa na tamaa ya kutongozwa ndiyomaana hakusita kumtembelea mganga mara baada ya kusikia taarifa za mganga Yule.

“Karibu malkia wadunia”, mganga alimkaribisha Sikujua kwenye kibanda cha uganga.
“Asante babu” huku akivua viatu vyake iliapande shuka jekundu lililokuwa limetandikwa mbele ya miguu ya mganga ambae muda wote ambao Sikujua anavua na kuanza kupanda juu ya shuka lile, alikuwa ana mpepea kwa mkia wa mnyama wa ajabu na hisi ulikuwa mkia wa fisi au mbweha vile.

Baaada ya Sikujua kupanda na kukaa kitako juu ya shuka lile jekundu kama
damu, mganga alibadilika ghafla na kuanza kupiga makelele na lugha zisizo eleweka hadi Sikujua akaingiwa na wasiwasi sana.

“Malaika!!!!!” baada ya ukimya kidogo akamuita Sikujua huku ametoa macho yaliyo kuwa tayari yameiva,
“Abee,babu” hukuakiongozwa na woga uliomwingia

“Wewe ni msichana mzuri sana tena sana, wewe ni mzuri sijawahi ona, angalia uzuri wako humu” huku akimwelekeza kuangalia ndani ya chungu chenye maji yaliyo kuwa masafi bila hila yeyote, baada ya muda mfupi Sikujua alirudi kukaa kusikiliza tena.

“Nisikilize ewe binti, sikia”
“Nakusikiliza mzee wangu”
“kabla hujakanyaga udongo wakijiji hiki kuna njiwa alikuja akanipasha habari kuwa unakuja ndiyo maana umenikuta nmekusubiri kwa hamu yafisi mwenye njaa, hivyo nakukaribisha unijuze shida yako”

Mzee ling’anyi akasikiliza shida ya Sikujua na Sikujua alipopata huomuda hakutaka
kuongea mambo mengi sana ndipo alipo mweleza kuwa yeye hafuatwi na wakaka ingali rafiki yake Abighaeli anafuatwa sana kama nyama iliyo oza kwa Nzi.

“hahahahahahah,ririririririririri” mganga akapandisha nakuanza kupiga kelele zaidi huku akirudiarudia neno moja tu kuwa“umepona,,,umepona….umepona….umep…..” aliyasema maneno haya huku akiwa anazungushazungusha macho yake kichawi,.

Baaada yaukimya kidogo“ binti,ukiona mwanamke anafuatwa sana na wakaka ujue njia zake zipo wazi hazina doa lolote, lakini kwako nimeona njia zako zimefungwa yaani zimezibwa na laana ndogo ambayo nyanya zako watano waliiweka” akamezamate kisha akaendelea”ukieendelea hivi hautakuja kupata mwanaume wakukufuata”

Sikujua akastuka kidogo kisha akaendelea kusikiliza
“Kwahi……iyo…..Kwahiyo babu unanisaidiaje Mimi?” Sikujua alipatwa na wasiwasi zaidi. Babu akacheka kidogo na akamtoa wasiwasi kuwa amefika kwake na kwakuwa amefika mapema basi atapa utautatuzi. Ling’anyi akamuomba aende nyumbani naarudi usiku wa manane kwaajili ya kuelekea kwenye makutano yanjia iliwaweze kuitoa hiyo laana. Sikujua hakutaka kuogopa juu ya hilo bali aliangalia kutolewa kwahiyo iliyoitwa laana na mganga.

Siku ile alirudi kwa bibi yake jioni mida ya saa kumi jioni, Sikujua mapema alipika harakaharaka chakula na ilipofika saa moja usiku alianzakutenga wakala na akadai amechoka anataka apumzike, siku ile ilikuwa tofauti kwa Sikujua kwani tangu afike kwa bibi ake ilikuwa ni desturi yake kumwomba amsimulie hadithi. Kila mmoja aliingia chumbani kwake na huku Sikujua akiangalia muda na ilipofika saa tano usiku akatoka polepole ili asimwamshe bibi ake, Sikujua akaondoka kuelekea kwa mganga wake.

Muda ulipofika, mganga na Sikujua wakawa tayari kuondoka kuelekea palipo na makutano yanjia, kwakufuata maelekezo ya mganga kutoka kwa mizimu yake wakawa uchi wamnyama nakisha wakaelekea njia panda. Walipofika sehemu hiyo mganga akaanza kuimba nyimbo za kiganga na baada ya muda akamuamuru Sikujua alale ndipo alipo anza kugundua kuwa huenda mganga nae anataka kweli kufungu anjia. Sikujua hakuwa na aibu juu ya kufanya mapenzi na mzee Yule labda pengine kwasababu ilikuwa usiku na hakukua na mtu yeyote angelijua chochote. Kweli mzee ling’anyi akafanikiwa kulala na binti huyu kamailivyo kawaida yake kwa mabinti wengi wa kijiji kile.

**********
Nimwezi mmoja sasa umepita tangu Sikujua atoke Kwa mzee Ling’anyi na sasa aliku watayari amesharudi Jama kala mjini.Sikujua hakupata mabadiliko yoyote kuhusu kufuatwafuatwa na wanaume, madiliko pekee alililo hisi ni mimba kwasababu tangu arudi kutoka kijini kutapikatapika ilikuwa kawaida yake na mbaya zaidi tayari alikuwa hajaona siku yake. Hali hii ilimfanya ahisi maumivu makali Sana moyoni huku akikosa namnayakufanya.

Sikujua alikuwa nimsiri Sana kwani Licha ya kuwa na urafiki wakaribu na Abighaeli bado hakutaka kumueleza juu ya ujauzitio huenda pengine alihisi aibu kwasababu ya kwamba mwenye hiyo mimba alikuwa mzee makamo ya babuyake. Swala hili kwake lilionekana Kamamzigo mkubwa kwake, lakini angeliaibikaje Kama angelikubalimimba ikue na ajifungue mtoto wa mganga Ling’anyi?? Aliikataza nafsi yake na kujipa msimamo wa kuitoa kwanamna yeyote ile.

Usiku mmoja mida ya saa nne hivi, Sikujua alitoroka nyumbani na akaelekea sehemu moja iliyo julikana kwa jinala “PESAYAKOTU”. Sehemu hii ilijulikana Kwajina hili kwasababu kulikuwa na wanawake ambao hujiuza kwa wanaume yaani mwanaume anaweza kupata mwanamke kulingana na pesa yake na siyo vitu vingine.

Ujio wa Sikujua katika eneo hilo, uliwafanya wamshangae sana Sikujua kwasababu wanasema kuku mgeni hakosi kamba mguuni. Uvaaji wanguo ndefu na kubwa uliwafanya wamshangae na kumuona kuwa yeye ni kuku wa shamba kweli. Kwani wao walivaa nguo ambavyo kusemakweli vilikuwa vimefunika robo moja ya sehemu ya miili yao na mingine iliachwa wazi kama sehemu ya matangazo ya bidhaa ile.Sikujua hakutaka kuendelea kushangaa akaamua kufanya kilicho kuwa kimempeleka mahala pale.

Sikujua alimfuata mwanamke mmoja na kumuuomba kidonge cha kutolea mimba, mdada Yule hakushangaa bali aliomba pesa shilingi elfukumi, Sikujua alikuwa na elfu tano akadai ampunguzie, akapewa dawa na pia wakapeana namba za simu kwa mawasiliano zaidi. Alimeza na baada ya siku moja alihisi maumivu na maumivu yale yaliambatana na kutoka kwa hiyo mimba. Kitendo hiki kilimfanya Sikujua kukosa marafiki na wazazi kumdhihaki.

Sikujua aliishi maisha ya kujuta Sana juu ya kitendo ambacho amekifanya.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom