Fun Fact: Kamala Harris ndiye atayepokea matokeo ya uchaguzi kutoka kwa electors na kuyawasilisha bungeni yakathibitishwe

Fun Fact: Kamala Harris ndiye atayepokea matokeo ya uchaguzi kutoka kwa electors na kuyawasilisha bungeni yakathibitishwe

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Electors kutoka majimbo yote hupeleka matokeo yao kwa Rais wa bunge la Senate. Na Rais huyu ni Makamu wa Rais wa Marekani.

Kama mnakumbuka January 6, 2021. Waandamaji walikuwa wanapiga kelele anyongwe Mike Pence! Huyu alikuwa Makamu wa Rais wa Rais Donald Trump na alikataa kufanya figisu zozote zile katika kupokea matoko na kuyawasilisha bungeni ili kumsaidia Donald Trump ashinde urais.

Mwaka huu Kamala Harris ni mgombea na vilevile ni Rais wa Senate ambaye atapokea matokea kutoka kwa electors na kuyawasilisha bungeni ili yapitishwe.

Ishu kama hii imewahi tokea mwaka 1960 ambapo Makamu wa Rais na mgombea Urais dhidi ya John Kennedy alipokea matokea kutoka kwa electors na kuyawasilisha bungeni yapitishwe japokuwa alikuwa ameshindwa.

Baada ya sakata la Trump kutaka kuiba uchaguzi wamepitisha sheria zinazombana Rais wa Snate kwa kiasi fulani.

Demokrasia hii wote bado tunajitafuta.
 
Back
Top Bottom