Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,884
- 21,175
Ndege hawana meno ya kusagia chakula kama binadamu. Hivyo tumboni mwao wanafirigisi inayofanya kazi kama meno. Firigisi ina misuli yenye nguvu ambayo ikijikunjakunja, pamoja na mawe yaliyomo ndani yake, mawe yale husaga chakula kama vile mbegu ngumu. Kwa watu wa machimbo, firigisi ni kama kalasha.
Wanyama wengine wanaotumia njia inayofanana na hiyo kusaga chakula ni mamba. Mamba huwa hawatafuni chakula. Wanameza mapande mapande. Sasa ili kusaidia kusaga chakula huwa wanameza mawe ambayo hufanya kazi kama mawe ya kwenye firigisi.
Habari kutoka kitabu-Wanyama na ndege wa Afrika.