Fundamentals of Enlightenment (Kwa kiswahili)

Emc2

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
16,808
Reaction score
16,887
Utangulizi
Katika jambo ambalo nitaliongelea nitatumia lugha ya Kiswahili na kingereza kutokana na baadhi ya maneno ya kingereza kukosa tafsiri ya moja kwa moja ya Kiswahili.

Ninashukuru machapisho mbalimbali waliyotolewa na wataalamu tofauti tofatu na kunifanya mimi leo kuleta maelezo haya mbele yenu leo. Nimefanya research na kusoma vitabu tofauti tofatu na leo ninapenda niongelee “Fundamentals of Enlightenment”

Kwanza kabla kabisa ya kuendelea mbele ninaomba nieleze kidogo maana ya Enlightenment.

Enlightenment kwa lugha rahisi tunaweza kusema kuangaziwa, kujitambua na maelezo mengine yafananayo na hayo. Kwahiyo ninaweza nikachagua kutumia neon kujjitambua. Sitaki nieleweke kwamba ninaongelea swala la kujua jina lako, jinsi yako, baba yako nk; bali ninataka kuongelea kwamba wewe na mimi tuanze kujua sisi kwa uhalisia ni nini.

Katika maelezo yangu haya nitaongelea misingi ya kujitambua. Na katika maelezo yangu haya ninaomba watafiti wa maswala ya elimu, dini, siasa nk wanaweza kuyachukua na kuweza kuwasaidia katika kukidhi adhima yao. Maelezo yangu pia yanaweza kuwa na faida katika kujenga taifa lenye msingi wa utambuzi. Taifa linataka liwe imara na liwe na watu imara litajenga msingi mzuri wa utambuzi kwa watu wake.

Bila kupoteza muda, katika maelezo yangu haya (tunaweza kuiita Makala); nitaelezea mambo manne kuhusiana na msingi wa kujitambua:-

1. Intellect

2. Memory

3. Identity

4. Intelligence

Bila kupotenza muda ninaanza kama ifuatavyo:-

Intellect
Intellect ni uwezo wa kutumia kitu ambacho umekihifadhi kwenye kumbukumbu. Kwa wale wanaotumia kompyuta mnajua kuhusiana na database. Kwamba unatumia taarifa ambazo zimeingizwa kwenye database. Application inayochukua taarifa kutoka kwenye database tunaweza kuiita “Intellect”.

Application inaweza ikawa tofauti kutoka kwa mmoja na kwa mwingine. Na ule uharaka wa kuchukua taarifa kutoka kwenye database unaweza kutofautiana kutoka kwa mtu mmoja na mtu mwingine.

Database inawezakuwa na ukubwa sawa kati ya mmoja na mwingine. Lakini kwakuwa mmoja anaweza kuchota taarifa nyingi kwa muda mchache tunamwita “Intelligent” lakini kwa uhalisia sio, ni kwamba yeye yupo sharp kuchota taarifa kutoka kwenye database.

Mara zote intellect inachukua kumbukumbu ambazo zimehifadhiwa kwenye ubongo, lakini kiuhalisia kumbukumbu zilizopo kwenye ubongo ni kidogo sana kulinganisha na kumbukumbu zilizo kwenye mwili mzima.

Ubongo ni rahisi sana kufuta na kuweka taarifa tofauti tofauti. Ni sehemu ambayo wataalamu wa elimu wamekuwa wakiitumia na kukuta wakiwajaza wanafunzi taarifa ambazo zinaweza zikafutika kwa muda mfupi. Halafu wanafunzi wanakuwa wanapimwa uwezo wa kuchukua taarifa zilizohifadhiwa kwenye ubongo kwa muda Fulani.

Mwisho wa siku tunazalisha jamii inayokuwa na hofu, isiyojiamini. Jamii iliyojaza mambo mengi wakati mwingine hayatendewi kazi. Kitu kinachosababisha tunakuwa na jamii iliyojaa stress za maisha.

Wataalamu waelimu wameweka kipimo kikubwa cha kujua kuwa huyu ni Intelligent ni kumuuliza maswali. Mwisho wa siku tunazalisha jamii inayochukiana na mambo yafananayo na hayo.

Sisemi kwamba intellect haifai katika maisha yetu ya kila siku, lakini ninataka tujue kwamba ni sehemu ndogo tu katika safari ya utambuzi.

Ieleweke kwamba kwamba intellect haiwezi kupata kumbukumbu zingine kwenye sehemu ya mwili. Kwa mfano ndani ya cells zetu kuna kumbukumbu zilizohifadhiwa kwenye DNA, tunatembea nazo lakini hatuwezi kuzifikia kutokana tu hatujui namna gani ya kuweza kuzifikia. Ndani ya DNA kuna kumbukumbu ya miaka na miaka ya sura za babu zako wa zamani. Lakini kwakuwa sisi tunakuwa tumejikita sana kwenye intellect hatuwezi kutambua mambo hayo.

Kuna baadhi ya nchi motto kuanzia darasa la kwanza mpaka la nne wanakuwa hawafanyi mitihani. Hii wanasema kwamba elimu anayoipata akiwa katika umri ule ni kwaajili ya kujenga msingi. Kwahiyo mtoto anakuwa na uwezo mkubwa kiasi cha kuweza kufanya mambo makubwa.

Kutokana na mifumo yetu ya elimu inayojikita katika kupima intellect unakuta mtoto kuanzia akiwa mtoto mdogo amejengwa katika misingi ya kushindana, kuzomea, kuchukia nk. Watoto wanakuwa wanajengwa na wataalamu wa elimu huenda kwa kutokujua au kwa shinikizo fulani.

Pale anapokuwa mtu mzima anakuwa na tabia za kuongonzwa kwa mashinikizo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi au kidini. Mtu huyo anakuwa hana uwezo wake anakuwa amefumbwa sasa na kuongozwa na miundo aliyojengewa.
 
Memory
Sitaki katika eneo hili niweke tafsiri ya moja kwa moja kwamba memory ni kumbukumbu. Lakini ninaweza nikatumia neon kumbukumbu kwa kufikisha ujumbe tu.

Memory zipo sehemu yote ya mwili. Brain ni sehemu moja wapo ambapo memory ipo. Kiuhalisia kila cell katika mwili ipo na memory na intelligence. Ndani ya cell hakuna intellect kuna intelligence.

Tunaweza tukatoa mfano kwamba katika kila cell ndani yake kuna kitu kinaitwa DNA. Kwamba DNA imebeba kumbukumbu na taarifa nyingi sana. Zinafanya kazi kwenye miili yetu, zinakumbuka miaka mamilioni iliyopita lakini hatuna uwezo wa kujua taarifa zilizomo ndani kwa kuwa tu sisi tunajali sana kwenye ubongo.

Tunajali sana kwenye ubogo kwa sababu ni rahisi kuweka na kutoa taarifa kutokana kwamba ubongo umeunganika moja kwa moja na mifumo ya fahamu.

Hiki kitendo cha kujua kuna taarifa sehemu zote na mwili ni hatua muhimu sana ya kujitambua.

Lile wazo la kwamba brain ndiyo inatufanya tuwe kama tulivyo imetufanya tuishie pale tulipo na tusiweze kusonga mbele.

Inaweza kuwa watu wanaweza wakawa wanatumia memory za sehemu zingine za mwili kwa kubuni tu. Lakini kiuhalisia hawajui maana hakuna mwalimu wa kufundisha. Kila mmoja anakimbizana na stress za maisha, kufanikiwa kuliko mwingine, hofu ya kesho. Kwahiyo hakuna muda wowote wa kutulia.
 
Identity
Identity ni ile hali ya kujitofautisha wewe na watu wengine. Hii inauhusiano na intellect. Identity inaweza kutafsiri kuwa ni ego. Lakini Identity katika swala la kujitambua inaendea zaidi ya hapo.

Ego ni ile hali ya kujitambua wewe ni wewe au kujiona kuwa binafsi ni muhimu. Ego haiji kutokana na kufanya jambo fulani vizuri au vibaya. Huwa inatokea tangu ukiwa tumboni mwa mama. Kwa mara nyingine inakuwa kama defense mechanism.

Kwenye swala la identity linakuwa zaidi ya hapo kwamba inafikia hali ya kujiona kabila lako, Jinsia yako, Umbo lako nk. Kwa hiyo hayo mambo yanakufanya ujione wewe wa kipee kuliko wengine.

Kutokana na mambo haya ya Identity yanatenda kazi kwenye Intellect huwezi kufikiria zaidi ya hapo. Unakuwa kama umefungwa.

Intellect haiwezi ku-transcend jambo hili kutokana na hali yake.

Sitaki kusema kwamba Identity haifai lakini ninachotaka kueleza ni namna gani inaweza kutufanya tubaki kwenye intellect tu. Identity itatusaidia katika maisha yetu ya kila siku. Kufanikisha mipango yetu.

Mifumo yetu tangu tukiwa wadogo tunakuwa tunatambulishwa na kujiona namna gani sisi tulivyo wa pekee, yaani tofauti na wengine. Ipo mifano mingi tu. Wengine wanakuwa katika makundi, dini, siasa, jamii na kujiona wao kwa sehemu yao ni bora zaidi ya wengine.

Watu katika dini fulani wanaweza wakajitofautisha kutoka katika jamii either kutokana na mavazi, wanavyoongea nk. Jambo hili linatufanya tuishi maisha ya sehemu ndogo sana yetu.

Vilevile tunaweza kuongelea ile hali ya mmoja kupata matumizi ya kila siku kiasi cha kuitwa tajiri, mtu huyo anakuwa analipenda jina hilo. Kitendo hicho kinamfanya aiogope kesho kuhofia kuaibika. Kwa hiyo atafanya vyovyote awezavyo ili kuhakikisha kesho yake isiharibike. Huo ni uwezo ambao upo limited, upo ndani ya brain tu.
 
mkuu hapa hujakamilisha kutoa ufafanuzi zaidi ya namna yakutumia sehemu nyingine zinazohifadhi kumbukumbu kuimprovise
 
Mkuu Annael kama itawezekana jaribu kuunganisha pale juu itakuwa inaleta mtiririko mzuri zaidi kwa wasomaji
 
Congrats mkuu kwa nondo makini kama hz , kiukweli ww na mshana jr mnanifanya nione jf ni kisiwa sahihi cha maarifa na chakula cha ubongo wangu
 
Back
Top Bottom