Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,887
Utangulizi
Katika jambo ambalo nitaliongelea nitatumia lugha ya Kiswahili na kingereza kutokana na baadhi ya maneno ya kingereza kukosa tafsiri ya moja kwa moja ya Kiswahili.
Ninashukuru machapisho mbalimbali waliyotolewa na wataalamu tofauti tofatu na kunifanya mimi leo kuleta maelezo haya mbele yenu leo. Nimefanya research na kusoma vitabu tofauti tofatu na leo ninapenda niongelee “Fundamentals of Enlightenment”
Kwanza kabla kabisa ya kuendelea mbele ninaomba nieleze kidogo maana ya Enlightenment.
Enlightenment kwa lugha rahisi tunaweza kusema kuangaziwa, kujitambua na maelezo mengine yafananayo na hayo. Kwahiyo ninaweza nikachagua kutumia neon kujjitambua. Sitaki nieleweke kwamba ninaongelea swala la kujua jina lako, jinsi yako, baba yako nk; bali ninataka kuongelea kwamba wewe na mimi tuanze kujua sisi kwa uhalisia ni nini.
Katika maelezo yangu haya nitaongelea misingi ya kujitambua. Na katika maelezo yangu haya ninaomba watafiti wa maswala ya elimu, dini, siasa nk wanaweza kuyachukua na kuweza kuwasaidia katika kukidhi adhima yao. Maelezo yangu pia yanaweza kuwa na faida katika kujenga taifa lenye msingi wa utambuzi. Taifa linataka liwe imara na liwe na watu imara litajenga msingi mzuri wa utambuzi kwa watu wake.
Bila kupoteza muda, katika maelezo yangu haya (tunaweza kuiita Makala); nitaelezea mambo manne kuhusiana na msingi wa kujitambua:-
1. Intellect
2. Memory
3. Identity
4. Intelligence
Bila kupotenza muda ninaanza kama ifuatavyo:-
Intellect
Intellect ni uwezo wa kutumia kitu ambacho umekihifadhi kwenye kumbukumbu. Kwa wale wanaotumia kompyuta mnajua kuhusiana na database. Kwamba unatumia taarifa ambazo zimeingizwa kwenye database. Application inayochukua taarifa kutoka kwenye database tunaweza kuiita “Intellect”.
Application inaweza ikawa tofauti kutoka kwa mmoja na kwa mwingine. Na ule uharaka wa kuchukua taarifa kutoka kwenye database unaweza kutofautiana kutoka kwa mtu mmoja na mtu mwingine.
Database inawezakuwa na ukubwa sawa kati ya mmoja na mwingine. Lakini kwakuwa mmoja anaweza kuchota taarifa nyingi kwa muda mchache tunamwita “Intelligent” lakini kwa uhalisia sio, ni kwamba yeye yupo sharp kuchota taarifa kutoka kwenye database.
Mara zote intellect inachukua kumbukumbu ambazo zimehifadhiwa kwenye ubongo, lakini kiuhalisia kumbukumbu zilizopo kwenye ubongo ni kidogo sana kulinganisha na kumbukumbu zilizo kwenye mwili mzima.
Ubongo ni rahisi sana kufuta na kuweka taarifa tofauti tofauti. Ni sehemu ambayo wataalamu wa elimu wamekuwa wakiitumia na kukuta wakiwajaza wanafunzi taarifa ambazo zinaweza zikafutika kwa muda mfupi. Halafu wanafunzi wanakuwa wanapimwa uwezo wa kuchukua taarifa zilizohifadhiwa kwenye ubongo kwa muda Fulani.
Mwisho wa siku tunazalisha jamii inayokuwa na hofu, isiyojiamini. Jamii iliyojaza mambo mengi wakati mwingine hayatendewi kazi. Kitu kinachosababisha tunakuwa na jamii iliyojaa stress za maisha.
Wataalamu waelimu wameweka kipimo kikubwa cha kujua kuwa huyu ni Intelligent ni kumuuliza maswali. Mwisho wa siku tunazalisha jamii inayochukiana na mambo yafananayo na hayo.
Sisemi kwamba intellect haifai katika maisha yetu ya kila siku, lakini ninataka tujue kwamba ni sehemu ndogo tu katika safari ya utambuzi.
Ieleweke kwamba kwamba intellect haiwezi kupata kumbukumbu zingine kwenye sehemu ya mwili. Kwa mfano ndani ya cells zetu kuna kumbukumbu zilizohifadhiwa kwenye DNA, tunatembea nazo lakini hatuwezi kuzifikia kutokana tu hatujui namna gani ya kuweza kuzifikia. Ndani ya DNA kuna kumbukumbu ya miaka na miaka ya sura za babu zako wa zamani. Lakini kwakuwa sisi tunakuwa tumejikita sana kwenye intellect hatuwezi kutambua mambo hayo.
Kuna baadhi ya nchi motto kuanzia darasa la kwanza mpaka la nne wanakuwa hawafanyi mitihani. Hii wanasema kwamba elimu anayoipata akiwa katika umri ule ni kwaajili ya kujenga msingi. Kwahiyo mtoto anakuwa na uwezo mkubwa kiasi cha kuweza kufanya mambo makubwa.
Kutokana na mifumo yetu ya elimu inayojikita katika kupima intellect unakuta mtoto kuanzia akiwa mtoto mdogo amejengwa katika misingi ya kushindana, kuzomea, kuchukia nk. Watoto wanakuwa wanajengwa na wataalamu wa elimu huenda kwa kutokujua au kwa shinikizo fulani.
Pale anapokuwa mtu mzima anakuwa na tabia za kuongonzwa kwa mashinikizo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi au kidini. Mtu huyo anakuwa hana uwezo wake anakuwa amefumbwa sasa na kuongozwa na miundo aliyojengewa.