Fundi kapokonywa AC yangu na mdai wake

Fundi kapokonywa AC yangu na mdai wake

JMF

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
1,758
Reaction score
2,770
Salaam wana JF,
Naombeni mnifafanulie nijue kisheria limekaaje hii jambo.
AC ya ofisini ilikuwa imeharibika, jamaayangu akanipa namba za fundi mmoja ambae alidai ni mzuri na alishawahi kumtengenezea yake vizuri. Nikampigia akaja, akaicheki na kusema inabidi iende ofisini kwake akaitengenezee huko. Sikuwa na shaka nae ingawa sikuwa napajua ofisini kwake. Nilimwamini kupitia jamaayangu.
Baada ya siku mbili nikampigia kujua maendeleo, akasema kazi ni nyingi, ila kesho yake itakamilika. Kesho yake nikaelekezwa kwake nikaenda kujionea. Kufika nikamkuta kweli yupo kabanwa na wateja anakamilisha ya mmojawapo. Nikaondoka nije jioni. Jioni sikumkuta, nikaambiwa na vijana wake kuwa ametoka. Ili kufipisha mada, tokea siku hiyo hatujawahi kuonana na simu hapokei zaidi ya sms aliyonitumia kuwa alipatwa na matatizo kasafiri ghafla atarudi baada ya wiki. Ni mwezi sasa, ofisini wapo mafundi wenzake wanaendelea na kazi na wanadai jamaa huenda asirudi na AC yangu haipo pale sababu alikuwa anadaiwa ac mbili za watu(hawajui alizipeleka wapi) hivyo mdai wake alifika ofisini akamkuta na kumpokonya simu, baadhi ya vitendea kazi na ile ac yangu. Wanamfahamu huyo mdai.
Sasa wakuu fundi katokomea nisikopajua, nami ac yangu naitaka. Kisheria nasimama wapi? Au nichukue hatua gani?
 
Ngoja waje wataalam. Ila nionavyo Mimi, kama lisit za ununuzi unazo, utaipata A C yako. Maana huyo mdai mwingine anatakiwa kudeal na fundi wake, sio kuchukua Mali za wateja.
 
Nenda polisi ukafungue mashtaka kuhusu iyo ofisi. ikiwezekana washikilie mali zote za hiyo ofisi.
 
..mdai wake alifika ofisini akamkuta na kumpokonya simu, baadhi ya vitendea kazi na ile ac yangu. Wanamfahamu huyo mdai.
Sasa wakuu fundi katokomea nisikopajua, nami ac yangu naitaka. Kisheria nasimama wapi? Au nichukue hatua gani?
Anayekamatwa na ngozi/minofu ndo mwizi..
Peleleza AC yako ilipo, fungua RB, nenda na polisi chukua mzigo!
 
Back
Top Bottom