Fundi kupaua (mrejesho wa kazi)

Mamujay

Senior Member
Joined
Dec 24, 2022
Posts
149
Reaction score
345
Napatikana kwa namba 0743257669
TUMEKABIDHI KAZI PANDE ZA KIGOGO MABIBO NYUMBA INAUKUBWA WA MITA 4.6 KWA 12M
Mbao 4×2 pcs 80×5500= 440,000
Mbao 2×2 pcs 60× 2800= 168,000
Mbao 10×1 pcs 12×16000= 192,000/=
Misumari nch4 kg 25×3500= 87,500/=
Misumari nch3 kg 5×3500= 17,500/=
Misumari nch2 kg 3×3500= 10,500/=
Rangi ya kupaka fisher board 50,000 /=
Bati ALAFU pc 60
33,000 x 60= 1,980,0000 =
Kofia pcs 12× 14,000 =168,000
Valley HAKUNA
Misumari ya bati pkt 25×8000= 200,000/=
JUMLA KUU .3,313.5,000/=..........................
UFUNDI MAELEWANO
 
Hongera, bado ile seksheni ya kizungu aka finishingi....

Kila la kheri.

Oooh, kumbe wewe ndo fundi wa kupaua, nilijua unaleta mrejesho umepaua nyumba yako.

Hongera tena, kazi nzuri, washwahili/vijana wanasema kazi imenyooka.
 
-Bado usukaji wa waya za umeme.
-Bado mabomba ya maji.
-Bado jipsam/siling boards.
-Bado ripu.
-Bado milango.
-Bado madirisha.
-Bado tailiz.
-Bado rangi.
-Bado holda za taa, swichi, sockets, breaker.
-Bado kuunganisha umeme.
-Bado kuunganisha maji.
Hongera, lakini endelea kujipanga maana mwendo bado umechangamka.
 
Hongera sana mkuu unatutia moyo kwakweli
 
unaweza kukadiria raman ukajua itataka mbao ngap na bat ngap?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…