Fundi Mpemba Kumzibiti Mume mcharuko.

Timor

Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
48
Reaction score
32
Najua pahala hapa hapaharibiki neno nimeolewa yapata miaka kadhaa sasa nina watoto wanne,Mume wangu hatulii kabisa, Ni mcharuko kwa kwenda mbele hapishi skirt wala gauni.Mie bado nampenda ila nahofu ataniletea maradhi mabaya.Nimemsomesha na kumsomesha imeshindikana.Jana shoga yangu kaniambia kuna wataalam wa kipemba wanaweza kumfunga luku/speed governor.Kwa anayemjua mjuzi wa shughuli hiyo naomba ani PM tafadhali sana.
 
Kama shoga yako amekwambia kuna wataalamu wa kipemba kwanini unakuja tena hapa kuuliza kwanini usimuulize huyo shoga yako akakupeleka huko kwa huyo mpemba.
 
Kama shoga yako amekwambia kuna wataalamu wa kipemba kwanini unakuja tena hapa kuuliza kwanini usimuulize huyo shoga yako akakupeleka huko kwa huyo mpemba.

Yeye ana simulizi tu hajui fundi huko. Naomba msaada pls
 
Una hatari weye....sa aki'over dose' badala ya kuwa 'speed governor' ndo ikawa 'engine blocker' kabisa utaweza kuishi naye bila ile shughuli? Tafuta njia nyingine bana usimfunge mwenzio na hizo mambo!
 
Yeye ana simulizi tu hajui fundi huko. Naomba msaada pls
Kabla haujaenda kwa huyo mpemba, Je? una uhakika kuwa huyo mpemba atamdhibiti mumeo maana isije ikawa wewe ndio ukaishia kwa mpemba.

ANGALIZO: Mungu ndio kimbilio letu sote tunapokuwa kwenye matatizo cha msingi nachokushauri, muombe Mungu na umueleze matatizo uliyonayo tusipende kuwa na shallow mind ya kufikiria fulani atamdhibiti fulani asitoke nje ya ndoa katika matatizo yanayotukabili hasa ya ndoa.
 
Mpemba ni mwanadamu!!
Hatuwezi kumtegemea Mpemba na wanadamu wengine kwenye matatizo yetu.

Muombee Mume wako, ajitambue!!!
Akiwa na hofu ya Mungu atafanikiwa kushinda vishawishi.

Ila bwana wanaume mi nahisi na nakaribia kukubali kwamba hawawezi kuishi na mwanamke mmoja.
Manake dah........
 
Acha hilo wazo kabisaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!! Mpemba? Utalia maisha yako yote, maana mumeo atakuja kuwa zezeta tu, hata kazi hatafanya tena, sana sana huyo Mpemba ndie atakuwa anaku-do!!!
 
Jamani yamenisibu haya,Ni kweli kimbilio ltu ni kwa BWANA, Lakini kwa huyu mwenzangu hapo ni pagumu etii.
 
Jamani yamenisibu haya,Ni kweli kimbilio ltu ni kwa BWANA, Lakini kwa huyu mwenzangu hapo ni pagumu etii.
Sasa wewe kimbilio lako ni MPEMBA kwanini umuamini mpemba kuwa atakusaidia kwenye tatizo lako??
 
Pamoja na yote uliyoambiwa, waogope sana hao mafundi kwani jambo la kwanza atakalofanya ni kukubanjua. Ikiwa mume wako ni kicheche bora la kufanya ni kujifunga luku wewe ili kuepuka maradhi. Mwambie ama anawacha au haonji kitu.
 
Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu......achana kabisa na hao wapemba na huyo shoga ako naona hakutakii mema,yeye alishapeleka wa kwake kwa mpemba au ndo anataka mumeo akafanyiwe majaribio???? muombe Mungu sana,hapa tunashuhuda za watu waliopita unakopita,wakaumia sana lakini wakazidi kumuomba Mungu na Mungu kwa rehema zake ameweza kuwajibu.mtegemee Mungu,anawaheshimu wanaomtumaini.Sijui kwa kiasi gani waweza vumilia au kuishi bila huyo mwanaume....ila jiweke wewe kwanza,mwenzio nina mashaka amezidiwa tamaa haoni kuna magonjwa au pengine anajikinga....kama unaweza zungumza nae kuwa sasa unahofia maisha yako,kama hawezi muache au kata kufanya nae tendo la ndoa.....he utakuja waacha wanao wanne hapa,bora afe yeye wewe ubaki!:juggle:
 
Sio kila kitu unachoambiwa na shoga yako unaona sawa
hilo la kwenda kwa MPEMBA wala sio suluhisho la matatizo
huyo mpemba unayemtaka atakuharibia kabisa ukajuta bora angeendelea kuwa hivyo alivyo.
tafuta chanzo kwa nini mumeo ameanzisha hiyo tabia je ni wewe ndio chanzo cha mabadiliko hayo?
kama ndio tabia yake endelea kumlilia Mungu ipo siku atambadilisha usitake
mabadiliko haraka Mungu atakujalia wakati ukifika

 
Jamani yamenisibu haya,Ni kweli kimbilio ltu ni kwa BWANA, Lakini kwa huyu mwenzangu hapo ni pagumu etii.

Ukikutana na huyo fundi atakuuliza 'Unataka nimdhibiti aweje?' Kwa taarifa yako nikuwa atamfanya mjinga mjinga, au atamuondolea nguvu za kiume. kwa vyovyote vile chochote atakachomfanyia kitakuathiri na wewe.
Rizika tu na jinsi alivyo, usitafute makuu mama yangu... plz.
 
Acha ushirikina wewe mchawi we mwenyewe hapo ulipo umejiuliza nini tatizo la mumeo??? Jichunguze wewe kwanza halafu uone unakosea wapi pengine humtimizii mumeo ndo maana anakuwa mcharuko unahakika unamtendea kila lililo jema wewe???

Acha mambo ya waganga kabisa hakuna zaidi ya maombi
 

Dena we mkali! Sipati picha ukiwa mwalimu wa primary...
 
Mbona wote mnadhani huyo mpemba ni mwanaume? Kwani hawezi kuwa mwanamke?? Shoga yake si kamwambia, "kuna wataalamu wa KIPEMBA!" Eti Timor!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…