Fundi mzuri wa Mark X napata wapi?

Job sanga

Member
Joined
Apr 3, 2019
Posts
61
Reaction score
74
Nna gari aina mark x inasumbua sana tatizo la starter na power steering. Hasa starter. Jinsi lilivyo ukiliwasha Majira ya asubuhi litawaka vzuri ukitembea kuanzia kilometer 40 kuendelea au ukikaa barabarani kwa muda kupata lisaa 1 af ukaja ukizima halitawaki tena muda huo hio mpaka usubiri saa lingine uje tena ukipiga starter ndio litawaka.

Nimeshashirikisha mafundi katika garage tatu naona wote wameshindwa. Kwa yeyote ambae ashawahi pata hili tatizo kalimaliza tafadhali share fundi wako au ujuzi cha kufanya.
 
Tatizo dogo sana mkuu nenda kwa fundi umeme wa magari nenda na jibu moja tu mwanbie fundi Armicher/ amicha ya stater ya gari yako imekufa sasa utaamua ww mwenyewe kufunga mpya au kununua starter mpya shida ni huyo tu mkuu means amicha ikipata moto injini lile joto linafanya itanuke pia badili na starter brush. Utakuja nishukuru kwa mrejesho
 
Fundi wa IST ndo huyo huyo wa Mark X
 
Mmoja kati ya mafundi ashabadilisha starter complete mbili. Ila tatzo linarudi tena
 
Issue ya power steering ni common sana kwenye hizi gari. Je inakuwashia taa ya P/S kwenye dashboard? Na taa ya check engine inawaka au vp?

Kama upo dar nitumie namba zako PM nikutafute turekebishe hio shida ila kama upo mikoani tafuta fundi mzuri wa umeme magari na diagnosis, ukihangaika na fundi mechanics hautotatuliwa hilo tatizo.
 
Umejaribu kutumia computer majibu yakawqje?

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…