Fundisho gani umechelewa kulijua maishani ila ulimwengu ukakufunza? Mimi ipo hivi, wewe je?

Fundisho gani umechelewa kulijua maishani ila ulimwengu ukakufunza? Mimi ipo hivi, wewe je?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,406
Reaction score
19,375
Huna haja ya kupoteza muda wako kwa mtu anaekuchukulia kama kituko.

Ukiniona kituko nakusahau kama utani.

Nakumbuka zamani kuna baadhi ya watu baadhi yao niliwaganda sana ila wao hawana time na mimi. Nilijikuta napoteza muda, pesa na hata kuziadhibu hisia zangu kwa kuruhusu kunyanyaswa.

Nlijifunza hiki kitu kwa maumivu mkali sana nilipokuwa nafanya mengi kusongesha urafiki na watu ambao hawana muda na mimi na pia nilijifunza kwa machozi kabisa pale binti fulani nilipomuhangaikia sana kumbe akili yake ipo kwengine kabisa.

Maisha yangu ya sasa nafata hii kanuni nyepesi sana inayotanguliza akili kufanya maamuzi sahihi kuliko kutumia hisia za moyo zinazoweza kunikwaza mbeleni.
 
Nilikua tayari kubeba mateso ya wenzangu (shuleni) nikijua ndio watu inavyotskiwa waishi. Kinyume chake nilichekwa na kuonekana fala nikawa dustbin yao. Ili utoboe maishani usiwe mwema kabisa, mpaka ukitoboa huko ndio uanze wema.

Peoples ain't give a fuc.k
 
Maisha hayako sawa kabisa. Dunia inayoonekana kwa macho siyo halisi na kinachotendeka nyuma ya pazia jikute mama au baba huruma uchekwe. Kila mtu yupo mahali fulani kwa maslahi yake fuata yako achana na ya wenzako.

Kila sekunde ni muhimu kwako kuwaza na kutenda positive ikipita hairudi hiyoo. Spend your time wise.
 
Post Chache Nilizozisoma Ni Kuwa Waliokomenti Kila Mtu Anajuta WEMA ALIOUFANYA,WAPENZI ALIOPITIA,MUDA ALIOUTOA na yafananayo Hayo....

Nadhani Ima Kuna Makosa Wazazi Wanatukuza Kitofauti Ama Mila Zetu Ama Dini(Imani)zetu Hatuzielewi Ama Tunazitafsiri Tofauti na Uhalisia....

Dunia Imeumbwa VYEMA TU Wala haina Makosa.....
Kuwepo Vipindi Vya Hali Ya Hewa Tofauti kunatufundisha kuwa na MIZANI katika KILA TULIFANYALO....

MIZANI ya Mambo ikikosekana KUFUNDISHWA VYEMA UTOTONI Basi huwa Ni MAJUTO kipindi cha UJANA ama hata UZEENI(desperation).

Ndio Mana Tunakutana na watu wana WAJIHI MZURI,ELIMU KUBWA NA BORA,VYEO NA NYADHIFA,FEDHA ZA KUMWAGA lakini Hawana furaha ya UKWELI....

Ukikaa nao chini na wakakueleza kwanini WANA HALI HIYO...utashangaa.......
1.Wako Wasioishi Maisha Asilia
2.Hupelekeshwa na Wapendwa Wao
3.Tamaa ya VItu Iliyopitiliza
4.Kupenda kufurahisha wengine bila MIZANI Wala NIDHAMU
5.Burudani na starehe zao Kukamilishwa na watu wengine.
6.Kutojiamini KIUKWELI na kutoacha PRETENCE
7.Kupenda Ukubwa Na "kuabudiwa".

Relaaaaaaaax.....

Maisha Ni Safari....
Jiamini Ulivyo ilimradi Huvunji Sheria za Nchi,ilimradi Unachunga Mipaka Na Uhuru Wako Na Kutoingilia Mipaka na Uhuru Wa Wengine.

#LifeIsJustADream
 
Uko vzr ndg....
emoji122.png
emoji122.png
emoji122.png
emoji106.png
 
Ndugu zangu wa baba mmoja mkiona sipokei Simu zenu au tukikutana mkiona tukikutana mahali nimejitenga sina time na nyie kama nakosea mnisamehe lakini kwangu neno kuu na msimamo ni palepale kwamba"HAPANA NDIO BASI TENA"
 
Ndugu zangu wa baba mmoja mkiona sipokei Simu zenu au tukikutana mkiona tukikutana mahali nimejitenga sina time na nyie kama nakosea mnisamehe lakini kwangu neno kuu na msimamo ni palepale kwamba"HAPANA NDIO BASI TENA"
Duuh Hatareee😁😁
 
Siku nikiwa na pesa basi ndo itakuwa furaha yangu na sio kingine. Twende mbele turudi nyuma pesa ndo kilakitu. Hata mtu akikuboa ukampa time yako lakini yeye akapuuza, kama unapesa utamuona takataka tu. Tutafute pesa hayo mambo mengine yatajiseti tu.

Enewei toa connection ya kupata pesa hapa.
 
Ndugu zangu wa baba mmoja mkiona sipokei Simu zenu au tukikutana mkiona tukikutana mahali nimejitenga sina time na nyie kama nakosea mnisamehe lakini kwangu neno kuu na msimamo ni palepale kwamba"HAPANA NDIO BASI TENA"
Nimekuelewa sana mkuu
 
When I scream: Nobody realized
When I cry: No body care
When I scream for help: Nobody comes
When I'm in danger: Nobody helps
But when I make mistakes: Everyone judges me.
It's called life.Kutoka YouTube.
 
Jamani eh,fanyeni wema si muonwe machoni pa watu na wala msiwe wenye kutegemea malipo kutoka kwao wawaonao au waupokeao msaada huo.

Fanyeni ili mpate furaha na amani ya kweli mioyoni mwenu,naye Mungu asiye mnafiki aonaye dhamira yenu atakuwa rafiki yenu asiye kigeu geu.

Mkorinto 5:2 JF(HHM).
 
Back
Top Bottom