Fungu la 10 ni kitu ambacho hakipo kwa sasa kwa mujibu wa biblia na ni kujiumiza bila sababu kuendelea kutoa

Fungu la 10 ni kitu ambacho hakipo kwa sasa kwa mujibu wa biblia na ni kujiumiza bila sababu kuendelea kutoa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Kwa sasa kumekuwa na msisitizo mkubwa mno makanisani watu kutoa pesa inayotajwa kama fungu la 10 (zaka) kiasi kwamba imegeuka kero kubwa kwenye jamii. Wanawake wamekuwa wahanga wa kuchotwa akili zao na kujikuta wanatoa hadi pesa za kujikimu na kuingiza familia kwenye matatizo yasiyo ya lazima. Sasa mimi leo natamka hadharani kuwa ACHA KUTOA FUNGU LA 10 KWA SABABU NI UTAPELI. Soma huu uzi bila hisia ili uelewe.

Kwanza ni lazima tujue historia fupi kuhusu fungu la 10 ni kwanini na wapi lilikuwa linatolewa? Historia inaonyesha Fungu la 10 lilikuwepo zamani enzi za Abrahamu ila likawa sheria kamili enzi za Musa. Abrahamu alitoa fungu la 10 kama zawadi kwa Mfalme na kuhani wa Salemu. Soma Mwanzo 14:18-20 ingawa haitajwi tena kama Abrahamu alishawahi toa tena fungu la 10. Pia Yakobo alitoa ahadi kwa Mungu kuwa atatoa fungu la 10 endapo Mungu angembariki. Mwanzo 28:20-22

Enzi za Musa ndo kukawepo na sheria kuwa kutoa fungu la 10 ni lazima. "Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka". Kumbukumbu la torati 14:22

Tukirudi nyuma kidogo tutaona waisrael wakiwa jangwani walikuwa wakiabudu kwenye kilichoitwa HEMA YA KUKUTANIA. Na kwa wakati huo Mungu alimteua Haruni kuwa kuhani mkuu huku wana wa Lawi wakiwa wafanyakazi kwenye hema la kukutania. Katika hao wana wa Lawi kulikuwa na wafanyakazi wasio makuhani na wale makuhani. Haruni na walawi hawakupaswa kufanya kazi nyingine yoyote zaidi ya zinazohusu dini yao. Walikuwa wanafanya kazi kanisani. Kutokana na hilo ndo ikabidi uwepo utaratibu ili na wao waishi bila shida.

Basi ndo sheria ikawepo ya wana wa Israel kutoa fungu la 10 kwenye mavuno yao na mifugo kuwapatia walawi waliokuwa wanafanya kazi za kiroho. Na walawi wakishapokea hizo zaka na sadaka basi kwa wale walawi wasio makuhani hutoa fungu la 10 ya vile walivyopokea na kuwapatia makuhani. Soma Hesabu 18. Pia fungu la 10 lilikuwa likitolewa kwa wale maskini wasio na uwezo kila baada ya miaka mitatu (Kumbukumbu la torati 14:28-29). Kimsingi hakuna zaka wala sadaka ambayo huenda kwa Mungu moja kwa moja. Mungu aliweka tu utaratibu ili wale waliokuwa wanafanya kazi za kiroho nao waishi. Ila Mungu hajawahi kuwa na dhiki ya kutaka tumpe hela.

Tukisoma Wakolosai 2:13-14 tunaona kuwa mara baada ya kifo cha Yesu hizi sheria za Musa hazikuendelea kutumika tena. Na pia ikasisitizwa mtu asije kukuhukumu kupitia sheria za Musa. Wakolosai 2:16 "Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;"

Sasa kama Zaka na sadaka sio lazima, nini kinatakiwa kutolewa kanisani? Jibu lipo kwenye 2 Wakorintho 9:6-12. Biblia imemtaka kila muumini atoe tu mchango wa fedha kanisani kwa ajili ya kuwezesha huduma ila sio lazima. 2 Wakorintho 9:7 "Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu". Na pia biblia haijataja kuwa ni dhambi kutokutoa. Mungu anataka utoe kwa moyo wako na sio kujilazimisha.

Kutoa fedha kanisani ni jambo lenye baraka nyingi ili kuwezesha huduma. Hiyo ni ahadi ya Mungu kupitia Malaki 3:10 "Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la". Lakini pia Mungu ametutaka tunapotoa iwe siri. Mathayo 6:3-4 "Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi".

Kwenye suala zima la utoaji mara baada ya kifo cha Yesu tumehimizwa zaidi kusaidia maskini na mtu mwingine yeyote mwenye uhitaji. Hakuna sehemu imetajwa fungu la 10. Hili suala la fungu la 10 linatumika na wachungaji matapeli kuvuna pesa bila jasho kutoka kwa waumini wajinga. Biblia imesisitiza mara nyingi sana kusaidia wasiojiweza. Hata fungu la 10 la enzi za Musa lilikuwa kuwasaidia walawi ambao hawakuwa na kazi nyingine zaidi ya ile ya kiroho. Hawa wachungaji wanaomiliki biashara mjini hakuna haja ya kuwachangia chochote. Soma zaidi mafungu yafuatayo ujue zaidi kuhusu utoaji. Mathayo 10:8, Mithali 3:27, Luka 6:38, Yakobo 2:15-17, Mithali 11:24-25, Kumbukumbu la torati 15:11, Mithali 3:9 - 10, Mathayo 25:40
 
Wayahudi ni mabingwa wa kila kitu duniani still wanatoa zaidi ya hio asilimia kumi na wanafanikiwa.
Kwa shetani wanatoa 60% na sio 10% kama kwa MUNGU ndo maana wana wa shetani wanafanikiwa sana.
 
Ukimalizana na fungu la 10 uje uangazie kidogo hii sadaka ya kujimaliza. Imo kwenye maandiko kweli? 🖐🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️
Sadaka ya kujimaliza haipo kimaandiko bali ni wizi wa hawa waganga wa kienyeji waliofungua makanisa.
Utoi sadaka ili uumie bali ili nia yako Mungu haione.Mungu ni tajiri haitaji sadaka yako bali kilichomo moyoni mwako.
 
Back
Top Bottom