MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
Wewe toa tu hakuna unachopoteza, acha ligi, unapishana na baraka bila sababu yoyote
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu hebu jazia nyama kidogo na sisi tujifunze.Zipo silaha kubwa zaidi ya Saba za kumshinda shetani sadaka ni moja ya silaha hizo.
Hii mbona ipo kama rushwa tu?Zipo silaha kubwa zaidi ya Saba za kumshinda shetani sadaka ni moja ya silaha hizo.
Nyama za nini mkuu wewe toa kama unatoa tu😁Mkuu hebu jazia nyama kidogo na sisi tujifunze.
Rushwa ni chukizoHii mbona ipo kama rushwa tu?
Hata sasa wanatoa zaidi ya hio tafuta kanuni ya mafanikio za kiyahudi utaonaIla sio kulazimishana 10% ya kipato chako. Hata hao waisrael walikuwa wanatoa kwa mwaka mara moja.
Hakuna silaha ya kumshinda shetani zaidi ya kufuata amri 10 za Mungu. Na katika hizo amri hakuna inayosema tutoe fungu la 10. Kuacha dhambi ndo namna pekee ya kumshinda shetani na sio janjajanja zingine. Kwenye hizo janjajanja shetani yuko mbele sana ya muda. Wakati wewe unampiga na silaha ya fungu la 10 yeye anakusogezea demu mwenye tako la dunia nzima ili unase..Zipo silaha kubwa zaidi ya Saba za kumshinda shetani sadaka ni moja ya silaha hizo.
Amri 10 zipo ndani ya silaha hizo,kushobokea tako means wewe bado mchanga kirohoHakuna silaha ya kumshinda shetani zaidi ya kufuata amri 10 za Mungu. Na katika hizo amri hakuna inayosema tutoe fungu la 10. Kuacha dhambi ndo namna pekee ya kumshinda shetani na sio janjajanja zingine. Kwenye hizo janjajanja shetani yuko mbele sana ya muda. Wakati wewe unampiga na silaha ya fungu la 10 yeye anakusogezea demu mwenye tako la dunia nzima ili unase..
Mama mdogo wangu alifariki mwaka jana, ukoo mzima tulikuwa na huzuni lakini baba mdogo alisema hivi "afadhali mke wangu amekufa, hapa sasa nitaishi kwa amani na wanangu" aise tulishangaa sana! Baada ya kumuuliza alituambia kuwa zaidi ya 200M za kwenye biashara zake KKOO ziliishia kanisani kwa mke wake! Alikuwa anashinda kwenye makanisa ya kiroho muda mwingi, na kila asubuhi anabeba kitita anasema ni sadaka! Hii ilimchosha baba mdogo kiasi kwamba alifurahia kifo cha mkewe!Ni kweli ila nimeandika makusudi kusaidia wapumbavu wanaoteswa na hawa wachungaji matapeli. Kuna ndoa zinapitia wakati mgumu sababu ikiwa manabii na wachungaji feki wanaowakomba hela zao.
Baba mdogo aliteseka sana itakuwa. Watumishi ni washenzi.Mama mdogo wangu alifariki mwaka jana, ukoo mzima tulikuwa na huzuni lakini baba mdogo alisema hivi "afadhali mke wangu amekufa, hapa sasa nitaishi kwa amani na wanangu" aise tulishangaa sana! Baada ya kumuuliza alituambia kuwa zaidi ya 200M za kwenye biashara zake KKOO ziliishia kanisani kwa mke wake! Alikuwa anashinda kwenye makanisa ya kiroho muda mwingi, na kila asubuhi anabeba kitita anasema ni sadaka! Hii ilimchosha baba mdogo kiasi kwamba alifurahia kifo cha mkewe!
Kwahiyo OP ulichoeleza nakubaliana na wewe kabisa, ni vyema tutoe sadaka kawaida ila sio zile sadaka za KUPANGIWA na watumishi.
Kuna binamu yangu wa kike aliniambia ili nifanikiwe natakiwa nitoe sadaka ile inayouma.Sadaka ni janga kwa wanawake kama unamke mlokole pole sana.......
Sana! Kwakweli tunahitaji neema ya Mungu kwenye hili, maana baadhi ya makanisa wanatambulisha sadaka mpya kila kukicha.Baba mdogo aliteseka sana itakuwa. Watumishi ni washenzi.
Mkristo halazimishwi kutoa fungu la kumi kwa sababu hayuko chini ya sheria bali katika neema ya Yesu Kristo.Kwa sasa kumekuwa na msisitizo mkubwa mno makanisani watu kutoa pesa inayotajwa kama fungu la 10 (zaka) kiasi kwamba imegeuka kero kubwa kwenye jamii. Wanawake wamekuwa wahanga wa kuchotwa akili zao na kujikuta wanatoa hadi pesa za kujikimu na kuingiza familia kwenye matatizo yasiyo ya lazima. Sasa mimi leo natamka hadharani kuwa ACHA KUTOA FUNGU LA 10 KWA SABABU NI UTAPELI. Soma huu uzi bila hisia ili uelewe.
Kwanza ni lazima tujue historia fupi kuhusu fungu la 10 ni kwanini na wapi lilikuwa linatolewa? Historia inaonyesha Fungu la 10 lilikuwepo zamani enzi za Abrahamu ila likawa sheria kamili enzi za Musa. Abrahamu alitoa fungu la 10 kama zawadi kwa Mfalme na kuhani wa Salemu. Soma Mwanzo 14:18-20 ingawa haitajwi tena kama Abrahamu alishawahi toa tena fungu la 10. Pia Yakobo alitoa ahadi kwa Mungu kuwa atatoa fungu la 10 endapo Mungu angembariki. Mwanzo 28:20-22
Enzi za Musa ndo kukawepo na sheria kuwa kutoa fungu la 10 ni lazima. "Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka". Kumbukumbu la torati 14:22
Tukirudi nyuma kidogo tutaona waisrael wakiwa jangwani walikuwa wakiabudu kwenye kilichoitwa HEMA YA KUKUTANIA. Na kwa wakati huo Mungu alimteua Haruni kuwa kuhani mkuu huku wana wa Lawi wakiwa wafanyakazi kwenye hema la kukutania. Katika hao wana wa Lawi kulikuwa na wafanyakazi wasio makuhani na wale makuhani. Haruni na walawi hawakupaswa kufanya kazi nyingine yoyote zaidi ya zinazohusu dini yao. Walikuwa wanafanya kazi kanisani. Kutokana na hilo ndo ikabidi uwepo utaratibu ili na wao waishi bila shida.
Basi ndo sheria ikawepo ya wana wa Israel kutoa fungu la 10 kwenye mavuno yao na mifugo kuwapatia walawi waliokuwa wanafanya kazi za kiroho. Na walawi wakishapokea hizo zaka na sadaka basi kwa wale walawi wasio makuhani hutoa fungu la 10 ya vile walivyopokea na kuwapatia makuhani. Soma Hesabu 18. Pia fungu la 10 lilikuwa likitolewa kwa wale maskini wasio na uwezo kila baada ya miaka mitatu (Kumbukumbu la torati 14:28-29). Kimsingi hakuna zaka wala sadaka ambayo huenda kwa Mungu moja kwa moja. Mungu aliweka tu utaratibu ili wale waliokuwa wanafanya kazi za kiroho nao waishi. Ila Mungu hajawahi kuwa na dhiki ya kutaka tumpe hela.
Tukisoma Wakolosai 2:13-14 tunaona kuwa mara baada ya kifo cha Yesu hizi sheria za Musa hazikuendelea kutumika tena. Na pia ikasisitizwa mtu asije kukuhukumu kupitia sheria za Musa. Wakolosai 2:16 "Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;"
Sasa kama Zaka na sadaka sio lazima, nini kinatakiwa kutolewa kanisani? Jibu lipo kwenye 2 Wakorintho 9:6-12. Biblia imemtaka kila muumini atoe tu mchango wa fedha kanisani kwa ajili ya kuwezesha huduma ila sio lazima. 2 Wakorintho 9:7 "Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu". Na pia biblia haijataja kuwa ni dhambi kutokutoa. Mungu anataka utoe kwa moyo wako na sio kujilazimisha.
Kutoa fedha kanisani ni jambo lenye baraka nyingi ili kuwezesha huduma. Hiyo ni ahadi ya Mungu kupitia Malaki 3:10 "Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la". Lakini pia Mungu ametutaka tunapotoa iwe siri. Mathayo 6:3-4 "Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi".
Kwenye suala zima la utoaji mara baada ya kifo cha Yesu tumehimizwa zaidi kusaidia maskini na mtu mwingine yeyote mwenye uhitaji. Hakuna sehemu imetajwa fungu la 10. Hili suala la fungu la 10 linatumika na wachungaji matapeli kuvuna pesa bila jasho kutoka kwa waumini wajinga. Biblia imesisitiza mara nyingi sana kusaidia wasiojiweza. Hata fungu la 10 la enzi za Musa lilikuwa kuwasaidia walawi ambao hawakuwa na kazi nyingine zaidi ya ile ya kiroho. Hawa wachungaji wanaomiliki biashara mjini hakuna haja ya kuwachangi chochote. Soma zaidi mafungu yafuatayo ujue zaidi kuhusu utoaji. Mathayo 10:8, Mithali 3:27, Luka 6:38, Yakobo 2:15-17, Mithali 11:24-25, Kumbukumbu la torati 15:11, Mithali 3:9 - 10, Mathayo 25:40
Hicho unachokitoa ndiyo baraka yako, yaani unatoa sadaka ya mkate ili upate baraka yq mkate, what a waste!Wewe toa tu hakuna unachopoteza, acha ligi, unapishana na baraka bila sababu yoyote
Peleka kwa watoto yatimaE bwana eeh usinambie...nina 110k hapa toka asubuh nawaza sijui niipeleke au??
Yaani wanaboa kweli maana wengine wanashindwa kujificha vizuri hadi kupelekea kuwapangia kiasi cha kutoa waumini wao kwangu sasa mwendo mbele hakuna kuwapa kitu hawaKwa sasa kumekuwa na msisitizo mkubwa mno makanisani watu kutoa pesa inayotajwa kama fungu la 10 (zaka) kiasi kwamba imegeuka kero kubwa kwenye jamii. Wanawake wamekuwa wahanga wa kuchotwa akili zao na kujikuta wanatoa hadi pesa za kujikimu na kuingiza familia kwenye matatizo yasiyo ya lazima. Sasa mimi leo natamka hadharani kuwa ACHA KUTOA FUNGU LA 10 KWA SABABU NI UTAPELI. Soma huu uzi bila hisia ili uelewe.
Kwanza ni lazima tujue historia fupi kuhusu fungu la 10 ni kwanini na wapi lilikuwa linatolewa? Historia inaonyesha Fungu la 10 lilikuwepo zamani enzi za Abrahamu ila likawa sheria kamili enzi za Musa. Abrahamu alitoa fungu la 10 kama zawadi kwa Mfalme na kuhani wa Salemu. Soma Mwanzo 14:18-20 ingawa haitajwi tena kama Abrahamu alishawahi toa tena fungu la 10. Pia Yakobo alitoa ahadi kwa Mungu kuwa atatoa fungu la 10 endapo Mungu angembariki. Mwanzo 28:20-22
Enzi za Musa ndo kukawepo na sheria kuwa kutoa fungu la 10 ni lazima. "Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka". Kumbukumbu la torati 14:22
Tukirudi nyuma kidogo tutaona waisrael wakiwa jangwani walikuwa wakiabudu kwenye kilichoitwa HEMA YA KUKUTANIA. Na kwa wakati huo Mungu alimteua Haruni kuwa kuhani mkuu huku wana wa Lawi wakiwa wafanyakazi kwenye hema la kukutania. Katika hao wana wa Lawi kulikuwa na wafanyakazi wasio makuhani na wale makuhani. Haruni na walawi hawakupaswa kufanya kazi nyingine yoyote zaidi ya zinazohusu dini yao. Walikuwa wanafanya kazi kanisani. Kutokana na hilo ndo ikabidi uwepo utaratibu ili na wao waishi bila shida.
Basi ndo sheria ikawepo ya wana wa Israel kutoa fungu la 10 kwenye mavuno yao na mifugo kuwapatia walawi waliokuwa wanafanya kazi za kiroho. Na walawi wakishapokea hizo zaka na sadaka basi kwa wale walawi wasio makuhani hutoa fungu la 10 ya vile walivyopokea na kuwapatia makuhani. Soma Hesabu 18. Pia fungu la 10 lilikuwa likitolewa kwa wale maskini wasio na uwezo kila baada ya miaka mitatu (Kumbukumbu la torati 14:28-29). Kimsingi hakuna zaka wala sadaka ambayo huenda kwa Mungu moja kwa moja. Mungu aliweka tu utaratibu ili wale waliokuwa wanafanya kazi za kiroho nao waishi. Ila Mungu hajawahi kuwa na dhiki ya kutaka tumpe hela.
Tukisoma Wakolosai 2:13-14 tunaona kuwa mara baada ya kifo cha Yesu hizi sheria za Musa hazikuendelea kutumika tena. Na pia ikasisitizwa mtu asije kukuhukumu kupitia sheria za Musa. Wakolosai 2:16 "Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;"
Sasa kama Zaka na sadaka sio lazima, nini kinatakiwa kutolewa kanisani? Jibu lipo kwenye 2 Wakorintho 9:6-12. Biblia imemtaka kila muumini atoe tu mchango wa fedha kanisani kwa ajili ya kuwezesha huduma ila sio lazima. 2 Wakorintho 9:7 "Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu". Na pia biblia haijataja kuwa ni dhambi kutokutoa. Mungu anataka utoe kwa moyo wako na sio kujilazimisha.
Kutoa fedha kanisani ni jambo lenye baraka nyingi ili kuwezesha huduma. Hiyo ni ahadi ya Mungu kupitia Malaki 3:10 "Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la". Lakini pia Mungu ametutaka tunapotoa iwe siri. Mathayo 6:3-4 "Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi".
Kwenye suala zima la utoaji mara baada ya kifo cha Yesu tumehimizwa zaidi kusaidia maskini na mtu mwingine yeyote mwenye uhitaji. Hakuna sehemu imetajwa fungu la 10. Hili suala la fungu la 10 linatumika na wachungaji matapeli kuvuna pesa bila jasho kutoka kwa waumini wajinga. Biblia imesisitiza mara nyingi sana kusaidia wasiojiweza. Hata fungu la 10 la enzi za Musa lilikuwa kuwasaidia walawi ambao hawakuwa na kazi nyingine zaidi ya ile ya kiroho. Hawa wachungaji wanaomiliki biashara mjini hakuna haja ya kuwachangi chochote. Soma zaidi mafungu yafuatayo ujue zaidi kuhusu utoaji. Mathayo 10:8, Mithali 3:27, Luka 6:38, Yakobo 2:15-17, Mithali 11:24-25, Kumbukumbu la torati 15:11, Mithali 3:9 - 10, Mathayo 25:40
Huko nako mbona wamejaa wapigaji tu hamna kituPeleka kwa watoto yatima