Fungu la 10 ni kitu ambacho hakipo kwa sasa kwa mujibu wa biblia na ni kujiumiza bila sababu kuendelea kutoa

Zipo silaha kubwa zaidi ya Saba za kumshinda shetani sadaka ni moja ya silaha hizo.
Hakuna silaha ya kumshinda shetani zaidi ya kufuata amri 10 za Mungu. Na katika hizo amri hakuna inayosema tutoe fungu la 10. Kuacha dhambi ndo namna pekee ya kumshinda shetani na sio janjajanja zingine. Kwenye hizo janjajanja shetani yuko mbele sana ya muda. Wakati wewe unampiga na silaha ya fungu la 10 yeye anakusogezea demu mwenye tako la dunia nzima ili unase..
 
Amri 10 zipo ndani ya silaha hizo,kushobokea tako means wewe bado mchanga kiroho
 
Kuna watu Hela Huwa zinawawasha au zimesha wakinai. Nje na fungu la kumi huwezi toa Hela Yako ununue mchanga wa Israel kutwa wanamwaga damu za watu heri uchukue udogo wa hapahapa Bongo
 
Ni kweli ila nimeandika makusudi kusaidia wapumbavu wanaoteswa na hawa wachungaji matapeli. Kuna ndoa zinapitia wakati mgumu sababu ikiwa manabii na wachungaji feki wanaowakomba hela zao.
Mama mdogo wangu alifariki mwaka jana, ukoo mzima tulikuwa na huzuni lakini baba mdogo alisema hivi "afadhali mke wangu amekufa, hapa sasa nitaishi kwa amani na wanangu" aise tulishangaa sana! Baada ya kumuuliza alituambia kuwa zaidi ya 200M za kwenye biashara zake KKOO ziliishia kanisani kwa mke wake! Alikuwa anashinda kwenye makanisa ya kiroho muda mwingi, na kila asubuhi anabeba kitita anasema ni sadaka! Hii ilimchosha baba mdogo kiasi kwamba alifurahia kifo cha mkewe!

Kwahiyo OP ulichoeleza nakubaliana na wewe kabisa, ni vyema tutoe sadaka kawaida ila sio zile sadaka za KUPANGIWA na watumishi.
 
Baba mdogo aliteseka sana itakuwa. Watumishi ni washenzi.
 
Mkristo halazimishwi kutoa fungu la kumi kwa sababu hayuko chini ya sheria bali katika neema ya Yesu Kristo.

Correction; Zaka sio kwamba walikua wanapeleka kanisani. Walawi walikua wanazipokea tu ila ilikua wanakula na kunywa zaka zao πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… sehemu ambayo BWANA ameichagua.

Ila mwaka wa tatu zaka unakula wewe na watu wa nyumba yako hapo ulipo ukiwakaribisha walawi, wahitaji.
(Reference Deut 12: 12-18, Deut 14: 26)

Makuhani walikua wanachukua 1 ya 10 sio zaka yote.

Kanuni ya utoaji kwa mkristo ni kutoa kwa moyo wa kupenda 2 Wakor 9:7
 
Yaani wanaboa kweli maana wengine wanashindwa kujificha vizuri hadi kupelekea kuwapangia kiasi cha kutoa waumini wao kwangu sasa mwendo mbele hakuna kuwapa kitu hawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…