Fungus ambao wananisumbua mwaka wa pili sasa, nimemaliza hela nyingi na nimetumia dawa nyingi sana ila sijapona

Fungus ambao wananisumbua mwaka wa pili sasa, nimemaliza hela nyingi na nimetumia dawa nyingi sana ila sijapona

Twalib Jr

Member
Joined
Jul 23, 2020
Posts
20
Reaction score
3
Habari zenu waungwana,

Jamani eh! Nina tatizo naomba someni uzi wangu mpaka mwisho na mnisaidie naomba mnisaidie tafadhali.

Nilikuja hapa kuomba ushauri miezi kadhaa nyuma kwa tatizo langu la {fungus} nilipewa ushauri na nikaufuata vyema na baadhi ya vitu ambavyo niliambiwa nitumie ila bado sijapona na tatizo limeongezeka.

Naomba nieleze vyema leo ninavyosumbuliwa ili mwenye kunisaidia anisaidie.

Ni hivi;

Nina fungus ambao hapo mwanzo walianza kutoa vipele vyenye maji maji na nikaenda kuchoma {powercef} nikapona, wakarudi tena nikatumia {azuma} nikapona, wakarudi mara ya tatu sasa hapa vilitoka vilengelenge na si chunusi tena, nikaona niende hospitali maana likaja na tatizo jingine ambapo ili njia ya mkojo inachoma choma na mishipa ya uume inavuta si kawaida.

Nilivyoenda Mwananyamala nikafanya vipimo vyote vya zinaa sikukutwa na tatizo nikaambiwa nifanye {culture} pia majibu yakawa hakuna mdudu aliyeota, nikapewa transfer ya Muhimbili nako nikafanya vipimo vikubwa nikaambiwa hakuna tatizo hivyo nikapewa dawa za kupaka kwa ajili ya {fungus} na ya lile tatizo la kuvuta na kuchoma choma katika njia ya mkojo nikatumia sikupona.

Hapo sasa ndio vikaanza kutoka vichunusi na vilengelenge, kuna dispensary moja nikaenda kuchoma sindano ya {alergy} na ya kuuwa vile vipele haikufanikiwa na hapo nikaanza kuona uchafu unatoka wa mfano wa shahawa na nikaanza kutoka na vipele mikononi ambavyo vinawasha sana na baadae hali kurudi kama kawaida katika sehemu za siri.

Na sasa hivi korodani zina washa, uume wenyewe unawasha na una vipele vidogo vidogo, mwili mzima unatoka vipele kimoja kimoja vyenye maji maji ambavyo ukikuna huwasha na hutoa maji maji, nawashwaa jamani nawashwaa haswaaaa nisaidie hili tatizo nimemaliza hela nyingi na nimetumia dawa nyingi sana ila sijapona.

Namba zangu ni +255686978566 au +255692224990

Naombeni msaada wenu

Na hizi ndio chunusi zinazo nisumbua zipo muundo huo.

1610700473901-287201505.jpg
 
Pole sana Twalib, Je, vipi ulishawahi kumla mke au mtoto wa shekhe?

Kama hospital wanasema hakuna ipo namna ya kutafuta history ya matukio yako na maadui zako. Waombe msamaha yataisha tu.
 
Jaribu kutibu scabies. Watu wengi huwa hawafikirii hili tatizo lakini linasumbua sana. Tafuta lotion ya BBE na ogea sabuni ya Tetmosol.
 
Pole sana! Huenda ukawa ugonjwa mpya umeanzia kwako! Tiba zitazalishwa kuanzia kwako!
Anyway!
Jaribu kuangalia MCHAFUKO WA DAMU!
Usihangaike na ngozi! Huenda tatizo liko ndani! Check damu
 
Ukiona 'fungikuvu' wamekuganda sana ujue wewe ni mtamu kwao, jivunie kuwa wanakupenda na wanafurahia kukutafuna.

Haya maisha tu![emoji1493][emoji1493][emoji1493]
 
Pole sana! Huenda ukawa ugonjwa mpya umeanzia kwako! Tiba zitazalishwa kuanzia kwako!
Anyway!
Jaribu kuangalia MCHAFUKO WA DAMU!
Usihangaike na ngozi! Huenda tatizo liko ndani! Check damu
Unarudia alichoeleza kuwa kapitia!
 
Pole sana twalib, Je, vip ulishawahi kumla mke au mtoto wa shekhe?

Kama hospital wanasema hakuna ipo namna ya kutafuta history ya matukio yako na maadui zako. Waombe msamaha yataisha tu.
Kiasi kikubwa naona umesem kitu flani kiko sahihi so kwa hilo ajaribu kurud nyuma ajue ukweli huenda historia ikamsaidia au aende kwa maombi
 
Umefanya kipimo cha FBP hivi karibuni?

Kama hutojali, naomba u-upload katika uzi huu.
 
Back
Top Bottom