Fungus ambao wananisumbua mwaka wa pili sasa, nimemaliza hela nyingi na nimetumia dawa nyingi sana ila sijapona

Fungus ambao wananisumbua mwaka wa pili sasa, nimemaliza hela nyingi na nimetumia dawa nyingi sana ila sijapona

Pole Mkuu kama umepima Damu Full blood picture na hakuna maradhi yailiyo onekana basi utakuwa una maradhi ya kichawi umefanyiwa uchawi na maaduwi zako kwa dawa za hospitali huwezi kupona kwa dawa za asili unaweza kupona uguwa pole.

Mzee wa porojo!
 
Jaribu kutibu scabies. Watu wengi huwa hawafikirii hili tatizo lakini linasumbua sana. Tafuta lotion ya BBE na ogea sabuni ya Tetmosol.
Naomba kujua ubora wa hiyo sabuni ya tetmosol mkuu
 
Naomba nikuulize kitu kama hautojali.

Ikifika jioni unakua unawashwa sana mpk kwenye Miguu na mda mwingine unakua kama unavimba?

Vipele vyako vimetokea kwenye Uume nivikubwa vinakua kama vinakuwasha vinaitaji ukune mda wote?

Kama ndio basi naomba nikuelekeze uende pale Posta kituo cha mwendo kasi Halmashauri ya jiji au Laptop city uende Bulhan hospital omba kukutana na daktari wa ngozi.

Uo ni ukurutu ni ugonjwa ulionisumbua kwa muda kidogo 2019 now nimepona kabisa na unaambukiza maana nyumba nzima nakumbuka walikua nao tukapata dozi wote.

Zingatia ufuaji wa Matandiko ya kulalia kwa wakati, kufua boxer kila baada ya siku 1 au 2 , tumia maji masafi yasiyo na wadudu muda wote kuogea na kunawa pia.

Zingatia usafi wa mwili namaanisha kuoga angalau mara 2-3 kwa siku.

Tumia dawa ya scaboma kupaka mwili wako kila wiki( siku moja ya wiki) kila utokapo kuoga kwa muda wa mwezi mzima ( inauzwa 8000/= Tsh)

Kuna vidonge jina sivijui ila nina picha unapewa dozi nzima inabidi umeze kila siku kimoja usiku kwa mwezi mzima ukianza meza ivi vidonge utaona mabadiliko ndani ya siku 2-3 vipele vya kwenye uume vitaanza kauka na kusinyaa( nakutumia picha ya vidonge chini uende kubitafuta duka la madawa au phamacy kubwa)

NB: MUONE DAKTARI KWA USHAURI ZAIDI
View attachment 1678024
Na mimi nimeipata hii kitu sasa hivi..

Nilikua dar es salaam kama wiki tatu zilizopita .. mwishoni kwenye tarehe 13-15 january maji yakawa ya shida ikabidi niogee maju ya kwenye kisima (wenyeji hua wanasema ni macahfu wao hutumia chooni na kufulia)..

Sasa nimekuja mkoani nashangaa usiku mwili unawasha sana,, na pia ivyo vipele vimenitokea kidogo baadhi ya sehemu za mwili..

Na hata kwenye uume ndo vimetokea vikubwa kiasi(kama malengelenge)...
 
Habari zenu waungwana,

Jamani eh! Nina tatizo naomba someni uzi wangu mpaka mwisho na mnisaidie naomba mnisaidie tafadhali.

Nilikuja hapa kuomba ushauri miezi kadhaa nyuma kwa tatizo langu la {fungus} nilipewa ushauri na nikaufuata vyema na baadhi ya vitu ambavyo niliambiwa nitumie ila bado sijapona na tatizo limeongezeka.

Naomba nieleze vyema leo ninavyosumbuliwa ili mwenye kunisaidia anisaidie.

Ni hivi;

Nina fungus ambao hapo mwanzo walianza kutoa vipele vyenye maji maji na nikaenda kuchoma {powercef} nikapona, wakarudi tena nikatumia {azuma} nikapona, wakarudi mara ya tatu sasa hapa vilitoka vilengelenge na si chunusi tena, nikaona niende hospitali maana likaja na tatizo jingine ambapo ili njia ya mkojo inachoma choma na mishipa ya uume inavuta si kawaida.

Nilivyoenda Mwananyamala nikafanya vipimo vyote vya zinaa sikukutwa na tatizo nikaambiwa nifanye {culture} pia majibu yakawa hakuna mdudu aliyeota, nikapewa transfer ya Muhimbili nako nikafanya vipimo vikubwa nikaambiwa hakuna tatizo hivyo nikapewa dawa za kupaka kwa ajili ya {fungus} na ya lile tatizo la kuvuta na kuchoma choma katika njia ya mkojo nikatumia sikupona.

Hapo sasa ndio vikaanza kutoka vichunusi na vilengelenge, kuna dispensary moja nikaenda kuchoma sindano ya {alergy} na ya kuuwa vile vipele haikufanikiwa na hapo nikaanza kuona uchafu unatoka wa mfano wa shahawa na nikaanza kutoka na vipele mikononi ambavyo vinawasha sana na baadae hali kurudi kama kawaida katika sehemu za siri.

Na sasa hivi korodani zina washa, uume wenyewe unawasha na una vipele vidogo vidogo, mwili mzima unatoka vipele kimoja kimoja vyenye maji maji ambavyo ukikuna huwasha na hutoa maji maji, nawashwaa jamani nawashwaa haswaaaa nisaidie hili tatizo nimemaliza hela nyingi na nimetumia dawa nyingi sana ila sijapona.

Namba zangu ni +255686978566 au +255692224990

Naombeni msaada wenu

Na hizi ndio chunusi zinazo nisumbua zipo muundo huo.

View attachment 1677961
Kaka naomba mrejesho
 
Hii iliwah nitokea nami..... nilikua ninawashwa mikono ...makwapa mpka mboo na inatoa tuvipele hospital nikienda kupima stds wapi......

Kuna mmama mmoja ni doctor mstaaf nilimwelezea akaniambia vuta kumbukumbu nani ume sex nae mala ya mwisho ndo ugonjwa ukaanza...

Bas nikakumbuka bint mmoja hiv chibongeee .....doctor akaniambia sio kwa ubaya lakin ....kama umepima na ukuwa na ugonjwa wowote..yule mwanamke ana..acid nyingi yawezekana pia zimekuingia mwilin wapo watu wa dizain hii.


Solution pata mlo kamili ..matunda maji mengi.... chakula cha proton nyingi ....zidisha usafi wa mwili vaa boxsa za cotton pana ..na usiludie boxsa pind uvaapo... na zianike Juan...ukifua.,

Mafuta ya kupaka tumia ya nazi hasa parachute ndio mazur zaid ..... sabun tumia za kawaida kwa sasa kama kipande maana bacteria washakua sugu ndan nje ....

Lakin kubwa zaid kiroho ...kila ukioga changanya maji na chumvi ya mawe mwez mzima ..... afu lud na majib
Tatzo la ngoz nilishalisahau muda tu mwilin mwangu.
 
Jaribu kutibu scabies. Watu wengi huwa hawafikirii hili tatizo lakini linasumbua sana. Tafuta lotion ya BBE na ogea sabuni ya Tetmosol.
Lindane ( Scaboma Lotion ) ilinisaidia sana kutibu Scabies, ila anatakiwa ajirizishe kuwa ni Scabies kwa sababu Iyo Lotion ina takiwa iwe ni last option ikiwa njia zote zimeshindikana.
Kama sio Scabies ,
Tumia Bicarbonate of Soda hiyo kama unasumbuliwa na Miwasho sehemu za siri

Chukua kijiko kimoja cha bicarnonate of soda, tia kwenye lita moja au mbili za maji kisha osha maeneo yenye muwasho walau asubuhi na usiku au kila unapotoka haja

Vaa nguo za ndani (cotton) pia pendelea kuwa mkavu maeneo ya sehemu nyeti maana uwepo wa unyevuvyevu sehemu za siri husababisha fangasi / bakteria kupata mazingira ya kukua na kuzaliana kwa wingi.

Kumbuka,

Ili uepuke hizi kero, ni vyema kwanza ujitahidi kuwa mtu wa kunywa maji walau lita moja kila siku

.....kunywa maji inakusaidia kukojoa na kuwaondoa idadi kubwa ya bakteria au fangasi kupitia mkojo.
Nimepata Fb ktk page ya Asili yetu Africa.
 

Attachments

  • FB_IMG_1732684520179.jpg
    FB_IMG_1732684520179.jpg
    35 KB · Views: 3
Back
Top Bottom